Tuesday, 25 October 2016

TAFAKARI Jumatano ya 30 ya Mwaka - C "Mlango wa kuingia katika ufalme wa Mungu".


TAFAKARI
      Jumatano, Oktoba 26, 2016,
     Juma la 30 la Mwaka wa Kanisa
 
        Efe 6:1-9;
            Zab 144:10-14;
              Lk 13:22-30
 
     
           MLANGO WAKUINGIA KATIKA UFALME WA MUNGU!

             Mungu ametuandalia maisha ya uzima wa milele na maisha haya ni kwa ajili ya wote. Yesu anasema katika Injili ya leo, “Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu” (Lk 13:29).
Kitu kimoja ambacho ni hakika ni kwamba hakuna upendeleo katika Ufalme wa Mungu. Petro anatuambia katika Kitabu cha matendo ya Mitume, “kwa hakika ninajua Mungu hana upendeleo, bali katika kila taifa anayemuogopa yeye nakufanya yalio haki anakubaliwa naye. (Mdo10:34-35).
Hivyo yule mtu alivyo muuliza Yesu, “je ni wachache watakao okolewa ?”. Yesu hakumjibu moja kwa moja. Yesu hasemi ni wachache au wengi, hawa au wale, anasema tu “jitahidini kuingia katika mlango mwembamba” . (Lk 13:23-24). Kwahiyo kwa kadiri ya Yesu ni kwa wale wanaojitahidi kuingia kupitia mlango huo watakao ingia. Na kwasababu mlango wa kuingia katika uzima wa milele ni mwembamba, waweza kujichunguza ni mizigo mingapi uliobeba ambayo yaweza kukuzuia kuingia, usije kukumbwa na mshangao. Yesu anasema “Na tazama, wako walio wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wa kwanza watakaokuwa wa mwisho” (Lk 13:30). Walioteuliwa waweza kuwa wa mwisho.
Watu kutoka kaskazini na kusini, magharibi na Mashariki waweza kuwatangulia. Kwahiyo, wale wanaodhani wana nafasi ya pekee katika Ufalme wa Mungu kwasababu tuu wana elimu kuhusu Yesu, au kwasababu wanaenda kanisani kila jumapili, au kwasababu wamesikia mahubiri ya kila jumapili wasije wakashangaa ikawa kinyume. Hili ndilo onyo la Yesu. Kwa njia nyingine tuangalie sana kama kila tunalotenda ni kwa ajili ya ufalme wa Mungu na kumrudishia yeye utukufu au ni kwa ajili ya utukufu binafsi? Manake twaweza kufanya yote vyema ili tuonekane machoni pa watu na kusifiwa na wanadamu, tukajijengea utukufu binafsi! Kwa njia hii tusishangae siku ya mwisho.

       Sala: Bwana Yesu, asante kwa zawadi ya ukombozi. Naomba unipe neema ili niweze kuwa miongoni mwao wote watakao okolewa nawe nakuingia katika Ufalme wako. Amina.

Copyright © 2016 Shajara and published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
      see: imani-katoliki.blogspot.com

MASOMO YA MISA, 26/10/2016 Jumatano ya 30 ya Mwaka - C


Jumatano ya 30 ya Mwaka

      SOMO LA 1
         Efe 6:1-9

        Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.
Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.Enyi watumwa, watiini wao walio bwana zenu kwa jinsi ya mwili, kwa hofu na kutetemeka, kwa unyofu wa moyo, kana kwamba ni kumtii Kristo;wala si kwa utumwa wa macho tu kama wajipendekazao kwa wanadamu bali kama watumwa wa Kristo, mkitenda yampendezayo Mungu kwa moyo;kwa nia njema kama kumtumikia Bwana wala si mwanadamu;mkijua ya kuwa kila neno jema alitendalo mtu atapewa lilo hilo na Bwana kwamba ni mtumwa au kwamba ni huru.Nanyi, akina bwana, watendeeni wao yayo hayo, mkiacha kuwaogofya, huku mkijua ya kuwa yeye aliye Bwana wao na wenu yuko mbinguni, wala kwake hakuna upendeleo

      WIMBO WA KATIKATI
          Zab 145:10-14

            Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru, Na wacha Mungu wako watakuhimidi. Wataunena utukufu wa ufalme wako, Na kuuhadithia uweza wako. (K)
             Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari ya ufalme wake. Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote, (K)
             Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote, Bwana huwategemeza wote waangukao, Huwainua wote walioinama chini. (K)

       SOMO LA INJILI
            Lk 13:22-30

              Yesu alikuwa akipita katika miji na vijiji, akifundisha, katika safari yake kwenda Yerusalemu.Mtu mmoja akamwuliza, Je! Bwana, watu wanaookolewa ni wachache? Akawaambia,Jitahidini kuingia katika mlango ulio mwembamba, kwa maana nawaambia ya kwamba wengi watataka kuingia, wasiweze. Wakati mwenye nyumba atakaposimama na kuufunga mlango, nanyi mkaanza kusimama nje na kuubisha mlango, mkisema, Ee Bwana, tufungulie; yeye atajibu na kuwaambia, Siwajui mtokako;ndipo mtakapoanza kusema, Tulikula na kunywa mbele yako, nawe ulifundisha katika njia zetu. Naye atasema, Nawaambia, Siwajui mtokako; ondokeni kwangu ninyi nyote mlio wafanyaji wa udhalimu. Ndipo kutakapokuwa na kilio na kusaga meno, mtakapomwona Ibrahimu na Isaka na Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, nanyi wenyewe mmetupwa nje. Nao watakuja watu toka mashariki na magharibi, na toka kaskazini na kusini, nao wataketi chakulani katika ufalme wa Mungu. Na tazama, wako walio wa mwisho watakaokuwa wa kwanza, na wa kwanza watakaokuwa wa mwisho.


Copyright © 2016 Shajara and published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG 

TAFAKARI 25/10/2016 Jumanne ya 30 ya Mwaka - C

Jumanne, Oktoba 25, 2016, Juma la 30 la Mwaka wa Kanisa Ef 5: 21-33; Zab 128: 1-5; Lk 13: 18-21 UFALME WA MUNGU-UPO NA BADO UTAKAMILIKA Katika somo la kwanza Mtume Paulo anaendelea na maelekezo yake kwa Waefeso jinsi ya kuenenda kama wafuasi wa Kristo na leo anaingia katika ngazi ya familia. Anawaambia wake wawatii waume zao na waume wawapende wake zao. Ni katika kuendeleza tunu hizi katika familia ndipo twaweza kusema kuwa tunajenga ufalme wa Mungu katika familia zetu. Tunapoishi vizuri na wenzetu kwa upendo na kwa fadhili za Kimungu kama alivyotufundisha Kristo tunakuwa tunaishi Ufalme wa Mungu tungali hapa duniani. Ni katika kuuishi vizuri ufalme huo hapa duniani inatupa kibali cha utimilifu wake katika maisha yajayo. Yesu anatoa mifano miwili katika akilielezea Ufalme huu wa Mungu. Ni ufalme ghani unao hubiriwa na Yesu? Mfano wa punji ya haradali na chachu unaelezea sifa za muhimu za Ufalme wa Mungu alio hubiri Yesu: udogo wake, tabia yake yakutokuonekana kirahisi; kazi yake na uwepo wake. Yesu leo anafananisha ufalme wa Mungu na punji ya haradali na chachu. Puche ya haradali ni ndogo tena sana. Inapopandwa ardhini inakuwa na kuwa mti mkubwa ambapo ndege wa angani hupata makao. Lakini, pamoja na kwamba ni ndogo, na haijulikani na kujificha inapokuwa ardhini haibaki hapo tu bali huchipua na kumea. Chachu kidogo sana, ambayo huwezi kuiona kwa macho baada ya kuwekwa katika unga, haibaki kama ilivyo bali huumua unga wote. Tabia ya Uwepo wake na utimilifu wake ujao wa Ufalme wa Mungu unaweza kuwa wetu tu kama matunda ya kazi ya Roho Mtakatifu. Sala: Bwana, tunaomba ufungue macho yetu tuweze kutambua maajabu ya Ufalme wako, uliojificha na uwepo wake katika mambo madogo. Amina.

MASOMO YA MISA, 25/10/2016 Jumanne ya 30 ya Mwaka - C



MASOMO YA MISA, 
OKTOBA 25, 2016 JUMANNE, 
    JUMA LA 30 LA MWAKA WA KANISA


       SOMO 1 
      Efe. 5:21 – 33
           Hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo. Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu. Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili. Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo, vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo. Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake; ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno; apate kujiletea Kanisa atukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wal alolote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda wenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye navyolitendea Kanisa. Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake. Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.
    Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu. 

    WIMBO WA KATIKATI
        Zab. 128:1 – 5 (K)
         (K) Heri kila mtu amchaye Bwana.

         Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake. Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema. (K)
         Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Vyumbani mwa nyumba yako. Wanao kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako. (K)
         Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye Bwana. Bwana akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako. (K)

        SHANGILIO 
          1Pet. 1:25 
                   Aleluya, aleluya, Neno la Bwana hudumu hata milele, na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu. Aleluya.

         INJILI
              Lk. 13:18-21
         Yesu alisema, Ufalme wa Mungu umefanana na nini? Nami niufananishe na nini? Umefanana na punji ya haradali aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake; ikamea, ikawa mti; ndege wa angani wakakaa katika matawi yake. Akasema mara ya pili, Niufananishe na nini ufalme wa Mungu? Umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke akaisitiri ndani ya pichi tatu za unga, hata ukachacha wote pia.

   Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.

TAFAKARI Jumatatu ya 30 ya Mwaka - C

TAFAKARI Jumatatu, Oktoba 24, 2016, Juma la 30 la Mwaka wa Kanisa Ef 4:32 – 5:8; Zab 1:1-4, 6; Lk 13:10-17 HURUMA YA MUNGU! Katika Injili ya Leo Yesu anamponya Mwanamke mmoja mgonjwa aliyekuwa na pepo kwa muda wa miaka kumi nane. Lakini cha kushangaza viongozi wa Sinagogi hawakufurahi, kwasababu wao walijishughulisha na Sabato na si yule Mwanamke aliyekuwa mgonjwa akiteseka. Ndio maana Yesu anawaita “Wanafiki” kwasababu walishindwa kutoa mahitaji ya watu, na badala yake kuwafundisha watu woga na kujenga watu wasiwasi mioyoni mwao kuhusu Mungu. Walishindwa kuonesha upendo na kufundisha huruma na msamaha wa Mungu Baba na mara nyingi walielekea kwenye adhabu, na kushika sheria kwa nguvu. Katika hali hiyo hiyo, Paulo anawaambia Waefeso wawe wakarimu, na wenye huruma moyoni na msamaha kwa wengine kwasababu Mungu amewaonesha huruma yake kwa njia ya Mwanae Yesu Kristo. Anawaita wamuige Mungu kwa kumpenda Yesu Kristo kama njia pekee ya kumwendea Mungu, ni Yesu pekee aliyetupa akili kamili kuhusu Mungu. Hakuna aliyefahamu ufalme wa Mungu unafananaje, kabla ya Yesu kuja kutupa mifano mbali mbali. Leo Yesu anatualika leo tuwatembelee wagonjwa, wanaoteseka na kuwaonesha huruma ambayo Mungu ameionesha kwetu. Sala: Bwana mpendwa, tusaidie tuweze kuhisi upendo wako na huruma yako ili tuweze kuwa mwanga wa kweli wa huruma na ukarimu wako kwa wanadamu wote. https://play.google.com/store/apps/details?id=tk.shajara.shajara

MASOMO YA MISA, Jumatatu ya 30 ya Mwaka- C

Jumatatu ya 30 ya Mwaka SOMO LA 1 Efe. 4:32 – 5:8 Iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi. Hivyo mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa; mkaenende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi; tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato. Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wowote wala kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu; wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru. Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu. Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi. Basi msishirikiane nao. Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru. WIMBO WA KATIKATI Zab. 68:1, 3, 5 – 6, 19 – 20 Heri mtu yule asiyekwenda Katika shauri la wasio haki; wala hakusimama katika njia ya wakosaji; Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha. Bali sheria ya Bwana ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku. (K) Mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa. Naye atakuwa kama mti uliopandwa Kandokando ya vijito vya maji, Uzaao matunda yake kwa majira yake, Wala jani lake halinyauki; Na kila alitendalo litafanikiwa. (K) Mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa. Sivyo walivyo wasio haki; Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo, Kwa kuwa Bwana anaijua njia ya wenye haki. Bali njia ya wasio haki itapotea. (K) Mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa. SHANGILIO Yak. 1:18 Aleluya, aleluya, Kwa kupenda kwake mwenyewe, Baba alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake. Aleluya. SOMO LA INJILI Lk. 13:10-17 Siku ya sabato Yesu alikuwa akifundisha katika sinagogi mojawapo. Na tazama, palikuwa na mwanamke aliyekuwa na pepo wa udhaifu muda wa miaka kumi na minane, naye amepindana, hawezi kujinyosha kabisa. Yesu alipomwona alimwita, akamwambia, Mama, umefunguliwa katika udhaifu wako. Akaweka mikono yake juu yake, naye akanyoka mara hiyo, akamtukuza Mungu. Basi mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu amemponya mtu siku ya sabato, akajibu akawaambia mkutano, Kuna siku sita zifaazo kufanya kazi, basi njoni mponywe katika siku hizo, wala si katika siku ya sabato. Lakini Bwana akamjibu akasema, Enyi wanafiki, kila mmoja wenu, Je! Hamfungi ng’ombe wake au punda wake siku ya sabato katika zizi, aende naye kumnywesha? Na huyu mwanamke, aliye wa uzao wa Ibrahimu, ambaye Shetani amemfunga miaka kumi na minane hii, haikupasa afunguliwe kifungo hiki siku ya sabato? Aliposema haya wakatahayari wote walioshindana naye; mkutano wote wakafurahi kwa sababu ya mambo matukufu yaliyotendwa na yeye. https://play.google.com/store/apps/details?id=tk.shajara.shajara

TAFAKARI Dominika ya 30 ya Mwaka - C

TAFAKARI Jumapili, Oktoba 23, 2016. Dominika ya 30 ya Mwaka C wa Kanisa YbS 35: 12-14, 16-18 Zab 34: 2-3, 17-19, 23 2 Tim 4: 6-8, 16-18 Lk 18: 9-14 KUKUBALIWA NA MUNGU! Katika somo la kwanza, nabii Yoshua Bin sira, anawaonya matajiri na viongozi waliowakandamiza wanyonge, yatima na wajane. Tena wakichukuwa mali zao nakujipatia utajiri, huku wakitolea sehemu ya mali hiyo ya udhalimu kama sadaka yao kwa Mungu. Nabii anawaandikia, nakuwaambia Mungu hapokei sadaka ya namna hiyo. Sadaka zitokanazo na udhalimu na uonevu wa wanyonge na maskini hazina kibali machoni pa Mungu. Kilio cha yatima na wajane kinamfikia Mungu haraka kabisa, anawaasa watu hao kuacha hali hiyo kwani Mungu hatakawia kujibu sala za wanyonge wake. Mungu yupo karibu na maskini na wanao onewa daima. Wanapo mwita yeye huja mara. Na zaidi sana anawaeleza kwamba sala ya mtu mnyenyekevu hupasua mawingu na haitatulia mpaka itakapo mfikia Mungu. Kumbe tunapo mwendea Mungu kwa moyo wa unyenyekevu na wa kweli, sala yetu hupenya na kumfikia yeye. “Mungu huwapinga wenye majivuno, lakini huwapa neema wanyenyekevu” (1 Pt 5:5). Injili ya leo ni Injili ambayo kila Muumini anapaswa kuwa makini kwa karibu kabisa. Ni kuhusu juu ya mfano aliotoa Yesu wa waamini wawili, Mfarisayo na mtoza ushuru. Ni vizuri kutambua kuwa wote wawili walikuwa waumini waliokuwa wakisali kwa Mungu mmoja, ni vizuri pia kutambua wote walikuwa katika dini moja na wote walikuwa katika kanisa(sinagogi) moja. Wote walikuwa ni waamini wanaoingia katika sinagogi na kusali sala za kila siku. Lakini sisi tunaona nini? Mwisho wa sala mmoja wao anaenda nyumbani kwa Amani lakini mwingine sivyo. Sisi wote, tuna mwamini Mungu, tunapaswa tuwe makini na ujumbe huu sio tuu kujifunza kutolea sadaka yenye kibali machoni pa Mungu bali kuishi maisha ya Imani ambayo yatatuongoza katika kustahilishwa na sio kuja kusikitishwa siku ya mwisho. Mafarisayo walikuwa ni watu ambao walijipa nidhamu na kujitoa kabisa katika dini yao. walikuwa ni waamini makini waliojitoa maisha yao kwa kusali kila mara na kushika neno la Mungu. Walitoa zaka za mapato yao yote sio tu kiasi kile walichotakiwa kutoa. Wakati Mfarisayo alivyosema katika mfano huu wa Yesu “mimi sio kama watu wengine: wanyanganyi, wadhalimu, wazinzi, wala sio kama huyu mtoza ushuru. Mimi ninafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote”. (Lk 18:11-12) hakuwa anatania. Ni wakristo wachache wanaweza kufikia kiwango hichi cha mafarisayo. Lakini walipungukiwa kitu. Watoza ushuru, kwa upande mwingine, kwa ujumla walikuwa wakichukuliwa kama watu walio na maadili hafifu. Kwasababu Watoza ushuru walifanya kazi kwa ajili ya wapagani Wakirumi, walijichanganya nao, na mara nyingi kuchukua fedha zisizo halali kutoka kwao, na inasemekana walikuwa katika hali ya unajisi. Kama dini ya kipindi hicho ilivyokuwa, watoza ushuru walichukuliwa kama wadhambi wa wakubwa sana tena wahadharani walio njiani kuelekea motoni. Lakini Watoza ushuru walijua pia sauti ya wengi si mara zote ni sauti ya Mungu. Walitumainia ukombozi sio kutokana na faida ya dini yeyote au faida ya maadili yao flani bali katika neema ya huruma ya Mungu. Kumwamini tu Mungu haimuokoi yeyote. Mt. Yakobo anatuambia hata shetani mwenyewe anamwamini Mungu na anatetemeka kwa hofu. (Yk 2:19). Mafarisayo katika Injili walimwamini Mungu kama Mungu aliye na ubaguzi, Mungu anaye wapenda watu wema tu na kuwachukia wabaya. Kwa hiyo mafarisayo kwa haraka walijua tu kuwapenda watu wema kama wao tu, na kuwaangalia wengine kama waovu na wadhambi kabisa kama watoza ushuru. Yesu anatoa mfano huu juu ya mafarisayo kwasababu “walijiamini wenyewe kwamba ni wenye haki na kuwachukulia wengine wadhambi” (mstari wa. 9). Mtoza ushuru kwa upande mwingine, hakujiaminisha mwenyewe, au kwa kitu kingine bali kwa huruma ya Mungu. Akisimama mbali, tena bila kujaribu kutazama mbinguni, anapiga kifua akiomba “Mungu, nionee huruma mimi mdhambi” huyu ndiye mtu aliyeenda nyumbani akiwa na Amani na Mungu na sio yule mfarisayo aliyejiwekea haki. Sisi pia kama Mafarisayo na watoza ushuru tunakuja mbele ya Mungu kila wakati kumwabudu na kusali. Sisi pia tunategemea kurudi nyumbani tukiwa na Amani na Mungu. Tujifunze kutoka kwa Mtoza ushuru siri ya kumwabudu Mungu katika hali ya kukubaliwa naye. Katika hali ya unyofu na unyenyekevu, katika hali ya kuwaombea wenzetu sio kuorodhesha dhambi zao. Kwanza kabisa, tunapaswa tusiwasikilize watu na hata nafsi zetu zinapotuambia Mungu ana hasira sana nasi, na kwamba hawezi kutusamehe. Pili, tunapaswa kukubali dhambi zetu na kujikabidhi na kuamini huruma ya Mungu ambayo ni kubwa kuliko dhambi yeyote tuliotenda. Na mwisho kabisa, tumuahidi Mungu tusije kuwaona wengine wadhambi na kuwahukumu bali tuwasaidie katika tamaa yao yakumtafuta Mungu, kama vile mtoza ushuru leo anavyotusaidia katika tamaa yetu yakumtafuta Mungu. Kumbuka, mara zote na nyakati zote, Mungu anawapinga wenye majivuno, lakini anawapa wanyenyekevu neema. Njia ya kwenda kwenye utakatifu wa kweli ni njia ya unyenyekevu. Ni vigumu kuwa mtakatifu bila unyenyekevu. Unyenyekevu una upendo ndani yake kama msingi wa fadhila zote za Kikristu. Watakatifu wote bila kumuacha yeyote walikuwa wanyenyekevu kabisa. Sala ya Mtoza ushuru ni sala ambayo watakatifu wengi waliisali kila mara na nyakati zote “Ee Mungu, unionee huruma mimi mdhambi”. Ndio maana watakatifu licha ya njia yao nzuri ya utakatifu ya maisha yao, bado walihudhuria sakramenti ya kitubio kila mara kama kiini cha maisha yao. Katika Mwaka huu wa huruma ya Mungu na siku zote za maisha yetu, tujipatanishe na Mungu kila mara kwa sakramenti ya Kitubio bila kuwa na wasi wasi, tusiwe na wasi wasi juu ya huruma ya Mungu. Sakramenti ya kitubio inatusaidia kukuwa katika kiini cha unyenyekevu na katika mstari wa utakatifu. Tukifanya hivyo tutaweza kusema kama Paulo anavyosema katika somo la pili kwamba amevipiga vita vilivyo vizuri na mwendo ameumaliza. Paulo aliteseka mahakamani huko Rumi na hakuna aliye mtetea kwasababu wakristo waliogopa utawala wa Kirumi. Paulo alisali na alikuwa na matumaini kwa Mungu. Paulo tofauti kabisa na yule mfarisayo tuliemuona katika somo la Injili, anasali akiwaombea Wakristo wenzake waliojua kabisa amefungwa gerezani lakini hawakwenda kumtetea, yeye anawaombea kwa Mungu asiwahesabie hatia kwa jambo hilo. Paulo anatupa mfano wa pekee wakuwaombea ndugu zetu. Tusiwe wabinafsi hata katika kusali, tusiwaombee wenzetu mabaya bali tuwaombee mema ili kwa wema huo sisi nasi tutakuwa tumeiga tabia ya Kimungu ya kuwapenda watu wote. Daima tujione sisi wote ni wadhambi tunaohitaji neema ya Mungu. Na daima tutafute huruma yake kwa mioyo ya unyenyekevu wa kweli. Sala: Bwana Yesu, ulijinyenyekesha mwenyewe kwenye mti wa msalaba, tujaze neema ya unyenyekevu ili tuweze kukubalika na kuwa wema machoni pako. Amina https://play.google.com/store/apps/details?id=tk.shajara.shajara

