TAFAKARI:
JUMANNE WIKI YA 27 YA MWAKA-C
Somo:
Gal 1:13-24
Zab/Kit: 139:1-3, 13-14ab, 14c-15
Injili: Lk 10:38-42
Gal 1:13-24
Zab/Kit: 139:1-3, 13-14ab, 14c-15
Injili: Lk 10:38-42
Nukuu:
“Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu,” Gal 1:13
“Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu,” Gal 1:13
“Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu,” Gal 1:14
“Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,” Gal 1:15
“Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie,” Lk 10:40
“Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi,” Lk 10:41
“lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa,” Lk 10:42
“lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa,” Lk 10:42
TAFAKARI:
“Jenga Urafiki na Kristo Yesu, na kaa naye daima. Kujisalimisha kwako kwa Kristo kuna uzima wa milele.”
“Jenga Urafiki na Kristo Yesu, na kaa naye daima. Kujisalimisha kwako kwa Kristo kuna uzima wa milele.”
Wapendwa wana wa Mungu, somo la Injili ya leo, Mariamu ndugu yake Martha anajielewa na kumfahamu yule anayemtumikia aliye kweli katika yote, na mwisho anajisalimisha kwake.
Yawezekana mimi na wewe tumeyapa maisha yetu kipaumbele chake cha kwanza katika kujishughulisha katika mambo mengi yasiyo na mwelekeo.
Maisha yetu hayajengwi kwa wingi wa vitu tunavyofanya, bali uelewa wa yale tunayoyafanya, na kwa nini tunafanya kama tunavyoyafanya.
Martha kama tulivyo wengi anajilinganisha na yale anayofanya na kukosa muda wa kujua chanzo ya yale yote tunayoyafanya na kwa nini tunayafanya kwa namna hiyo, na ni nani anayeyaratibisha.
Martha anamlalamikia Yesu kwa nini Mariamu ndugu yake hamsaidii. Yesu anamkumbusha Martha jambo la muhimu na kusema, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi,” Lk 10:41.
Furaha yetu haitokani na vitu tunavyofanya. Kujishughulisha huku katika maana ya kufanya hivyo tu, kutatuletea mfadhaiko mkubwa sana. Maisha yetu yanamaana kwanza kabisa tunapojitambua na mwisho kujisalimisha muda wote kwa yule atupaye uzima wa milele.
Huyu ndiye chanzo cha furaha yetu na umilele wa maisha yetu. Kwake yatupasa kutumia muda mwingi naye. Huyu ndiye Kristo; njia, ukweli, na uzima wetu, Yoh 14:6.
Kuwa na Kristo ni kuchagua fungu lililo jema ambalo kwalo hatuwezi ondolewa.
Ukweli huu ndio Yesu anaomwambia Martha na sisi leo kwamba pamoja na yote tuyafanyayo, “lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa,” Lk 10:42.
Kukaa chini ya miguu ya Yesu ni ule utayari wa kulishwa neno la uzima, na kujazwa ufahamu na kufunuliwa siri ya uzima wa milele.
Kujisalimisha ndani na katika Kristo Yesu hukupa maana ya maisha yako. Mtume Paulo anathibitisha kweli hiyo kwa kusema, “Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena nayatimiliza katika mwili wangu yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo, kwa ajili ya mwili wake, yaani, Kanisa lake,” Kol 1:24.

Kristo ndiye uzima ule uupiganiao kila siku. Na hii ndiyo siri iliyofichwa kwa wamchao Mungu, yaani Watakatifu wake. Ni “siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake,” Kol 1:26.
Na kwa siri hii, Mtume Paulo amefanywa ‘mhudumu wake, sawasawa na uwakili wa Mungu, aliyopewa kwa faida watu, akilitimize neno la Mungu,’ Kol 1:25. Ndugu yangu, Kristo ndiyo njia ile sahihi unayoitafuta kila siku na mara nyingine kupotea kabisa.

