Monday, 10 October 2016

MASOMO YA MISA, 10/10/2016 Jumatatu ya 28 ya Mwaka. "Wanataka ishara".


Jumatatu ya 28 ya Mwaka

   SOMO LA 1
          Gal 4:22-24, 26-27, 31;5:1

                Imeandikwa ya kuwa, Ibrahimu alikuwa na wana wawili mmoja kwa mjakazi, na mmoja kwa mwungwana. Lakini yule wa mjakazi alizaliwa kwa mwili, yule wa mwungwana kwa ahadi.
Mambo haya husemwa kwa mfano; kwa maana hawa ndio kama maagano mawili, moja kutoka mlima Sinai, lizaalo kwa utumwa, ambalo ni Hajiri.Bali Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi. Kwa maana imeandikwa, Furahi, wewe uliye tasa, usiyezaa; Paza sauti, ulie, wewe usiye na utungu; Maana watoto wake aliyeachwa pekee ni wengi Kuliko wa huyo aliye na mume. Ndiposa, ndugu zangu, sisi si watoto wa mjakazi, bali tu watoto wa huyo aliye mwungwana. Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.

Neno la Mungu......  Tumshukuru Mungu.

     WIMBO WA KATIKATI
          Zab 113:1-7 

          (1).   Enyi watumishi wa Bwana, sifuni, Lisifuni jina la Bwana. Jina la Bwana lihimidiwe Tangu leo na hata milele.
                  (K) Jina la Bwana lihimidiwe milele.
          (2).   Toka maawio ya jua hata machweo yake Jina la Bwana husifiwa. Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote, Na utukufu wake ni juu ya mbingu.
                     (K) Jina la Bwana lihimidiwe milele.
           (3).   Ni nani aliye mfano wa Bwana, Mungu wetu aketiye juu; Anyenyekeaye kutazama, Mbinguni na duniani? Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Na kumpandisha maskini kutoka jaani.
                       (K) Jina la Bwana lihimidiwe milele.

             SOMO LA INJILI
                   Lk 11:29-32

           Makutano walipokuwa wakimkusanyikia, alianza kusema, Kizazi hiki ni kizazi kibaya; kinatafuta ishara, wala hakitapewa ishara, ila ishara ya Yona. Maana, kama vile Yona alivyokuwa ishara kwa Waninawi, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu kwa kizazi hiki. Malkia wa Kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, naye atawahukumu kuwa na hatia; kwa sababu yeye alikuja kutoka ncha za dunia aisikie hekima ya Sulemani; na hapa pana mkubwa kuliko Sulemani. Watu wa Ninawi watasimama siku ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao watakihukumu kuwa na hatia; kwa sababu wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na hapa pana mkubwa kuliko Yona.

Neno la Mungu......  Sifa kwako Ee Kristu.

Copyright © 2016 by shajara  and published  by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
   see: imani-katoliki.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

"Asante sana kwa maoni yako"

NYIMBO ZA DOMINIKA YA 29 YA MWAKA- C WA KANISA.

Nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka C Karibu kwa ajili ya nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka "C" Mwanzo: Ee Bwana Nimekuita  ...