MASOMO YA MISA, Dominika ya 30 ya Mwaka.

Dominika ya 30 ya Mwaka SOMO LA 1 Ybs 35:12-14,16-19 Kwa kuwa Bwana ndiye mhukumu wala hakijali cheo cha mtu. Hatamkubali ye yote juu ya maskini, naye ataisikiliza sala yake aliyedhulumiwa. Hatayadharau kamwe malalamiko ya yatima, wala ya mjane amwelezapo habari zake. Malalamiko yakealiyeonewa yatapata kukubaliwa, na dua yake itafika hima mbinguni. Sala yake mnyenyekevu hupenya mawingu; wala haitatulia hata itakapowasili; wala haitaondoka hata Aliye juu atakapoiangalia, akaamua kwa adili, akatekeleza hukumu. Wala Bwana hatalegea, walahatakuwa mvumilivu kwa wanadamu. WIMBO WA KATIKATI Zab 34:1-2, 16-18, 22 Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima. Katika Bwana nafsi yangu itajisifu, Wanyenyekevu wasikie wakafurahi. (K) Maskini huyu aliita Bwana akasikia Uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya, Aliondoe kumbukumbu lao duniani. Walilia, naye Bwana akasikia, Akawaponya na taabu zao zote. (K) Maskini huyu aliita Bwana akasikia Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa. Bwana huzikomboa nafsi za watumishi wake, Wala hawatahukumiwa wote wamkimbiliao. (K) Maskini huyu aliita Bwana akasikia SOMO LA 2 2 Tim 4:6-8, 16-18 Mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika. Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda; baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake. Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote; nami nikaokolewa katika kinywa cha simba. Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina. SHANGILIO Yn 8:12 Aleluya, aleluya Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana, Yeye anifuataye atakuwa na nuru ya uzima. Aleluya SOMO LA INJILI Lk 18:9-14 Yesu aliwaambia mfano huu watu waliojikinai ya kuwa wao ni wenye haki, wakiwadharau wengine wote. Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru. Yule Farisayo akasimama akiomba hivi moyoni mwake; Ee Mungu, nakushukuru kwa kuwa mimi si kama watu wengine, wanyang'anyi, wadhalimu, wazinzi, wala kama huyu mtoza ushuru. Mimi nafunga mara mbili kwa juma; hutoa zaka katika mapato yangu yote. Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua macho yake mbinguni, bali alijipiga-piga kifua akisema, Ee Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi. Nawaambia, huyu alishuka kwenda nyumbani kwake amehesabiwa haki kuliko yule; kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. https://play.google.com/store/apps/details?id=tk.shajara.shajara

Saturday, 22 October 2016

TAFAKARI 22/10/2016 Jumamosi ya 29 ya Mwaka - C wa Kanisa." Thamani ya wakati wa sasa"


TAFAKARI

      Jumamosi, Oktoba, 22, 2016, Juma la 29 la Mwaka wa Kanisa
        Kumbukumbu ya Mt. Yohane Paulo II, Papa.(hiari)
                 Ef 4:7-16;
             Zab 121:1-5;
                      Lk 13:1-9

      THAMANI YA WAKATI WA SASA!
                Majanga au ajali katika maisha ya watu mara nyingi zinawafanya wajiulize maswali kama vile, kwanini? Au kwanini wao? Katika Injili ya leo Yesu anaeleza juu ya tukio baya lililosababisha vifo vya baadhi ya Wagalilaya waliouwawa na jeshi la Warumi chini ya utawala wa Kamanda Pilato. Kipindi flani watu walisema kwamba hii ilikuwa adhabu ya Mungu kwa hawa watu kwasababu ya maadili yao mabaya. Yesu anakataa akisema mwadhani walikuwa ni wakosefu kuliko watu walioishi Yerusalemu? “Kwahakika hapana!” Alisema.
Kwa uhakika anawaambia Wafuasi wake kwamba nao watakutana na mambo kama hayo wasipobadili mienendo yao.
Dhambi za waliokufa haikuwa sababu ya kifo chao, bali ni onyo kwetu ili kuona kama tupo tayari kwa tukio kama hilo. Yesu anaendelea akielezea maana ya hayo akitumia mfano wa Mtini.
Katika taswira watu aliokuwa anaongea nao walikuwa kama mtini ambao haujazaa matunda. Miaka mitatu iliyotajwa katika mfano huu inaweza kulinganishwa na urefu wa miaka mitatu ya utume wa Yesu. Lakini, bado wana muda wakuchunguza maisha yao, muda ambao hawakupewa wale waliokufa katika matukio yale mawili. Sisi nasi tumepewa muda- siku? Mwezi? Miaka mingi? Hatuna habari juu ya hilo. Lililo wazi ni kwamba hamna muda wa kupoteza, tunaanza leo, na zaidi sana sasa hivi.
Kwa Mungu, miaka iliyopita haijalishi wala si maisha ya baadaye, kinacho jalisha ni “sasa”. Kama nipo naye sasa katika maisha yangu, sina chochote cha kuhofia.
       
            SALA: Bwana nisaidie niweze kutumia vizuri muda ulionipa, niweze kubadili maisha yangu. Amina.