Na Kristo ndiye kweli yenyewe kwa sababu ndiye ufunuo wa kweli ya Mungu Baba. Ni katika kweli hii “ambayo Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa Utukufu wa siri hii katika Mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la Utukufu,” Kol 1:27.
Kumbe wito wako na wangu kama wabatizwa na wafuasi wa Kristo walio hai kama asemavyo Mtume Paulo ni “kuhubiri habari zake tukimwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtu katika hekima yote, tupate kumleta kila mtu mtimilifu katika Kristo,” Kol 1:28.
Na huu ndio ushuhuda wa kweli. Wapendwa wana wa Mungu, hatutaweza kutoa ushuhuda huu wa Mungu kama hatupo tayari kulishirikisha kwa ukarimu neno la Mungu. Ushirikishaji huu wa Neno la Mungu kwa ukarimu tumeona leo ukifanyika kwa vitendo kutoka kwa Mariamu kwa kujisalimisha chini ya miguu ya Yesu, na kutoka kwa Mtume Paulo kwa kujitoa bila kujibakiza kwa Kanisa la Kristo na watu wake.
Hata hivyo tutaweza tu kulishirikisha neno la Mungu kwa ukarimu kama tutaweza kulitafakari kwa kina Neno la Mungu. Kulitafakari kwa kina neno la Mungu kunahitaji utayari bila shuruti wa kulipokea Neno la Mungu.
Na tutaweza kulipokea Neno la Mungu bila shuruti pale tu tutakapokuwa tayari kulisikia Neno la Mungu. Mtume Paulo anatufundisha tumaini la kweli pale tupatwapo na sintofahamu nyingi katika maisha.
Na tutaweza kulipokea Neno la Mungu bila shuruti pale tu tutakapokuwa tayari kulisikia Neno la Mungu. Mtume Paulo anatufundisha tumaini la kweli pale tupatwapo na sintofahamu nyingi katika maisha.
Mtume Paulo hakuwa na historia nzuri katika maisha yake kabla ya kuongoka. Bila shaka nawe pia ukiitazama historia yako na hayo yanayokutokea leo unakata tamaa na kujihukumu kila kukicha.
Tazama tumaini lililo mbele yako, na hasa ukitazama historia ya Mtume Paulo na kuongoka kwake. Katika hili, Mtume Paulo mwenyewe anatusimulia kwa ufupi historia ya maisha yake. Naye anasema, “Mimi ni mtu wa Kiyahudi, nalizaliwa Tarso, mji wa Kilikia, ila nililelewa katika mji huu, miguuni pa Gamalieli, nikafundishwa sheria ya baba zetu kwa usahihi, nikawa mtu wa jitihadi kwa Mungu kama ninyi nyote mlivyo leo hivi; nikawaudhi watu wa Njia hii hata kuwaua, nikawafunga, nikiwatia gerezani, wanaume na wanawake,” Mdo 22:3.

Historia hii ya Mtume Paulo inasema chochote kuhusu hali na maisha yako? Kama haitoshi, mtazame Yesu pale msalabani, kwani kaubebe ujumbe mzito sana juu ya maisha yako.
Kwa kuwambwa kwake Msalabani anakuambia hivi; “ona nilivyo hapa. Nimeyafanya haya yote kwa sababu na kupenda upeo.”
Kwa kuwambwa kwake Msalabani anakuambia hivi; “ona nilivyo hapa. Nimeyafanya haya yote kwa sababu na kupenda upeo.”
Hakika hakuna sababu ya kujiona mnyonge na mtu aliyetengwa ninapoutafakari Msalaba Mtakatifu. Kristo ndilo tumaini la kweli, na Yeye ndiye njia, kweli, na uzima wetu, Yoh 14:6. Mtume Paulo baada ya kuongoka kwake, ikiwa ni msukumo wa moja kwa moja wa Kristo mwenyewe baada ya kutupwa chini, Mdo 9:4-5, tumaini lake lote alilielekeza kwa Kristo Yesu.
Naye kwa kutoa ushuhuda wa kweli hiyo anasema, “Kwa maana, ndugu zangu, injili hiyo niliyowahubiri, nawajulisha ya kuwa siyo ya namna ya kibinadamu,” Gal 1:11.
Kwa maneno mengine ni kwamba kile alicho na anachokihubiri Mtume Paulo siyo tokeo la nguvu zake au maarifa yake binafsi, bali ni neema ya Kristo iliyo ndani yake. “Kwa kuwa sikuipokea kwa mwanadamu (Injili hiyo) wala sikufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo,” Gal 1:12. Mtume Paulo hafichi historia yake mbaya na kuona aibu kuisema mbele za watu.

