Thursday, 6 October 2016

TAFAKARI: Alhamisi, Oktoba 6, 2016, Juma la 27 la Mwaka-C wa kanisa." Ombeni nanyi mtapewa"


TAFAKARI

        Alhamisi, Oktoba 6, 2016,
    Juma la 27 la Mwaka C wa Kanisa
          Gal 3: 1-5;
      Lk 1: 69-75;
        Lk 11: 5-13

          KUOMBA!
        “Ombeni nanyi mtapewa…”
               nimeomba mara nyingi, lakini sikupata hata kimoja.
     Haya ni majibu yetu kila mara kwenye huo ujumbe katika Injili.
     Lakini tujiulize, tunatulia nakujitafiti na kutafakari; je, nimeomba kwa ajili ya malengo sahihi? Je, ninafahamu thamani ya vitu ninavyo omba? Je, vitu ninavyo omba na kuhitaji nivya lazima kabisa? Mtoto asiye na meno anaweza kumuomba baba yake mua. Je, baba yake atampa? Hapana. Baba atasubiri mpaka akue awe na meno ndio ampe.
Nyani hafahamu thamani ya dhahabu ulioshika. Lakini aweza kunyosha mkono kuomba, je utampatia? Hapana, haumpi. Kwasababu unafahamu thamani yake! Ni katika hali hiyo tunaweza tusijue tunanyoosha mkono kuomba nini, lakini Mungu anajua.
          Hii haimanishi tusiombe chochote tunacho penda. Tunaweza kuomba lakini kama hatuvipati tunavyo omba, tusikatishwe tamaa. Mungu anajibu katika hali ambayo itakunufaisha na njia ambayo itakufanya ulicho omba kisikutenge naye.

       Sala: Bwana, naomba mapenzi yako yatendeke. Amina

Copyright © 2016 by Shajara and published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
    see: imani-katoliki.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

"Asante sana kwa maoni yako"

NYIMBO ZA DOMINIKA YA 29 YA MWAKA- C WA KANISA.

Nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka C Karibu kwa ajili ya nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka "C" Mwanzo: Ee Bwana Nimekuita  ...