Karibu tujuzane juu ya watakatifu katika ukurasa huu.
==================================MATAKATIFU WA LEO,3/9/2016.
>Mt.Gregori Mkuu. Baba Mtakatifu na Mwalimu wa kanisa.
==================================
MTAKATIFU WA LEO,9/9/2016.
> Mt.Petro Kleveri, Padri.
==================================
MTAKATIFU WA LEO
*Leo kanisa linamkumbuka mtakatifu Peter Wa Alcantara Padre*
Mtakatifu Peter,alizaliwa mwaka 1499, huko Alcantara ,Hispania.Baba yake alikuwa gavana wa jimbo, na mama yake alitoka katika familia njema.
Mtakatifu Peter,alianza kufundishwa na walimu akiwa nyumbani.Baadae alijiunga na chuo kikuu cha Salamanca.Alijiunga na Wa Franciscan mwaka 1515 huko Manxaretes Extramadura,Hispania.Akiwa na miaka 22 aliagizwa kwenda katika mji wa Badajoz,kuanzisha tawi jingine la Wafranciscan. Mwaka 1524 alipata daraja la Upadre,na mwaka 1525 akawa msimamizi wa shirika huko Robredillo,Old Castile.Mwaka 1538, alichaguliwa kuwa mkuu wa kanda ya my Gabriel.Akataka kurekebisha sheria,lakini hakufanikiwa.Hivyo aliamua kujiuzulu.Akaamua kuanza kuwahubiria watu maskini.Aliwafundisha mambo mengi,akikazia uvumilivu..Mwaka 1553-1555 aliamua kukaa peke yake,akisali,akifunga na kuomba.Aliamua pia kwenda Roma kuhiji, ambapo alitembea mwendo wote bila viatu.Akiwa huko aliomba kibali cha Papa Julius III,kuanzisha vituo vya watawa.Alikubaliwa.Akiwa njiani kurudi,aliweza kuanzisha vituo kadhaa,ambavyo vilikuwa na sheria kali kidogo.
Alipokaribia kufa,alipiga magoti,akasali.Alipopewa Maji ya kunywa alikataa,akisema ``hata Bwana Yesu alisikia kiu msalabani``. Mtakatifu Peter alikufa akisali October 18 1562.
Mwaka 1622 April 16 Papa Gregory XV alimtangaza mwenye heri .Mwaka 1669,April 28 Papa Clement IX alimtangaza kuwa mtakatifu.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Faustina Kowalska
Bl. Alberto Marvelli
Mt. Alexander
Mt. Anna Schaeffer
Mt. Apollinaris
Mt. Attilanus
Mt. Aymard
Bl. Bartholomew Longo
Mt. Boniface
Mt. Charitina
Wt. Firmatus na Flaviana
Mt. Flora
Bl. Francis Xavier Seelos
Mt. Galla
Mt. Magdalevus
Mt. Meinuph
Mt. Palmatius
Mt. Placid
Bl. Raymond wa Capua
Bl. Robert Sutton
Mt. Thraseas
Bl. William Hartley
==================================
MTAKATIFU WA LEO
*Leo kanisa linamkumbuka mtakatifu Bruno Padri*
Mtakatifu Bruno alizaliwa huko Cologne katika familia maarufu.Alisoma katika shule ya Cathedral ya Rheims,na akarudi Cologne mwaka 1055.Akapata daraja la upadri na akawa paroko wa parokia ya Mtakatifu Cunibert.Akarudi tena Rheims mwaka 1056,akiwa profesa wa teologia.Akawa mkuu wa chuo pale Rheims.Mwaka 1076 mt Bruno na mapadri wengine walikimbia kutoka Rheims baada ya kutangaza kuwa Askofu Manasses hakufaa kuwa mwakilishi wa papa pale jimboni.Mt Bruno alirudi tena Cologne mwaka 1080, baada ya Askofu huyo kuondoka.Watu wa Rheims walitaka awe Askofu wao.Lakini alikataa na akaenda kuishi maisha ya upweke na mt Robert wa Molesmes.Hata hivyo baadae aliondoka na kwenda Grenoble,yeye na wenzake 6.Baadae tena walikwenda kuishi katika eneo la milima la Le Grande Chartreuse, chini ya Askofu Hugh,wakifuata sheria za Wa Benedictine.Hapo ukawa mwanzo wa shirika la Carthusian.Hao waliishi maisha ya kimaskini,wakifanya kazi na kusali.Shirika lilisambaa sehemu kubwa.Mwaka 1090 mt Bruno aliitwa na Papa Urban huko Roma.Akapewa kazi ya kuwa mshauri wa Papa. Mt Bruno alimuomba Papa ,amruhusu abaki alikokuwa ili kuendeleza shirika.Papa akataka awe Askofu wa Reggio,huko Italia.Mtakatifu Bruno pia akakataa.Akawa rafiki wa mtawala wa Sicily aliyeitwa Robert.Akakaa huko mpaka alipokufa Mwezi Octoba 6 1101 ,huko Serra San Bruno,Italia.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Bl. Adalbero
Mt. Aurea
Mt. Ceollach
Bl. Diego Luis de San Vitores
Mt. Epiphania wa Pavia
Mt. Erotis
Mt. Faith
Mt. Faith
Mt. Francis Trung
Bl. Isidore wa mt Joseph
Mt. Magnus
Mt. Mary Frances
Bl. Marie Rose Durocher
Mashahidi wa Trier
Mt. Nicetas
Mt. Pardulphus
Mt. Sagar
==================================
MTAKATIFU WA SIKU YA LEO 7/10/2016
*Mama Bikira Maria wa Rozari takatifu*
Mwaka 1571, mtakatifu Papa Pius V,aliandaa jeshi kutoka Hispania na kutoka katika falme ndogondogo za kikristu,na askari waliojitolea kwenda kuipigania nchi ya Cyprus.Nchi hiyo ya kikristu,ilikuwa katika hatari ya kutekwa na majeshi ya waarabu.