Copyright © 2016 Shajara  and  published  by  MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
      see: imani-katoliki.blogspot.com

Friday, 21 October 2016

MASOMO YA MISA, 22/10/2016 Jumamosi ya 29 ya Mwaka- C


Jumamosi ya 29 ya Mwaka

           SOMO LA 1
       Efe 4:7-16

                Kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. Hivyo husema, Alipopaa juu aliteka mateka, Akawapa wanadamu vipawa. Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi? Naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa juu sana kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote. Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.

Neno la Mungu...... Tumshukuru Mungu.

       WIMBO WA KATIKATI
              Zab 122:1-5

        (1).    Nalifurahi waliponiambia, Na twende nyumbani kwa Bwana. Miguu yetu imesimama Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu.
                (K) Nalifurahi waliponiambia, na twende nyumbani kwa Bwana.
       (2).   Ee Yerusalemu uliyejengwa Kama mji ulioshikamana, Huko ndiko walikopanda kabila, Kabila za Bwana;
               (K) Nalifurahi waliponiambia, na twende nyumbani kwa Bwana.
       (3).    Ushuhuda kwa Israeli, Walishukuru jina la Bwana. Maana huko viliwekwa viti vya hukumu, Viti vya enzi vya mbari ya Daudi.
               (K) Nalifurahi waliponiambia, na twende nyumbani kwa Bwana.

       SHANGILIO
             2Tim. 1:10

                  Aleluya, aleluya, Mwokozi wetu Yesu Kristo alibatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika kwa Injili. Aleluya.

            SOMO LA INJILI
                   Lk 13:1-9

                Wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao. Akawajibu akawaambia, Je! Mwadhani ya kwamba Wagalilaya hao walikuwa wenye dhambi kuliko Wagalilaya wote, hata wakapatwa na mambo hayo? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo.
Au wale kumi na wanane, walioangukiwa na mnara huko Siloamu, ukawaua, mwadhani ya kwamba wao walikuwa wakosaji kuliko watu wote waliokaa Yerusalemu? Nawaambia, Sivyo; lakini msipotubu, ninyi nyote mtaangamia vivyo hivyo. Akanena mfano huu; Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake la mizabibu; akaenda akitafuta matunda juu yake, asipate.
          Akamwambia mtunzaji wa shamba la mizabibu, Tazama, miaka mitatu hii naja nikitafuta matunda juu ya mtini huu, nisipate kitu; uukate, mbona hata nchi unaiharibu? Akajibu akamwambia, Bwana, uuache mwaka huu nao, hata niupalilie, niutilie samadi; nao ukizaa matunda baadaye, vema! La, usipozaa, ndipo uukate.

Neno la Bwana ..... Sifa kwako Ee Mungu.

Copyright © 2016 by Shajara and published  by  MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
   see:   imani-katoliki.blogspot.com

TAFAKARI 21/10/2016 Ijumaa ya 29 ya Mwaka- C

TAFAKARI

           Ijumaa, Oktoba, 21, 2016, Juma la 29 la Mwaka wa Kanisa

          Ef 4:1-6;
      Zab 23:1-6;
              Lk 12:54-59

         KUFAFANUA ALAMA ZA NYAKATI ZETU!
              Injili ya leo kutoka kwa Mt. Luka, inatuelezea ni kwa jinsi ghani watu wakipindi cha Yesu walivyokuwa wakiweza kufafanua majira na nyakati zao, kutambua uso wa nchi na mbingu, lakini walishindwa kutambua alama za Yesu alizoweka mbele ya macho yao katika kutangaza Ufalme wa Mungu. Je, si kweli zaidi hata kwetu sasa? Tumebobea sana katika teknologia na tunajivuna katika hali ya ukuwaji wa sayansi tuliofanya kama jamii, lakini mara nyingi tunakosa ujumbe wa Mungu anaojaribu kuwasiliana nasi kila siku.
  “Alama za nyakati” ilikuwa ni ujumbe muhimu katika mkutano wa pili wa Vatikan, kama ulivyotutaka kuelezea ujumbe wa Mungu katika alama za nyakati zetu, na pia kubaki katika ukweli wa ujumbe wa Yesu na habari njema iliohubiriwa na Mababa wa kanisa.
Wakati watu wanaongelea kuhusu siasa, michezo au dini, mara nyingi midahalo ni ya kutumia nguvu nyingi na hisia.
Lakini tunapoulizwa ni nini mpango wa Mungu katika maisha yetu, wengi wetu twaweza kusema hatujui. Mara nyingi hatuna uhakika na anacho tuambia Mungu tufanye katika maisha yetu, tofauti na mipango yetu na tamaa zetu.
Mara nyingi tunajifanya na kupotea huku tukijifanya hamna chochote kibaya kwa uchaguzi wetu na maamuzi yetu; kwa kifupi, inatuwia vigumu kubadilika.
Mt. Paulo katika somo la kwanza anawaandikia Waefeso akiwaeleza kuwa wajiandae kushika mambo ya msingi kwa kushika njia sahihi. Waenende kadiri ya wito wao walioitiwa na Mungu.

        Sala: Bwana, tusaidie leo, ili tuweze kuelezea kwa usahihi neno lako kwa njia ya alama za nyakati zetu. Amina

MASOMO YA MISA, 21/10/2016 Ijumaa ya 29 ya Mwaka- C

Ijumaa ya 29 ya Mwaka

            SOMO LA 1
         Efe 4:1-6
                 Nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa; kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.
Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja.
Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.

          WIMBO WA KATIKATI
     Zab 24:1-6

           (1).  Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, Dunia na wote wakaao ndani yake. Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha.
                       (K) Hiki ndicho kizazi cha wakufuatao, Ee Bwana.
          (2).    Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili
                      (K) Hiki ndicho kizazi cha wakufuatao, Ee Bwana.
         (3).    Atapokea baraka kwa Bwana, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake. Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.
                     (K) Hiki ndicho kizazi cha wakufuatao, Ee Bwana.
  

           SHANGILIO
       Efe. 1:17, 18

          Aleluya, aleluya, Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, awape roho ya hekima mjue tumaini la mwito wake. Aleluya.

     
          SOMO LA INJILI
                Lk 12:54-59
            Yesu aliwaambia makutano pia, kila mwonapo wingu likizuka pande za magharibi mara husema, Mvua inakuja; ikawa hivyo.
Na kila ivumapo kaskazi, husema, Kutakuwa na joto; na ndivyo ilivyo. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wa nchi na mbingu; imekuwaje, basi, kuwa hamjui kutambua majira haya? Na mbona ninyi wenyewe kwa nafsi zenu hamwamui yaliyo haki? Maana, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidii kupatanishwa naye, asije akakuburuta mpaka mbele ya kadhi; yule kadhi akakutia mikononi mwake mwenye kulipiza, na yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani. Nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.

  
Copyright © 2016 by shajara  and  published  by  MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
   see: imani-katoliki.blogspot.com

TAFAKARI 20/10/2016 Alhamisi ya 29 ya Mwaka- C

TAFAKARI

         
            Alhamisi, Oktoba 20, 2016, Juma la 29 la Mwaka wa Kanisa

             Ef 3:14-21
       Zab 32:1-2, 4-5, 11-12, 18-19
                  Lk 12: 49-53

  
           MUNGU NI MOTO UNAOPENDEZESHA VYOTE.

              Yesu aliwashtuwa wafuasi wake pale aliposema kuwa amekuja kutupa moto na kusababisha mgawanyiko badala ya amani duniani. Je, ni aina gani ya moto ambao Yesu alikuwanao akilini mwake? Moto katika neno la Kibiblia ulihusianishwa na Mungu pamoja na kuhusianishwa na matendo yake ulimwenguni katika maisha ya watu wake. Wakati mwingine Mungu anadhihirisha uwepo wake kwa uwepo wa moto, kama vile kichaka kiwakacho ambacho hakiteketei alipoongea na Musa (Kut 3:2).
Alama ya moto ilitumika pia kuwakilisha utukufu wa Mungu (Eze 1:4, 13), uwepo wa ulinzi wake (2Fal 6:17), utakatifu wake (Kum 4:24), hukumu ya haki (Zek 13:9), na hasira yake dhidi ya dhambi (Isa 66:15-16). Pia imetumika pia ikimaanisha Roho Mtakatifu (Mt 3:11 na Mat 2:3). Moto wa Mungu unasafisha na huondoa uchafu, na unavuvia mwanga na hofu ya kumuabudu Mungu na nguvu ya neno lake ndani yetu. Basi tuchukue mfano mmoja kutoka kwenye Biblia uhusuo moto – kichaka kiwakacho katika kitabu cha Kutoka. Kichaka chaonekana kuwa kinawaka tu badala ya kuteketea. Sifa ya asili ya moto ni kuchoma na kuteketeza. Lakini kinachotokea hapa ni hali ya tofauti.
Je, unasema nini juu ya Mungu wetu? Ndio Mungu wetu ni moto, sio moto uharibuo bali moto unaobadilisha. Unatuunguza sisi kufikia uzuri. Mara utakapo unguzwa na moto huu katika uhalisia unakuwa kiumbe kipya, unatoka kwenye uovu na kusimama njee. Kama upo katika familia yako ya watu wanne na ukawa umeunguzwa mpaka kufikia uzuri katika uhalisia utakuwa nje.
Unasimama njee ukiwa tofauti na hapo huenda ukachukiwa au kupendwa au kuigwa. Inawezekana familiya yetu na marafiki zetu kuwa maadui zetu. Kama mawazo yao yatatuzuia sisi kutenda yale tunayoyajua kuwa Mungu anapenda sisi kuyafanya ni dhahiri tutamtii Mungu zaidi kuliko wao, na hapo huenda uadui ukawepo. Je, upendo wa Yesu Kristo unakusukuma wewe kumuweka Mungu kwanza kwa yale yote uyatendayo (2 Kor 5:14)?

