KUMBUKUMBU YA MT. TERESIA WA AVILA, BIKIRA NA MWALIMU WA KANISA
SOMO LA 1
Efe 1:15-23
Tangu nilipopata habari za Imani yenu katika bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote, siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu, Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu awape ninyi roho wa hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, tumjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo ;na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo.
Kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake;ulipotenda katika kristo alipomfufua katika wafu,akamwekea mkono wake wa kuume katika ulimwngu wa roho ; juu sana katika ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani na kila jina litajwalo wala si ulimwenguni humu tu bali katika ule ujao pia akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.
Neno la Mungu ...... Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab 8:1-6
(1). Wewe Mungu Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni; Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao.
(K) Umemtawaza mwanao juu ya kazi za mikono yako
(2). Nikiziangalia mbingu zako, Kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha, Mtu ni kitu gani hat umkumbuke Na binadamu hata umwangalie.
(K) Umemtawaza mwanao juu ya kazi za mikono yako
(3). Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
(K) Umemtawaza mwanao juu ya kazi za mikono yako
SHANGILIO
Mt 11:35
Aleluya, Aleluya Nakushukuru baba Bwana wa mbingu na nchi Kwa kuwa mambo haya uliyaficha Wenye hekima na akili Ukawafunulia watoto wachanga Aleluya.
SOMO LA INJILI
Lk 12:8-12
Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Nami nawaambia, kila atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu; na mwenye kunikana mbele ya watu, huyo atakanwa mbele ya malaika wa Mungu. Na kila mtu atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali aliyemkufura Roho Mtakatifu hatasamehewa. Na watakapowapeleka ninyi mbele ya masinagogi na maliwali na wenye mamlaka, msifadhaike kwa kuwaza maneno yenu jinsi mtakavyojibu au kusema; kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema.
Neno la Bwana...... Sifa Kwako Ee kristu.
Copyright © 2016 shajara and published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
see: imani-katoliki.blogspot.com
No comments:
Post a Comment
"Asante sana kwa maoni yako"