Monday, 3 October 2016

TAFAKARI: Jumatatu, Oktoba 3, 2016. Juma la 27 la Mwaka- C.


TAFAKARI
     Jumatatu, Oktoba 3, 2016.
   Juma la 27 la Mwaka

 
       Gal 1: 6-12
       Zab 111: 1-2, 7-10
             Lk 10: 27-37

         “KATIKA JIONI YA MAISHA YAKO UTACHUNGUZWA TU JUU YA UPENDO” (Mt. Yohane wa Msalaba)
             Leo katika Injili mwalimu wa sheria anamuuliza Yesu swali ambalo, sisi tungeweza kujiuliza katika maisha yetu ya kila siku. “Bwana, nifanye nini niurithi Ufalme wa milele?” (Lk 10: 25). Yesu, lakini, tena katika hekima anajibu kwa yale yalioandikwa katika Maandiko: ‘kumpenda Bwana Mungu wako na jirani yako kama nafsi yako’ (rej. Lk 10: 27). Kupenda maana yake ni kujitoa kwa wengine kwa yote tulio nayo na yote jinsi tulivyo. 
     Kujitoa kusikiliza wengine kujitoa kuelewa wengine na kuwa na subira kwa ajili ya wengine. Huo ndio upendo. 
   Upendo huu unakuwa na asili ya Kimungu tunapo ueneza zaidi kwa wale walio tuumiza katika maisha au kwa wengine tusio waona hata macho kwa macho. Upendo unakuwa na Mguso wa Kimungu tunapo toka njee kwenda kuwasaidia hata watu tusio wafahamu. ‘Kama mtu mmoja anateseka, watu wote wanateseka naye, kama mmoja anaheshimiwa, watu wote wanashiriki katika furaha yake’ (1 Cor 12: 26). 
  Hii ndio fadhila ya Msamaria Mwema. 
      Sala: Bwana naomba nisitoe kisingizio chochote kwenye amri ya “Mpende jirani yako kama nafsi yako”. Amina

Copyright © 2016 by shajara and published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
      see: imani-katoliki.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

"Asante sana kwa maoni yako"

NYIMBO ZA DOMINIKA YA 29 YA MWAKA- C WA KANISA.

Nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka C Karibu kwa ajili ya nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka "C" Mwanzo: Ee Bwana Nimekuita  ...