     
            Sala: Bwana, naomba upendo wako unitawale na uyarekebishe maisha yangu. Amina

MASOMO YA MISA, 20/10/2016 Alhamisi ya 29 ya Mwaka- C

Alhamisi ya 29 ya Mwaka

        SOMO LA 1
                Efe 3:14-21
          Nampigia Baba magoti, ambaye kwa jina lake ubaba wote wa mbinguni na wa duniani unaitwa, awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu. Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu; naam, atukuzwe katika Kanisa na katika Kristo Yesu hata vizazi vyote vya milele na milele. Amina.

Neno la Mungu....... Tumshukuru Mungu.

           WIMBO WA KATIKATI
       Zab 33:1-2, 4-5, 11-12, 18-19

        (1).    Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. Mshukuruni Bwana kwa kinubi, Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.
                    (K) Nchi imejaa fadhili za bwana.
       (2).   Kwa kuwa neno la Bwana lina adili, Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu. Huzipenda haki na hukumu, Nchi imejaa fadhili za Bwana.
                   (K) Nchi imejaa fadhili za bwana.
        (3).  Shauri la Bwana lasimama milele, Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi. Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, Watu aliowachagua kuwa urithi wake.
                  (K) Nchi imejaa fadhili za bwana.
        (4).   Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao, Wazingojeao fadhili zake. Yeye huwaponya nafsi zao na mauti, Na kuwahuisha wakati wa njaa.
                  (K) Nchi imejaa fadhili za bwana.

       SHANGILIO
             Yn. 17: 17
              Aleluya, aleluya, Neno lako ndiyo kweli, Ee Bwana, ututakase kwa ile kweli. Aleluya.

      SOMO LA INJILI
         Lk 12:49-53
              Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Nimekuja kutupa moto duniani; na ukiwa umekwisha washwa, ni nini nitakalo zaidi? Lakini nina ubatizo unipasao kubatiziwa, nami nina dhiki kama nini hata utimizwe! Je! Mwadhani ya kwamba nimekuja kuleta amani duniani? Nawaambia, La, sivyo, bali mafarakano.
  Kwa kuwa tokea sasa katika nyumba moja watakuwamo watu watano wamefarakana, watatu kwa wawili, wawili kwa watatu. Watafarakana baba na mwanawe, na mwana na babaye; mama na binti yake, na binti na mamaye; mkwe mtu na mkwewe, mkwe na mkwe mtu.

Neno la Bwana ....... Sifa kwako Ee Kristo.

Wednesday, 19 October 2016

TAFAKARI: 19/10/2016 Juma la 29 la Mwaka- C " Wito wa kuwa Mwaminifu."


TAFAKARI

         Jumatano, Oktoba 19, 2016, Juma la 29 la Mwaka wa Kanisa
             Ef 3:2-12;
         Is 12:2-6;
                 Lk 12:39-48


            UFUASI: WITO WA KUWA MWAMINIFU, SI KWAAJILI YA MAFANIKIO!
                   Uaminifu na ukweli ni mambo makuu matakatifu na mazuri kabisa yaliowekwa kama zawadi katika akili ya mwanadamu. Kuwa mwaminifu katika mambo madogo sana ni njia ya kuelewa, kuboresha, na kuelezea nguvu itakiwayo kutenda mambo makubwa.
Uaminifu si kutenda mambo sahihi mara moja tu nakuacha, bali kufanya mambo sahihi mara zote na zaidi ya kawaida. Mfano katika Injili unatutaka sisi kuwa tayari, kuwa waaminifu kila wakati, tutende mema na kuwa waaminifu si kwasababu tunaogopa siku ya mwisho bali tutende wema na kuwa waaminifu kwani ndio tabia ya Kimungu. Je, kadiri ya Yesu nini maana ya uaminifu? kuyashika maneno ya mtu husika, ahadi, na majitoleo, bila kujali unapata ugumu au hatari ya namna gani.
Uaminifu ni sifa ya msingi ya Mungu na ndiyo anayoitegemea kutoka kwetu. Bahati nzuri Mungu pia anatoa neema na nguvu ya kutusaidia kubaki waaminifu na anatarajia sisi tuvitumie vema vipaji na neema atukirimiazo sisi.
Wale wote wanaojua mwalimu wao anahitaji nini (kama wafuasi wake) lakini wanatenda mambo mabaya atakapo rudi atawaadhibu vibaya sana.
Wale wote wasio jua (wasio wafuasi, watu wa nje) bado wataadhibiwa kwa kufanya makosa lakini adhabu yao itakuwa ndogo.
       Basi tusijifanye kuwa wajinga na kuziacha kazi na majukumu yetu. Imani katika kipimo cha ukamilifu hutufanya sisi kuwa ‘waaminifu’ na wakati tukiwa waaminifu, watu wanapata matumani ‘kujiaminisha kwetu na kwa pamoja tunajiunga na kumwamini Mungu na kuwa mwaminifu kwake.
   Je, sisi tu waaminifu kwa Mungu na tupo tayari kumtolea yeye hesabu ya uaminifu wetu?

            Sala: Bwana tusaidie sisi tuwe waaminifu daima, kwasababu katika uaminifu tunapata nguvu zetu. Amina


Copyright © 2016  by Shajara  and  published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
      see: imani-kayoliki.blogspot. com

MASOMO YA MISA, 19/10/2016 Juma la 29 la Mwaka


Jumatano ya 29 ya Mwaka

       SOMO LA 1
            Efe. 3:2 – 12

                  Mmesikia habari ya uwakili wa neema ya Mungu niliyopewa kwa ajili yenu; ya kwamba kw akufunuliwa nalijulishwa siri hiyo, kama nilivyotangulia kuandika kwa maneno machache. Kwa hayo, myasomapo, mtaweza kuutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo. Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine; kama walivyofunuliwa mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho; ya kwamba Mataifa ni warithi pamoja nasi wa urithi mmoja, na wa mwili mmoja, na washiriki pamoja nasi wa ahadi yake iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya Injili; Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake.
Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika; na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote; ili sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu war oho; kwa kadiri ya kusudi la milele alilolikusudia katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini.

Neno la Mungu ...... Tumshukuru Mungu.


             WIMBO WA KATIKATI
             Isa. 12:2 – 6

          (1).   Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana Bwana Yehova ni nguvu zangu Na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu. Basi, kwa furaha mtateka maji Katika visima vya wokovu.
                    (K) Kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.
         (2).     Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa, Litajeni jina lake kuwa limetukuka. Mwimbieni Bwana.
                    (K) Kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.
         (3).   Kwa kuwa ametenda makuu, Na yajulikane haya katika dunia yote. Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni; Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.
                    (K) Kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu.


        SHANGILIO
            Yn. 14:23
                       Aleluya, aleluya, Mtu akinipenda, atalishika neno langu, na Baba yangu atampenda, na sisi tutakuja kwake. Aleluya.


        SOMO LA INJILI
              Lk. 12:39-48

            Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Fahamuni neno hili, Kwamba mwenye nyumba angalijua saa atakayokuja mwivi; angalikesha, wala asingaliacha nyumba yake kuvunjwa. Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo ajapo Mwana wa Adamu.
    Petro akamwambia, Bwana, mithali hiyo umetuambia sisi tu, au watu wote pia? Bwana akasema, Ni nani, basi, aliye wakili mwaminifu, mwenye busara, ambaye bwana wake atamweka juu ya utumishi wake wote, awape watu posho kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta anafanya hivyo.
Kweli nawaambia, atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini, mtumwa yule akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia kuja, akaanza kuwapiga wajoli wake, wanaume kwa wanawake, akila na kunywa na kulewa; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wasioamini. Na mtumwa yule aliyejua mapenzi ya bwana wake, asijiweke tayari, wala kuyatenda mapenzi yake, atapigwa sana. Na yule asiyejua, naye amefanya yastahiliyo mapigo, atapigwa kidogo. Na kila aliyepewa vingi, kwake huyo vitatakwa vingi; naye waliyemwekea amana vitu vingi, kwake huyo watataka na zaidi.

Neno la Bwana ..... Sifa kwako Ee Kristo.


Copyright © 2016  by  Shajara  and published by  MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
       see: imani-katoliki.blogspot.com

TAFAKARI: 19/10/2016 Juma la 29 la Mwaka- C wa Kanisa " Sikukuu ya Mt. Luka Mwinjili."


TAFAKARI

          Jumanne, Oktoba 18, 2016, Juma la 29 la Mwaka wa Kanisa
       Sikukuu ya Mt. Luka Mwinjili,
               2 Tim 4:10-17
           Zab 144:10-13, 17-18
                 Lk 10: 1-9
       

        TUMEITWA KUWA MASHAHIDI WA YESU!

                   Katika Injili, Luka leo anatuonesha tena wengine sabini ambao Yesu anawatuma baada ya kupokea maelekezo.
Luka lazima atakuwa pia ni mmoja wapo wa Wafuasi waliotumwa kwa utume.
   Ni vigumu kwa mtu ambaye hakuwa karibu na Yesu kufahamu namna hiyo na kuweka katika mpangilio katika kumwelezea kama mtu mkamilifu. Sisi pia maagizo haya yanatolewa kwetu.
           Tunapaswa kujitoa kwa ufahamu wetu wote kuhubiri Ufalme wa Mungu na sio kuyumbishwa na vitu vingine vidogo.
       Kufanya haya ni lazima kusafiri na mwanga-chukua tu, vile vya muhimu na tuacha nyuma yote ambayo yanaweza kutuharibu. Tunakaribishwa kufanya kazi hii, si kwasababu ya chochote tutakachopata kutokana nayo, bali kwa yale tutakayo wapa wengine bila malipo, bila kutegemea heshima Fulani au malipo flani. Bwana anataka wafuasi wake wamtegemee yeye na sio kujitegemea wenyewe.
 