Mtume Paulo anataka mimi na wewe tuelewe kwamba misimamo yetu iliyojengwa na inayojegwa na mila na desturi zetu potofu, ndani yake hakuna uzima. Naye anasema, “Maana mmesikia habari za mwenendo wangu zamani katika dini ya Kiyahudi, kwamba naliliudhi kanisa la Mungu kupita kiasi, nikaliharibu,” Gal 1:13.
Ndugu yangu, kama wewe ni mmoja wa kujipambanua kwa ubora wa kabila lako, misimamo ya kabila lako isiyo na mwono wa Kimungu, na hata umaarufu wake, basi elewa haupo njia sahihi kama wataka kuwa mfuasi wa Yesu. Mtume Paulo anakuambia wewe na mimi kwamba, “Nami naliendelea katika dini ya Kiyahudi kuliko wengi walio hirimu zangu katika kabila yangu, nikajitahidi sana katika kuyashika mapokeo ya baba zangu,” Gal 1:14.
Hata kwa kufanya hayo yote, Mtume Paulo anagundua hapakuwa na tumaini lolote, zaidi ya kupotea kwa misimamo isiyo na mwelekeo wa Kimungu na kuikosa njia ile sahihi. Wapendwa katika Kristo, usipotambua uwepo wa Mungu katika maisha yake, chochote ujengacho juu yake hukosa msingi imara, na mwisho wake uporomoka.
Baada ya kuongoka kwake, Mtume Paulo anagundua nguvu na uwepo wa Mungu katika maisha yake. “Mungu aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu, akaniita kwa neema yake,” Gal 1:15.
Hivyo kile alicho Paulo baada ya kuongoka kwake, yaani, kurudi katika njia iliyo sahihi, Kristo ndiye kila kitu kwake. Ni kwa sababu hiyo Paulo anasema kwamba, Mungu “alipoona vema kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri na watu wenye mwili na damu; wala sikupanda kwenda Yerusalemu kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu; bali nalikwenda zangu Arabuni, kisha nikarudi tena Dameski,” Gal 1:16-17.

Je, umeyapitia machungu na mahangaiko kama Mtume Paulo? Pamoja na kulihujumu Kanisa la Kristo Yesu, Mtume Paulo hakuona haya kulijenga na kujumuika na wenzake na kuwa sehemu ya mwili wa Kristo, yaani, Kanisa.
Naye anasema, “Kisha, baada ya miaka mitatu, nalipanda kwenda Yerusalemu ili nionane na Kefa, nikakaa kwake siku kumi na tano,” Gal 1:18. Tunakumbushwa pia kama wasemavyo waswahili kwamba, ‘kutenda kosa si kosa, bali kurudia kosa ni kosa.’ Kwa mara ya kwanza waweza kutenda kosa kwa kutokuwa na ufahamu kuhusu kile ukitendacho. Ila kutenda kosa lilele ilhali una ufahamu nalo, kosa hili ujeuka na kuwa dhambi. Kuongoka kwa Mtume Paulo kunayabadili maisha yake yote kwa sababu kesha kutana na kweli ambayo ndiye Kristo mwenyewe. Mtu mwingine anayeyagusa maisha yake huko Yerusalemu ni Mtume Yakobo.

Na hivi ndivyo ilivyokuwa; “Lakini sikumwona mtume mwingine, ila Yakobo, ndugu yake Bwana. Na hayo ninayowaandikia, angalieni, mbele za Mungu, sisemi uongo,” Gal 1:19-20.
Ukweli ndani na katika Kristo unamweka huru Mtume Paulo, Yoh 8:32. Kuchangamana kwake Mtume Paulo na Wakristo wenzake hakukuwa rahisi kutokana na historia yake juu ya Kanisa la Kristo aliyolitesa, na kumbukumbu walizobaki nazo vichwani mwao Jumuiya ile ya kwanza ya Wakristo. Na katika kweli hii Mtume Paulo anasema, “sikujulikana uso wangu na makanisa ya Uyahudi yaliyokuwa katika Kristo,” Gal 1:22.
Na sababu ya kutokujulikana kwake kulitokana na matendo yake juu ya Jumuiya ya kwanza ya Wakristo, na kuogopa pia kuuwawa na Wayahudi wenzake ambao kwas asa anaonekana kama kuwasaliti. Hata hivyo Wakristo wa Uyahudi kama asemavyo Paulo, “wamesikia tu ya kwamba huyo aliyetuudhi hapo kwanza, sasa anaihubiri imani ile aliyoiharibu zamani,” Gal 1:23.
Na kwa neema na tendo hilo “Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu (Paulo Mtume),” Gal 1:24. Ndugu yangu, badili mwenendo wa maisha yako, na jenga urafiki na Kristo Yesu kwa sababubu ndani na katika Kristo Yesu kuna uzima.
Mariamu na Paulo Mtume wameweza nawe na mimi tunaweza pia. Tumsifu Yesu Kristo! “Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi,” Lk 10:41
Mariamu na Paulo Mtume wameweza nawe na mimi tunaweza pia. Tumsifu Yesu Kristo! “Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi,” Lk 10:41
Tusali:-Ee Yesu na Mwokozi wangu, napenda daima kuwa rafiki yako. Niwezeshe hilo toka ndani ya Moyo wangu. Amina
Copyright © 2016 by Fr Edgar Tanga Ngowi,OSA and published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
see: imani-katoliki.blogspot.com
see: imani-katoliki.blogspot.com
No comments:
Post a Comment
"Asante sana kwa maoni yako"