Tuesday, 25 October 2016

TAFAKARI 25/10/2016 Jumanne ya 30 ya Mwaka - C

Jumanne, Oktoba 25, 2016, Juma la 30 la Mwaka wa Kanisa Ef 5: 21-33; Zab 128: 1-5; Lk 13: 18-21 UFALME WA MUNGU-UPO NA BADO UTAKAMILIKA Katika somo la kwanza Mtume Paulo anaendelea na maelekezo yake kwa Waefeso jinsi ya kuenenda kama wafuasi wa Kristo na leo anaingia katika ngazi ya familia. Anawaambia wake wawatii waume zao na waume wawapende wake zao. Ni katika kuendeleza tunu hizi katika familia ndipo twaweza kusema kuwa tunajenga ufalme wa Mungu katika familia zetu. Tunapoishi vizuri na wenzetu kwa upendo na kwa fadhili za Kimungu kama alivyotufundisha Kristo tunakuwa tunaishi Ufalme wa Mungu tungali hapa duniani. Ni katika kuuishi vizuri ufalme huo hapa duniani inatupa kibali cha utimilifu wake katika maisha yajayo. Yesu anatoa mifano miwili katika akilielezea Ufalme huu wa Mungu. Ni ufalme ghani unao hubiriwa na Yesu? Mfano wa punji ya haradali na chachu unaelezea sifa za muhimu za Ufalme wa Mungu alio hubiri Yesu: udogo wake, tabia yake yakutokuonekana kirahisi; kazi yake na uwepo wake. Yesu leo anafananisha ufalme wa Mungu na punji ya haradali na chachu. Puche ya haradali ni ndogo tena sana. Inapopandwa ardhini inakuwa na kuwa mti mkubwa ambapo ndege wa angani hupata makao. Lakini, pamoja na kwamba ni ndogo, na haijulikani na kujificha inapokuwa ardhini haibaki hapo tu bali huchipua na kumea. Chachu kidogo sana, ambayo huwezi kuiona kwa macho baada ya kuwekwa katika unga, haibaki kama ilivyo bali huumua unga wote. Tabia ya Uwepo wake na utimilifu wake ujao wa Ufalme wa Mungu unaweza kuwa wetu tu kama matunda ya kazi ya Roho Mtakatifu. Sala: Bwana, tunaomba ufungue macho yetu tuweze kutambua maajabu ya Ufalme wako, uliojificha na uwepo wake katika mambo madogo. Amina.

1 comment:

  1. Hakika, hali ya kiroho hudhibiti mambo ya kimwili.

    Mimi na mume wangu tulikuwa tumeoana kwa zaidi ya miaka 8 bila kupata mtoto. Tulitembelea hospitali tofauti, lakini kimatibabu sote tulikuwa sawa, lakini mimba haikutokea. Siku moja, nilikutana na mpenzi wangu wa zamani. Tulitumia muda pamoja, tukazungumza kuhusu yaliyopita, na hatimaye tukafanya ngono. Baadaye, nikapata mimba. Nilichanganyikiwa na sikujua la kufanya.

    Nilijua mtoto hakuwa wa mume wangu, lakini kwa udadisi, nilifanya kipimo cha ubaba kwa siri bila idhini ya mume wangu, na matokeo yakathibitisha kwamba hakuwa baba mzazi. Hata hivyo, sikutaka kuharibu ndoa yangu au kuharibu furaha na furaha ambayo mtoto alileta kwa familia yetu, hasa mama mkwe wangu.

    Rafiki yangu kisha akanipendekeza mtaalamu wa mizimu mwenye nguvu. Niliwasiliana naye na kumuelezea kila kitu, Alinipa maagizo, ambayo nilifuata, na akafanya ibada ambayo ilitakiwa kufanya kipimo cha ubaba kilingane na mume wangu na kufanya damu ilingane na yake. Mwanzoni, sikuamini kwa sababu ilisikika kuwa ya ajabu.
    Miezi sita baada ya ibada, tulifanya mtihani mwingine wa ubaba, na kwa mshangao wangu, matokeo yalionyesha kuwa mtoto sasa alikuwa wa mume wangu.

    Nataka kutumia fursa hii kumthamini mtaalamu wa mizimu.

    Ninampendekeza. Ikiwa unahitaji ibada ili kupata mimba haraka.

    .Ibada ya kumrudisha mwenzi wako wa zamani.

    Ibada ya kurejesha urithi wako/kushinda bahati nasibu na zaidi.

    Maelezo yake. wightmagicmaster@gmail.com

    WhatsApp: +2349046229159

    ReplyDelete

"Asante sana kwa maoni yako"

NYIMBO ZA DOMINIKA YA 29 YA MWAKA- C WA KANISA.

Nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka C Karibu kwa ajili ya nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka "C" Mwanzo: Ee Bwana Nimekuita  ...