           Sala: Bwana, naomba furaha na ukweli wa Injili ubadili maisha yangu ili niweze kuutoa ushuhuda kwa wale wote walioo karibu name. Amina

Copyright © 2016  by  Shajara  and published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
   see: imani-katoliki.blogspot.com

MASOMO YA MISA, 18/10/2016 Juma la 29 la Mwaka.


Jumanne ya 29 ya Mwaka

        SOMO LA 1
               Efe. 2:12 – 22

            Msisahau kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani. Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo.
Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba.
Akaja akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani kwao wale waliokuwa karibu. Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja. Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.
        Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe na jiwe kuu la pembeni. Katika yeye jingo lote linaungamanishwa vema na kuku ahata liwe hekalu takatifu katika Bwana.
Katika ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.
   

          WIMBO WA KATIKATI
               Zab. 85:9 – 14

             Nisikie atakavyosema Bwana, Maana atawaambia watu wake amani. Hakika wokovu wake u karibu na wamchao, Utukufu ukae katika nchi yetu.
                            (K) Bwana anawaambia watu wake amani.
              Fadhili na kweli zimekutana, Haki na amani zimebusiana. Kweli imechipuka katika nchi, Haki imechungulia kutoka mbinguni.
                            (K) Bwana anawaambia watu wake amani.
               Bwana atatoa kilicho chema, Na nchi yetu itatoa mazao yake. Haki itakwenda mbele zake, NATO itazifanya hatua zake kuwa njia.
                            (K) Bwana anawaambia watu wake amani.


           SHANGILIO
      Yn. 10:27

                        Aleluya, aleluya, Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata. Aleluya.

            SOMO LA INJILI
        Lk. 12:35-38

                      Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Viuno vyenu na viwe vimefungwa, na taa zenu ziwe zinawaka; nanyi iweni kama watu wanaomngojea bwana wao, atakaporudi kutoka arusini, ili atakapokuja na kubisha, wamfungulie mara.
Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha. Amin, nawaambieni, atajifunga na kuwakaribisha chakulani, atakuja na kuwahudumia.
Na akija zamu ya pili, au akija zamu ya tatu, na kuwakuta hivi, heri watumwa hao.

Copyright © 2016  by shajara  and  published  by  MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
    see: imani-katoliki.blogspot.com

Monday, 17 October 2016

TAFAKARI: 17/10/2016 Juma la 29 la Mwaka- C


TAFAKARI

         Jumatatu, Oktoba 17, 2016,
      Juma la 29 la Mwaka wa Kanisa

                  Kumbukumbu ya Mt. Ignasio wa Antokia, Askofu na Mfiadini
                Ef 2:1-10
          Zab 100:2-5
                Lk 12:13-21

         KUWA TAJIRI KUMWELEKEA MUNGU!
         Katika somo la kwanza, Mt. Paulo, kwa barua yake kwa Waefeso, inatoa ufafanuzi mzuri kuhusu kazi ya Mungu ya ukombozi ndani ya Yesu Kristo, kwa mapendo yake kwa wanadamu.
“Mungu ambaye ni mwingi wa huruma” anasema, “kutoka katika mapendo yake makubwa aliotupenda nayo, hata tulipokufa katika dhambi kwa njia ya makosa yetu, alitufanya hai pamoja na Kristo”. Anamalizia na kitu ambacho Mungu anategemea katika maisha yetu: “sisi tupo kwa jinsi alivyo tuumba, alituumba katika Kristo kwa kazi njema alio andaa Mungu mbele yetu iwe njia yetu ya maisha”.
Mfano uliopo katika Injili kuhusu tajiri mpumbavu unatoa mlio kamili wa tafakari ya somo la kwanza. Baada ya kuelezea nafasi ya tajiri bahili asiyetaka kumpa Mungu chochote kwa yale anayopata, na kudhani yote ni mali yake, kutumia anavyopenda, Yesu anasema wazi “ni kama wale wanaojiwekea akiba kwa ajili yao binafsi na wala sio matajiri katika kumwelekea Mungu”. Mungu kwa njia ya upendo ametupa sisi, sio tu vitu mbali mbali bali kitu muhimu kabisa, zawadi ya Imani yetu ndani ya Yesu Kristu iliotuletea ukombozi. Pia, “na kila mmoja aliyepewa vingi, vingi vitatakwa kwake, na kwa aliyekabidihiwa vingi, vingi vitatakwa zaidi”, (Lk 12:48).
Hatuwezi kusema tunakuwa ‘watu wema zaidi’ kwasababu ni wakarimu, “Mungu aliandaa haya kabla, yawe njia yetu ya maisha”.
Kwahiyo, hatuwezi kusema tunanunua ukombozi wetu kwasababu tunafanya matendo mema.
      Mt. Paulo anaeleza wazi kwamba, “kwa neema ya Mungu mmekombolewa kwa njia ya Imani, na hili sio kwamba mmelisababisha ninyi, bali ni zawadi ya Mungu-sio matokeo ya kazi zenu”. Kwasababu tumepokea zawadi ya ukombozi, tunapaswa kuwa watu wa matendo ya huruma, na sio kinyumbe chake . Kwa hiyo, Yesu anatuambia kuwa “tuwe matajiri katika kumwelekea Mungu” ambaye amekuwa mkarimu bila kipimo juu yenu.
Kwa maneno mengine, muwe wakarimu katika kufanya mapenzi yake, kwa kushika amri zake, kwa kumpa utukufu kwa kila kitu unachofanya.

         Sala: Bwana, nakushukuru kwa zawadi zako. Nisaidie niweze kuwashirikisha wengine. Amina.


Copyright © 2016 shajara  and  published  by  MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
      see: imani-katoliki.blogspot.com

MASOMO YA MISA, 17/10/2016 Juma la 29 la Mwaka.


Jumatatu ya 29 Mwaka

     SOMO LA 1
      Efe. 2:1 – 10

             Mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye zake sasa katika wana wa kuasi; ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili nay a nia, tukawa kwa tabia yenu watoto wa hasira kama na hao wengine. Lakini Mungu, kw akuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani mmeokolewa kwa neema.
Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu war oho, katika Kristo Yesu. Ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu. Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya Imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.


            WIMBO WA KATIKATI
    Zab. 100

                  Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote; Mtumikieni Bwana kwa furaha; Njoni mbele zake kwa kuimba.
                           (K) Ndiye aliyetuumba, na sisi tu watu wake.
                Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
                            (K) Ndiye aliyetuumba, na sisi tu watu wake.
                  Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake.
                            (K) Ndiye aliyetuumba, na sisi tu watu wake.
                   Kwa kuwa Bwana ndiye mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake vizazi na vizazi.
                             (K) Ndiye aliyetuumba, na sisi tu watu wake.


           SHANGILIO
      Yn. 8:12

                    Aleluya, aleluya, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima. Aleluya.

             SOMO LA INJILI
        Lk. 12;13-21

                  Mtu mmoja katika mkutano alimwambia Yesu, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu. Akamwambia, Mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu? Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu.
Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.


Copyright © 2016 Shajara  and  published  by  MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
     see: imani-katoliki.blogspot.com

TAFAKARI: 16/10/2016 Dominika ya 29 ya Mwaka.


TAFAKARI

          Jumapili, Oktoba 16, 2016, 
          Dominika ya 29 ya Mwaka

JUMAPILI YA UMISIONARI ULIMWENGUNI 2016
              Kut 17: 8-13
         Zab 121: 1-8
                2 Tim 3:14 – 4:2
           Lk 18: 1-8

