Dominika ya 27 ya Mwaka
SOMO LA 1
Hab. 1:2 – 3; 2:2 – 4
Ee Bwana, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa. Mbona wanionyesha uovu, na kunitazamisha ukaidi? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea. Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi asana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia; ingojee; kwa kuwa haina bidi kuja, haitakawia. Tazama, roho yake hujivunia, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa Imani yake.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 95:1 – 2, 6 – 9
(1). Njoni tumwimbie Bwana, Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu. Tuje mbele yake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi.
(K) Ingekuwa heri leo tusikie sauti yake! Tusifanye migumu mioyo yetu.
(2). Njoni, tuabudu tusujudu, Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba. Kwa maana ndiye Mungu wetu, Na sisi, tu watu wa malisho yake, Na kondoo za mkono wake.

(3). Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! Msifanye migumu mioyo yenu; Kama huko Meriba; Kama siku ile ya Musa jangwani, Hapo waliponijaribu baba zenu, Wakanipima, wakayaona matendo yangu.

SOMO LA 2
2Tim. 1:6 – 8; 13 – 14
Ndugu yangu, nakukumbusha, uichochee karama ya Mungu, iliyo ndani yako kwa kuwekewa mikono yangu. Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu nay a upendo nay a moyo wa kiasi. Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wal ausinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu. Shika kielelezo cha maneno yenye uzima uliyoyasikia kwangu, katika Imani na upendo ulio katika Kristo Yesu. Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu.

SHANGILIO
Yn. 15:15
Aleluya, aleluya, Ninyi nimewaita rafika, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa baba yangu nimewaarifuni. Aleluya!

SOMO LA INJILI
Lk. 17:5 – 10
Mitume walimwambia Bwana, Tuongezee Imani. Bwana akasema, Kama mngekuwa na Imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng’oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii. Lakini, ni nani kwenu mwenye mtumwa alimaye au achungaye ng’ombe, atakayemwambia mara arudipo kutoka shambani, Njoo upesi, keti, ule chakula? Je! Hatamwambia, Nifanyie tayari chakula, nile; jifunge unitumikie, hata niishe kula na kunywa, ndipo nawe utakapokula na kunywa? Je! Atampa asante yule mtumwa; kwa sababu ameyafanya aliyoagizwa? Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya.

Copyright © 2016 by shajara and published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
see: imani-katoliki.blogspot.com
see: imani-katoliki.blogspot.com
No comments:
Post a Comment
"Asante sana kwa maoni yako"