Oktoba 7,mwaka 1571 majeshi ya muungano ya kikristu ,yaliondoka katika Bandari ya mji wa Messina, Sicily kwenda kupambana na majeshi yenye nguvu ya waarabu huko Lepanto.Baba mtakatifu,Papa Pius V ,akijua nguvu ndogo ya jeshi la wakristu, aliomba wakristu wote Ulaya ,kusali Rozari ili kupata ushindi.Yeye mwenyewe alianzisha Rozari Roma.
Baada ya Masaa 5 ya mapigano makali, katika ghuba ya Corinth,Ugiriki,majeshi yaliyokuwa chini ya Papa,yalimudu kuzuia majeshi ya waarabu kusonga mbele.Majeshi majeshi yaliyokuwa chini ya Papa,yaliwazuia waarabu kuisogelea bahari ya Atlantic, ambayo ilikuwa mlango wa kuingilia Ulaya.Hiyo ingekuwa fursa kwa waarabu kuishambulia Roma pia.
Papa Pius V aliitangaza Siku hiyo kuwa ni ya Mama yetu wa Ushindi.Mwaka 1573,Papa Gregory XIII,aliibadili Siku hiyo kuwa siku ya Rozari takatifu.Mwaka 1960, Papa John XXIII,aliibadilisha tena Siku hiyo na kuiita *Siku ya Mama yetu wa Rozari takatifu.*
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Artaldus
Mt. Adalgis
Mt. Apuleius
Mt. Augustus
Mt. Canog
Mt. Dubtach
Mt. Helanus
Mt. Justina wa Padua
Mt Pope Mark
Mt. Osyth
Mt. Palladius
Wt. Sergius na Bacehus
SMt. Sergius
==================================
*Leo Kanisa linamkumbuka mtakatifu Wilfrid Askofu*
Mtakatifu Wilfrid alizaliwa Northumberland, Uingereza mwaka 634.Akasoma huko Lindesfarne ,na akaishi pia huko Lyons ,Ufaransa na Roma Italia.Mwaka 658 alichaguliwa kuwa Abati Wa Ripon,akaanzisha taratibu zilizofuatwa Roma huko kaskazini mwa Uingereza.Mwaka 664 alichaguliwa kuwa Askofu wa York,na kutokana na matatizo mbalimbali,alianza kazi hiyo mwaka 669.Akaanza kwa kuanzisha seminari nyingi za Wabenedictine.Akalazimika pia kwenda Roma kuzuia mgawanyo wa jimbo lake ambao ungefanywa na mtakatifu Theodere,Askofu wa Canterbury. Wakati akisubiri maamuzi, aliamua kuhamia kusini ya Saxon ,kuinjilisha huko mpaka mwaka 686 alipoitwa tena.Mwaka 691 alienda tena kuhubiri sehemu nyingine ndani ya Uingereza .Mwaka 703, alijiuzuru nafasi yake ambapo alirudi katika seminari ya Ripon,mpaka alipokufa mwaka 709.
*Watakatifu wengine wa leo ni*
Mt. Amicus
Bl. Camillus Constanzi
Mt. Cosmas of Maiuma
Mt. Domnina wa Anazarbus
Mt. Edistius
Mt. Edwin wa Northumbria
Mt. Eustace
Mt. Evagrius
Wt. Felix na Cyprian
Mt. Fiace
Mt. Heribert wa Cologne
Bl. Maria Teresa Fasce
Mt. Maximilian wa Lorch
Mt. Monas
Mt. Pantalus
Mt. Salvinus
Mt. Seraphinus

No comments:
Post a Comment
"Asante sana kwa maoni yako"