Thursday, 13 October 2016

TAFAKARI: Alhamisi, Oktoba 13, 2016, Juma la 28 la Mwaka -C wa Kanisa. " thinking Capacity "


TAFAKARI

       Alhamisi, Oktoba 13, 2016,
   Juma la 28 la Mwaka wa Kanisa
        Ef 1:1-10;
     Zab 97:1-6;
           Lk 11:47-54

            JE TUNA UPANA WA AKILI KATIKA MAISHA YETU?
           Injili ya leo inaongelea kuhusu kutokuelewana kati ya Yesu na viongozi wa dini wa wakati huo. Walimu washeria walimwelezea Mungu kama hakimu mkali sana na wakaweka sheria na miiko ambazo hazikuwa na ushusiano kabisa na amri za Mungu.
Wao kwa njia ya mafundisho ya uongo waliwahukumu na kuwaua Manabii, na baadaye walitengeneza makaburi kwa heshima yao.
Leo Yesu anawanyoshea kidole, kwamba wanajizuia wenyewe nakujiwia mizigo katika kuingia Ufalme wa Mungu na pia kuua hamu ya wengine ya kumtumikia Mungu.
Swali ambalo tunaweza kujiuliza wenyewe:
              • Je, tuna sura ya uongo ya Mungu na tunajaribu kuiweka kwa wengine?
        
              • Je, tuna upana mdogo wa uwelewa kama Waandishi ambao waliwapinga wengine kwasababu tu, wanafikiri tofauti na kutenda tofauti?

               Sala: Bwana, naomba utupilie mbali mawazo yote mabaya na mitazamo yote mibaya inayonizuia kujikabidhi kwangu kwako, mimi na jirani yangu, nisaidie niweze kuwa na upana wa akili katika kukuelewa wewe katika jamii na jumuiya yangu. Amina


Copyright © 2016 Shajara  and published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
   see: imani-katoliki.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

"Asante sana kwa maoni yako"

NYIMBO ZA DOMINIKA YA 29 YA MWAKA- C WA KANISA.

Nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka C Karibu kwa ajili ya nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka "C" Mwanzo: Ee Bwana Nimekuita  ...