Wednesday, 12 October 2016

MASOMO YA MISA, 12/10/2016 Jumatano ya 28 ya Mwaka. "Maisha ya kiroho na ya kidunia."


Jumatano ya 28 ya Mwaka

         SOMO LA 1
              Gal 5:18-25

                  Mkiongozwa na roho, hampo chini ya sheria.
Basi matendo ya mwili ni dhahiri ndiyo haya uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina,faraka, urushi,husuda, ulevi,ulafi na mambo yanayo fanana na hayo; katika hayo nawaambia mapema kama nilivyokwisha kuwaambia ya kwamba watu watendayo mambo ya jinsi hiyo hawata urithi ufalme wa Mungu.Lakini tunda la roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi;juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Na hao walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na mawzo yake mabaya na tamaa zake.
Tukiishi kwa Roho na tuenende kwa Roho.

Neno la Mungu......  Tumshuru Mungu.

        WIMBO WA KATIKATI
             Zab 1:1-4, 6

          (1).   Heri mtu yule asiye kwenda Katika shauri la wasio haki Wala hakusimama katika njia ya wakosaji Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha Bali sheria ya bwana ndiyo impendezayo Na sheria yake huitafakari mchana na usiku
                     (K) Wanaokufuata, EeBwana, watakuwa na nuru ya uzima
         (2).    Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya kijito vya maji Uzaao matunda yake kwa majira yake Wala jani lake halinyauki Na kila alitendalo litafanikiwa
                     (K) Wanaokufuata, EeBwana, watakuwa na nuru ya uzima
         (3).    Sivyo walivyo wasio haki Hayo ni kama makapi yapeperushwayo na upepo Kwa kuwa bwan anaijua njia ya wenye haki Bali njia ya wasio haki itapotea
                       (K) Wanaokufuata, EeBwana, watakuwa na nuru ya uzima

           SHANGILIO
                Zab 111:7, 8

          Aleluya, aleluya Maagizo yako yota Ee Bwana ni amini Yamethibitika milele na milele Aleluya

            SOMO LA INJILI
                  Lk. 11:42-46

             Yesu aliwaambia Mafarisayo: Ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili.
Ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwapenda kuketi mbele kakika masinagogi, na kusalimiwa masokoni. Ole wenu, kwa kuwa mmefanana na makaburi yasiyoonekana, ambayo watu wapitao juu yake hawana habari nayo. Mtu mmoja katika wanasheria akajibu, akamwambia, Mwalimu, kwa kusema hayo umetushutumu sisi nasi. Akasema, Nanyi wanasheria, ole wenu, kwa sababu mwawatwika watu mizigo isiyochukulika, wala ninyi wenyewe hamwigusi mizigo hiyo hata kwa kimoja cha vidole vyenu.

Neno la Mungu...... Sifa kwako Ee Mungu.

Copyright © 2016 Shajara  and  published  by  MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
     see: imani-katoliki.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

"Asante sana kwa maoni yako"

NYIMBO ZA DOMINIKA YA 29 YA MWAKA- C WA KANISA.

Nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka C Karibu kwa ajili ya nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka "C" Mwanzo: Ee Bwana Nimekuita  ...