Friday, 7 October 2016

TAFAKARI: 7/10/2016 Juma la 27 la Mwaka-C wa kanisa. Kumbukumbu ya Bikira Maria wa Rozari.


Ijumaa, Oktoba 7, 2016,
Juma la 27 la Mwaka wa Kanisa
      Kumbukumbu ya Bikira Maria wa Rozari
            Gal 3:7-14
        Zab 111:1-6 (K) 5
              Lk. 11:15-26

           ROZARI: TAFAKARI NA SALA ILIOJIKITA KATIKA KRISTO !
         Wengi wetu tunasali rozari wenyewe, katika jumuiya au katika familia lakini huenda mara nyingi hatujui maana yake na umuhimu wake. Mt. Papa Yohane Paulo wa pili katika barua yake ya Kitume “Rozari ya Bikira Maria” anasema “Rozari, ingawaje ina tabia ya Maria, katika moyo wake ni sala iliojikita katika Kristo. 
Ina kina cha ujumbe wa Injili katika hali yake yote. Ina sauti ya Maria, wimbo wake wa daima kwa kazi ya ukombozi-umwilisho ilioanza ndani ya tumbo lake…..”. Kielelezo cha Rosari ni juu ya Yesu-kuzaliwa kwake, maisha yake, kifo na ufufuko. Sala ya ‘Baba Yetu’ inatukumbusha kwamba Baba yake Yesu ndiye chanzo cha Ukombozi.
     ‘Salamu Maria’ inatusaidia kuungana na Maria kutafakari mafumbo hayo. Inatusaidia kutambua pia Maria alikuwepo na ameunganika na Mwanae katika mafumbo yote duniani na uwepo wake Mbinguni. ‘Atukuzwe Baba’ inatukumbusha kwamba umuhimu wa maisha yote ni kwa ajili ya utukufu wa Utatu Mtakatifu.
     Hivyo, Rozari inatusaidia kutafakari juu ya umuhimu wa mafumbo ya wokovu wetu.
    Rosari inapaswa ituguse sisi.
    Ni rahisi. Kurudia kwa maneno kila mara inatusaidia kujenga hali ambayo tutatafakari mafumbo ya Mungu. Tutambue kuwa, Yesu na Maria wapo nasi katika furaha na uchungu katika maisha yetu. Tumuombe Bikira Maria atuombee tuweze kujenga tabia ya ndani ya kusali rosari kila siku.
               Hii ni nyenzo ya sala zetu zote: tufikie mahali ambapo “tutasali bila kuchoka” kama Mtakatifu Paulo alivyosema.

Tumsifu Yesu Kristo!

“Mtu ambaye si pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutawanya,” Lk 11:23

Tusali:-Ee Yesu Mwema, tujalie neema tudumu katika imani ndani na katika Wewe. Amina.


Copyright © 2016 by shajara and published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
   see: imani-katoliki.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

"Asante sana kwa maoni yako"

NYIMBO ZA DOMINIKA YA 29 YA MWAKA- C WA KANISA.

Nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka C Karibu kwa ajili ya nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka "C" Mwanzo: Ee Bwana Nimekuita  ...