Monday, 10 October 2016

TAFAKARI: Juma la 28 la Mwaka- C wa kanisa." Uhuru wa kweli ndani ya Yesu".



Jumatatu, Oktoba 10, 2016,
Juma la 28 la Mwaka wa Kanisa
          Gal 4:22-24, 26-27, 31 - 5:1;
      Zab 112:1-7;
           Lk 11:29-32

          UHURU WA KWELI NDANI YA YESU!
                Kama Mt. Paulo anavyotuambia katika Somo la kwanza, tusiache kwamwe kuadhimisha bahati kubwa ya Baraka ambayo kila mmoja anatumaini kuishiriki-baada ya kupewa uhuru wa kweli kama watoto wa Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. 
Watu wengi hawazaliwi tu katika hali ya utumwa kwasababu ya serikali zinazo kandamiza watu kwa ukosefu wa haki, bali wanazaliwa pia katika falsafa mbali mbali na dini ambazo, hatujui kama zitakuwa na uhusiano wowote na Mungu wa kweli, huaribu kile kilicho cha kweli kiasi kwamba dini huwa kama aina ya utumwa ya kuogopa zaidi kuliko uhuru wa kutoka katika dhambi ulioletwa na Kristo. Tusichukulie uhuru wetu kwa mizaha, bali tukumbuke kumshukuru Mungu kila siku kwa kujikuta tumezaliwa katika hali tuliopo, au tuliofanikiwa kuingia tangu kuzaliwa.
 Katika Injili ya leo, Yesu anaposema “tazama, yupo mkuu kuliko Yona hapa” Yesu anamuongelea nani? Anajiongelea Mwenyewe. 

Tumfanye Yesu awe rafiki na wa muhimu sana katika maisha yetu. Tuweke akilini kwamba yupo nasi kila mahali, sio wakati wa kusali tu, bali wakati unacheza, unafanya kazi, unakula, una lala.
Yesu anataka kufanya kila kitu pamoja nasi. Kadiri unavyotambua uwepo wa Yesu katika kila jambo unalofanya katika maisha yako, ndivyo unavyokuwa katika hali ya juu ya muunganiko wa ndani pamoja naye. Ukitambua upo na Yesu kila wakati huwezi kumtenda jirani yako vibaya kwa jinsi yeyote ile, labda kwa kumsema vibaya au kwa namna nyingine ile. Wayahudi wengi walikataa urafiki wake.
Je, unataka kukataa uhuru unaokuja kwasababu ya kuwa na urafiki na Yesu?

                Sala: Nakushukuru Ee Bwana, kwa uhuru tunaofurahia kama watoto wa Baba Yetu wa Mbinguni. Amina.

Copyright © 2016 by shajara  and published  by  MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
     see: imani-Katoliki.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

"Asante sana kwa maoni yako"

NYIMBO ZA DOMINIKA YA 29 YA MWAKA- C WA KANISA.

Nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka C Karibu kwa ajili ya nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka "C" Mwanzo: Ee Bwana Nimekuita  ...