        KANISA LA KIMISIONARI, LENYE KUSHUHUDIA HURUMA!
                Ulishawahi kujiuliza, “wakati mtu anavyokuwa Mkristo, kwanini Mungu asiwachukue moja kwa moja Mbinguni?” jibu ni kwamba Mungu amempa kila mtu kazi ya kutimiza, uliumbwa kuwa mmisionari. Umisionari unaanza na maneno ya Yesu katika Injili Mt. 4:18 “njoo nifuate, nitakufanya kuwa mvuvi wa watu”.
Ilikuwa wazi kwamba wakati Yesu alivyokuwa akiwaita watu hakuwaita kwenye dini flani bali aliwaita wawe wajumbe wa Injili kwa umisionari.
   Hakuwaita waje kwenye Sinagogi, au kushika Torati, bali maisha ya ufuasi kamili. Matendo ya Mitume 1:8, tunaona kwamba kabla ya kupaa kwake, Yesu anawaambia wafuasi wake kwamba watakuwa mashahidi wake katikaYerusalemu, Yudea, Samaria mpaka miisho ya dunia.
Na katika Matendo ya Mitume 2, Roho Mtakatifu alimiminwa kwa watu wa Mungu kama zawadi ya kuwasaidia kuendeleza ujumbe wa Mungu ulimwenguni.
Tangu siku ya Pentekoste umisionari wa Mungu umeendelea hadi leo. Unaendelea pande zote, huku Kristo akiwa kiini cha umisionari. Umisionari ni kitu ambacho sisi wote tumealikwa kukifanya, na kujiingiza ndani yake.
Kujiingiza kwenye umisionari maana yake kuwa shuhuda wa Yesu na kwa kuhubiri kile tunacho kiamini na kukiishi katika maisha yetu ya kila siku kwa vitendo, vitendo vya upendo kwa Mungu na upendo kwa watu wote. Mungu wa Biblia sio Mungu wa kujiwekea umashuhuri. Kwanza anatutikisa sisi, na hapo anatutumia sisi kuutikisa ulimwengu.
Na hivyo kila wakati kuwa wajumbe wa Mungu. Wakati Mungu alivyotaka kubadili dunia alimwambia Noah, afanye kitu ambacho hakuwa amewahi kukifanya kabla,(kutengeneza safina) kujiandaa kwa kitu ambacho hakuwahi kukiona kabla (mvua kumbwa). Wakati Mungu alivyotaka kuleta taifa kubwa, alimwita Abram, akamwambia aondoke katika Ur ya Wakaldea. Wakati Mungu alivyotaka kuwaokoa watu wake, alimpata kwanza kijana ambaye hakuwa muongeaji sana (Musa) na kumtuma kwa Farao. Wakati Mungu alivyomtaka mtu wa kumuangamiza Goliath, alimchagua kijana mdogo tena mchungaji, Daudi. Wakati Mungu alivyotaka kuwaokoa watu wake kutoka katika uharibifu, alimchagua mschana mdogo tu anaitwa Esta.
Wakati Kristo alivyotaka watu wawe katika mzunguko wake wa ndani wa ujumbe wake, aliwachagua wavuvi na watoza ushuru. Kijana muongeaji tena asana, Petro na ndugu wawili waitwao “wana wa ngurumo” na kuwaambia waache kila kitu wamfuate. Shahidi ni mtu ambaye anayasema yale aliyeona na kuyashuhudia. Ni hivyo tu. Mtu haihitaji kuwa mwana theologia mkubwa. Wewe ni mtaalamu kwa yale unayo amini na kuyaishi.
Unachopaswa kufanya shirikisha yale Mungu aliyokutendea katika maisha yako. Kila Mmmoja wetu ameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Barua ya mtume Paulo kwa Wathesalonike inadai uangalifu mkubwa “kuhubiri Injili inadhihirisha kwamba sio maneno yenu matupu, bali moja wapo ya nguvu”.
Habari njema kama Paulo alivyo ihubiri kwa Wayunani katika zama hizo, walikuwa hawaja anguka katika ukiziwi na mioyo migumu; hivyo ilipokelewa kwa furaha na kuiruhusu kumea katika udongo mzuri wa Imani na matumaini. Kwa njia ya nguvu za Roho Mtakatifu zilizo ndani ya Paulo na wale wote waliopokea Imani hiyo, Injili ya Yesu ilimwilishwa na kuingia ndani mwao, ushuhuda wa kweli katika thesalonika.
Je, sio muda sahihi sasa lengo letu, habari njema ina hubiriwa? Je, tunapaswa tuishirikishe wapi habari hii Njema. Je, umisionari huu unawezekana? Nianzie wapi? Hapa hapa tulipo. Katika Yerusalemu yetu, kwa marafiki zetu, familia, wafanyakazi wenzetu, ndugu zetu, kwa watu wote wanaopita katika maisha yetu. Na hapo ndio sehemu ya pili tunapaswa kufanya hayo, sio tu katika Yerusalemu yetu, bali pia katika Yudea na samaria Yesu alisema. Na hawa ni kondoo, haya ni maeneo tunayofika tofauti na mazingira ya Yerusalemu yetu, watu waliokaribu yetu wasio wa asili ya tamaduni zetu, elimu yetu, pengine uchumi wetu. Paulo anasema “Nimekuwa hali zote kwa, watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa watu.” (1Kor 9:22) Jubilee hii ya hali ya Juu kabisa ya Huruma, ambayo Kanisa ina iadhimisha, inatoa mwanga tofauti katika Ulimwengu.
                 Inatoa mwanga tofauti katika jumapili ya leo ya umisionari; inatualika tuone na kuchukulia utume/umisionari wa Kanisa kama kazi kubwa ya huruma, katika Nyanja zote mbili kiroho na kimahitaji ya mwili. Katika siku hii ya umisionari, sisi wote tunaitwa “kwenda njee” kama wafuasi wa umisionari, kila mmoja kwa ukaribu kushirikisha vipaji vyake, ubunifu, hekima na uzoefu wake ili kuleta ujumbe wa Mungu wa ukarimu na huruma katika familia yote ya ubinadamu.
           Kwa njia ya fadhila ya umisionari, Kanisa lina wajali wale wote wasio ijua Injili, kwasababu linataka kila mtu akombolewa na kushuhudia Upendo wa Mungu. Kanisa “lina agizwa kuhubiri huruma ya Mungu, iliyo mapigo ya moyo wa Injili,” (Misericordiae Vultus, 12) katika kila kona ya Ulimwengu, ikimkuta kila mtu, mdogo au mkubwa. Watu wote na tamaduni zote wana haki ya kupokea ujumbe wa Injili ya ukombozi ambayo ni zawadi ya Mungu kwa kila mtu. Hii ni zaidi ya jinsi tunavyofikiri, ni zaidi ya jinsi ghani tunavyo fikiria kulivyo na ukosefu wa haki, vita, migongano mbali mbali inayohitaji usuluhisho katika dunia. Wamisionari wanajua Kwamba katika Injili ya msamaha na huruma inaleta furaha na msamaha, haki na Amani. Mwaliko wa Injili kwamba “nendeni ulimwenguni kote mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi wangu, mkiwa batiza kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, mkiwafundisha yote niliowafundisheni” (Mt 28:19-20) haupaswi kuachwa; bali wito huu ni kwetu wote katika nyakati zetu pamoja na changamoto zake zote, tusikie wito wa kuwa mmisionari mpya. Kila Mkristo na kila jumuiya wanapaswa kuchagua ile njia alioonesha Bwana, sisi wote tunaagizwa kutii wito wake, kwenda njee ya maeneo yetu ili kuzifikia sehemu za “mwisho kabisa,” zinazo hitaji mwanga wa Injili” (Evangelii Gaudium, 20).
      Tusifunge mioyo yetu, nakujiweka katika mahitaji yetu binafsi tu, bali tuifungue kwa wanadamu wote. 

                 Sala: Bwana, nipo hapa, nitume mimi kwenye umisionari wako. Amina

MASOMO YA MISA, Dominika ya 29 ya Mwaka.

Dominika 29 ya Mwaka

        SOMO LA 1
               Kut 17:8-13
         Wakati huo Waamaleki wakatokea, wakapigana na Israeli huko Refidimu.
Musa akamwambia Yoshua, Tuchagulie watu, ukatoke upigane na Waamaleki; kesho nitasimama juu ya kilele kile, na ile fimbo ya Mungu nitakuwa nayo mkononi mwangu. Basi Yoshua akafanya kama Musa alivyomwambia, akapigana na Amaleki; na Musa na Haruni na Huri wakapanda juu ya kile kilima. Ikawa, Musa alipouinua mkono wake, Israeli walishinda; na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda.
Lakini mikono ya Musa ilikuwa mizito; basi wakatwaa jiwe, wakaliweka chini yake akalikalia. Haruni na Huri wakaitegemeza mikono yake, mmoja upande huu na mmoja upande huu; mikono yake ikathibitika hata jua lilipokuchwa. Yoshua akawaangamiza Amaleki na watu wake kwa ukali wa upanga.

        WIMBO WA KATIKATI
             Zab 121
          Nitayainua macho yangu niitazame milima, Msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.
                   (K) Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.
          Asiuache mguu wako usogezwe; Asisinzie akulindaye; Naam, hatasinzia wala hatalala usingizi, Yeye aliye mlinzi wa Israeli.
                    (K) Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.
             Bwana ndiye mlinzi wako; Bwana ni uvuli mkono wako wa kuume. Jua halitakupiga mchana, Wala mwezi wakati wa usiku.
                   (K) Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.
              Bwana atakulinda na mabaya yote, Atakulinda nafsi yako. Bwana atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.
                  (K) Msaada wangu u katika Bwana, Aliyezifanya mbingu na nchi.

        SOMO LA 2
              2Tim 3:14- 4:2
           Wewe ukae katika mambo yale uliyofundishwa na kuhakikishwa, kwa maana unajua ni akina nani ambao ulijifunza kwao; na ya kuwa tangu utoto umeyajua maandiko matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake; lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.

         SHANGILIO
              Yn 17:17
           Aleluya, aleluya Neno lako ndiyo kweli, ee Bwana; Ututakase sisi kwa ile kweli Aleluya
 

         SOMO LA INJILI
        Lk 18:1-8
                  Yesu aliwaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa. Akasema, Palikuwa na kadhi katika mji fulani, hamchi Mungu, wala hajali watu. Na katika mji huo palikuwa na mwanamke mjane, aliyekuwa akimwendea-endea, akisema, Nipatie haki na adui wangu. Naye kwa muda alikataa; halafu akasema moyoni mwake, Ijapokuwa simchi Mungu wala sijali watu, lakini, kwa kuwa mjane huyu ananiudhi, nitampatia haki yake, asije akanichosha kwa kunijia daima. Bwana akasema, Sikilizeni asemavyo yule kadhi dhalimu.
Na Mungu, je! Hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, naye ni mvumilivu kwao? Nawaambia, atawapatia haki upesi; walakini, atakapokuja Mwana wa Adamu, je! Ataiona imani duniani?

