Tuesday, 11 October 2016

MASOMO YA MISA, 11/10/2016 Jumanne ya 28 ya Mwaka. "Kudumu katika imani kwa Mwokozi pekee".


Jumanne ya 28 ya Mwaka

                SOMO LA 1
         Gal 5:1-6

          Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simameni, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa.
Tazama, mimi Paulo nawaambia ninyi ya kwamba, mkitahiriwa, Kristo hatawafaidia neno.
Tena namshuhudia kila mtu atahiriwaye, kwamba ni wajibu wake kuitimiza torati yote.
Mmetengwa na Kristo, ninyi mtakao kuhesabiwa haki kwa sheria; mmeanguka na kutoka katika hali ya neema. Maana sisi kwa Roho tunalitazamia tumaini la haki kwa njia ya imani. Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo.

Neno la Mungu......  Tumshukuru Mungu.

      WIMBO WA KATIKATI
           Zab 119:41, 43-45, 47-48

        (1).   Ee Bwana, fadhili zako zinifikie na mimi, Naam, wokovu wako sawasawa na ahadi yako.
                (K) Ee Bwana, fadhili zako zinifikie na mimi
         (2).   Usiliondoe neno la kweli kinywani mwangu kamwe, Maana nimezingojea hukumu zako.
                (K) Ee Bwana, fadhili zako zinifikie na mimi
         (3).    Nami nitaitii sheria yako daima, Naam, milele na milele. (K) Ee Bwana, fadhili zako zinifikie na mimi Nami nitakwenda panapo nafasi, Kwa kuwa nimejifunza mausia yako.
                 (K) Ee Bwana, fadhili zako zinifikie na mimi
        (4).   Nami nitajifurahisha sana kwa maagizo yako, Ambayo nimeyapenda.
                  (K) Ee Bwana, fadhili zako zinifikie na mimi
         (5).      Na mikono yangu nitayainulia maagizo yako niliyoyapenda, Nami nitazitafakari amri zako.
                   (K) Ee Bwana, fadhili zako zinifikie na mimi
        

          SHANGILIO
                Zab 119:135

           Aleluya ,aleluya, Umwangazie mtumishi wako uso wako, Na kunifundisha amri zako. Aleluya.

             SOMO LA INJILI
                    Lk 11:42-46

             Yesu aliwaambia Mafarisayo: Ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili.
Ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwapenda kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni. Ole wenu, kwa kuwa mmefanana na makaburi yasiyoonekana, ambayo watu wapitao juu yake hawana habari nayo. Mtu mmoja katika wana-sheria akajibu, akamwambia, Mwalimu, kwa kusema hayo umetushutumu sisi nasi. Akasema, Nanyi wana-sheria, ole wenu, kwa sababu mwawatwika watu mizigo isiyochukulika, wala ninyi wenyewe hamwigusi mizigo hiyo hata kwa kimoja cha vidole vyenu.

Neno la Mungu ......  Sifa kwako Ee Mungu.

Copyright © 2016 -Shajara   and. Published   by. MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
   see: imani-katoliki.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

"Asante sana kwa maoni yako"

NYIMBO ZA DOMINIKA YA 29 YA MWAKA- C WA KANISA.

Nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka C Karibu kwa ajili ya nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka "C" Mwanzo: Ee Bwana Nimekuita  ...