Wednesday, 5 October 2016

TAFAKARI: Jumatano, Oktoba 5, 2016 Juma la 27 la Mwaka-C.


TAFAKARI

      Jumatano, Oktoba 5, 2016, 
         Juma la 27 la Mwaka wa Kanisa
         Gal 2: 1-2, 7-14;
              Zab 116: 1-2;
         Lk 11: 1-4

        NAMNA YA KUSALI
               Maana rahisi ya sala twaweza sema, ni kuongea na Mungu. Biblia inatupa mfano wa Yesu anamkaa mapema na kupanda mlimani kusali. Katika sala tunaleta nini? Tunaweza kuleta chochote kinacho tusumbua wakati wa sala zetu, matatizo ya familia, matatizo ya mahusiano, matatizo ya afya au mambo ya kiroho. Katika Injili ya leo Yesu anawafundisha wafuasi wake kusali kwa ajili ya kuanzishwa kwa Ufalme wa Mungu, ambao ni kupenda na kutumikia mbele ya Mungu.
           Ana waambia wafuasi wa sali kwa ajili ya mkate wetu wa kila siku ambao unatupatia nguvu za kimwili na kwa wakati huo, “mkate wa uzima”- Ekaristi Takatifu ambayo ni kwa ajili ya uzima wa roho zetu.
        Na zaidi ya hayo anawaambia wasali kwa ajili ya msamaha, uponyaji wa hali yetu iliovunjika. Ni njia ipi sahihi ya kusali? Abudu kwa ukimya na ongea na Mungu mbele ya Sakramenti ya Ekaristi Takatifu.
           Wamonaki, Watawa husali na kuimba zaburi. Watu husali rosari wakati flani kabla ya kulala, wengine wakati akitembea mwenyewe njiani, Wakaresmatiki husali kwa sauti hata kunena kwa lugha. Kila mtu ana namna yake ya kuwasiliana na Mungu. La muhimu zaidi ni kuwasiliana na Mungu kweli bila kujibakiza.

          Sala: Bwana Yesu, tufundishe kusali kama ulivyo wafundisha wafuasi wako na utusaidie tuwe waaminifu na wanyovu kama watoto na kujiamini katika sala zetu. Amina.

Copyright © 2016 by shajara   and  published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
    see: imani-katoliki.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

"Asante sana kwa maoni yako"

NYIMBO ZA DOMINIKA YA 29 YA MWAKA- C WA KANISA.

Nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka C Karibu kwa ajili ya nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka "C" Mwanzo: Ee Bwana Nimekuita  ...