Saturday, 15 October 2016

TAFAKARI:15/10/2016 Juma la 28 la Mwaka. " Imani iliyo Jaribiwa" .

TAFAKARI
 
          Jumamosi, Oktoba 15, 2016, Juma la 28 la Mwaka

         Kumbukumbu ya Mt. Teresia wa Avila, Bikira na Mwalimu wa Kanisa

           Efe 1: 15-23;
         Zab 8: 2-7;
              Lk 12: 8-12.

       IMANI ILIYO JARIBIWA!
             Nguvu na uwezo unajaribiwa zaidi ya kuwa na vyeti.
Hii ni kweli pia katika Imani yetu. Sio wengi watakao simama katika kujaribiwa huku kwa Imani. Yesu analifahamu hili na anataka kutoa somo kamili katika Injili. Masharti yake kama vile, ‘Kama” “Lakini” yanamuonesha wito wake kwetu wa kuwa makini. Haongei kwa mafumbo wala mfano.
Anataka Imani kamili isiotikiswa kwa Mungu na msukumo kamili katika kumfuata Yeye katika hali zote. Kukubali kwamba wewe ni Mkristo kwa baadhi ya Nchi inamaana umejitangazia kifo.
Na sehemu nyingine, ina maana umejitangazia, mateso, kukataliwa baadhi ya huduma au kuto kuchaguliwa kwa ajili ya jambo flani. Ni katika hali hiyo pia kumkubali Kristo inaweza kuhatarisha mambo binafsi, usalama wako wa kifedha na umuhimu wako pengine.
Lakini Yesu anasisitisa kwamba kama tunataka kukubaliwa mbinguni mbele ya Malaika watakatifu kama watoto wa kweli wa Mungu, tunapaswa kukiri ukweli huo mbele ya ulimwengu, hata katika mateso na kutengwa.
Kanisa lina wakumbuka watakatifu kwa sababu hii. Utukufu wao ni matokeo ya Imani yao na kujitoa kwao katika maisha yao ya Ukristo. Mt. Teresia wa Avila ambaye tunamkumbuka leo ni mmoja wapo katika hili. Mwanamke aliyekuwa na Imani ya juu kabisa, alipighana na mambo yote yaliokuwa kinyume wakati wake ili kuleta mabadiliko katika shirika la Wakarmeli.
Maisha ya sala yalikuwa ndio silaha yake kuu, na zaidi ya yote Yesu aliyesema “ msiwe na wasi wasi mtasema nini” kila mara alisimama kadiri ya Imani yake.
Huu ndio wito wetu kuwa imara katika kila hali.

            Sala: “Kusiwe na kitu cha kukusumbua. Kila kitu kitapita. Mungu habadiliki. Uvumilivu unapata mambo yote. Hahitaji kitu mtu aliye na Mungu. Mungu mwenyewe anatenda”. Amina.

Copyright © 2016 shajara  and  published  by  MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
       see:  imani-katoliki.blogspot.com

MASOMO YA MISA, 15/10/2016 Juma la 28 la Mwaka. " Kumbukumbu ya Mt. Teresia wa Avila, Bikira na Mwalimu wa Kanisa.

KUMBUKUMBU YA MT. TERESIA WA AVILA, BIKIRA NA MWALIMU WA KANISA

     SOMO LA 1
          Efe 1:15-23
              Tangu nilipopata habari za Imani yenu katika bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote, siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu, Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu awape ninyi roho wa hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, tumjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo ;na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo.
Kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake;ulipotenda katika kristo alipomfufua katika wafu,akamwekea mkono wake wa kuume katika ulimwngu wa roho ; juu sana katika ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani na kila jina litajwalo wala si ulimwenguni humu tu bali katika ule ujao pia akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.

Neno la Mungu ...... Tumshukuru Mungu.

     
         WIMBO WA KATIKATI
        Zab 8:1-6
         (1).   Wewe Mungu Bwana wetu, Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani mwote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni; Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao.
                   (K) Umemtawaza mwanao juu ya kazi za mikono yako
       (2).    Nikiziangalia mbingu zako, Kazi ya vidole vyako, Mwezi na nyota ulizoziratibisha, Mtu ni kitu gani hat umkumbuke Na binadamu hata umwangalie.
                   (K) Umemtawaza mwanao juu ya kazi za mikono yako
      (3).    Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
                   (K) Umemtawaza mwanao juu ya kazi za mikono yako

         SHANGILIO
       Mt 11:35
               Aleluya, Aleluya Nakushukuru baba Bwana wa mbingu na nchi Kwa kuwa mambo haya uliyaficha Wenye hekima na akili Ukawafunulia watoto wachanga Aleluya.

           SOMO LA INJILI
                Lk 12:8-12
             Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Nami nawaambia, kila atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu; na mwenye kunikana mbele ya watu, huyo atakanwa mbele ya malaika wa Mungu. Na kila mtu atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali aliyemkufura Roho Mtakatifu hatasamehewa. Na watakapowapeleka ninyi mbele ya masinagogi na maliwali na wenye mamlaka, msifadhaike kwa kuwaza maneno yenu jinsi mtakavyojibu au kusema; kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema.

Neno la Bwana......  Sifa Kwako Ee kristu.

Copyright © 2016 shajara  and  published  by  MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
      see:  imani-katoliki.blogspot.com

TAFAKARI: 14/10/2015 Juma la 28 la Mwaka. "Kutangaza injili bila woga."

TAFAKARI

            Ijumaa, Oktoba 14, 2016,
   Juma la 28 la Mwaka

          Ef 1:11-14;
   Zab 32:1-2, 4-5, 12-13;
          Lk 12:1-7
   

          KUTANGAZA INJILI BILA WOGA!
                 Je, inakusumbua kuhusu wengine wana waza nini juu yako? Kwa namna unavyo vaa? Kwa namna unavyosema? Je, unashindwa kufanya kitu flani au kutokufanya kwasababu mtu flani atafikiri je? Hii ndio hofu ya mwanadamu na hii sio hofu sahihi. Hofu sahihi ni hofu ya Mungu, kuhusu anachofikiri na anacho tuamuru, na nini anacho tegemea. Lakini sio kwa hofu kama ya mtu anaye adhibu.
Hofu ya mwamini ni heshima kwa Mungu. Hofu hii ni msukumo wetu wakujikabidhi kwa Muumbaji wa ulimwengu. Ambaye ni Mungu. Katika Injili ni mwaliko wa kuwa bila hofu na hasa wakati wa majaribu na mateso. Mkristo hapaswi kuwa na hofu anavyo hubiri Injili ya upendo, ndio, hata katika mapaa ya nyumbani.
Ili kuhubiri huku kuwe na matunda kamili, Mungu amesia ndani mwetu na kututia mafuta kwa Roho Mtakatifu (Efe 1:13; 2 Kor 1:21) kama kusimikwa kwetu kwanza kwa ajili ya safari ya wokovu wetu. Hatujapokea roho wa utumwa wa kutupeleka kwenye hofu, bali Roho wa Mwana ambaye kwa njia yake tunalia ‘Abba Baba” (Rumi 8:15). Kwa ajili ya kuhubiri kusiko na hofu, na sio kuanguka kwenye hofu na ni vizuri kwamba tukuwe katika Roho Mtakatifu.

       Sala: Bwana, tusaidie tuweze kutenda kwa kadiri wa Roho asiye na hofu, ambaye umetuita kuhubiri katika Injili. Amina.

Copyright © 2016 shajara and published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
see: imani-katoliki.blogspot.com

MASOMO YA MISA, 14/10/2016 Juma la 28 la Mwaka.


SOMO LA 1

             Efe 1:11-14

       Ndani yake kristo sisi nasi tulifanywa urithi, huku tukichaguliwa tangu awali sawasawa na kusudi lake yeye, ambaye hufanya mambo yote kwa shauri la mapenzi yake. Nasi katika huyo tupatane kwa sifa ya utukufu wake sisi tulio tangulia kumwekea Kristo tumaini letu.
Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye mtakatifu.
Ndiye aliye arabuni ya urithi wenu, ili kuleta ukombozi wa milli yake, kuwa sifa ya utukufu wake.

       WIMBO WA KATIKATI
           Zab 33:1-2, 4-5, 12-13

           Mpigieni Bwana vigelegele enyi wenye haki Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo Mshukuruni bwana kwa kinubi Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa
                        (K) Heri Taifa, Mungu aliowachagua kuwa urithi wake.
            Kwa kuwa neno la Bwana lina adili Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu Huzipenda haki na hukumu Nchi imejaa fadhili za Bwana
                        (K) Heri Taifa, Mungu aliowachagua kuwa urithi wake.
            Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao Watu waliochaguliwa kuwa urithi wake Toka mbingu bwana huchungulia Huwatazama wanadamu wote pia
                         (K) Heri Taifa, Mungu aliowachagua kuwa urithi wake.
      

     SHANGILIO
        Zab 147:12-15

                    Aleluya , aleluya Msifuni bwana, Ee Yerusalemu Huipeleka amri yake juu ya nchi Aleluya.


           SOMO LA INJILI
                    Lk. 12:1-7

             Wakati huo, makutano walipokutanika elfu elfu, hata wakakanyagana, alianza kuwaambia wanafunzi wake kwanza, Jilindeni na chachu ya Mafarisayo, ambayo ni unafiki. Lakini hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa, wala lililofichwa ambalo halitajulikana. Basi, yoyote mliyosema gizani yatasikiwa mwangani; na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatahubiriwa juu ya dari. Name nawaambia ninyi rafiki zangu, msiwaogope hao wauuao mwili, kisha baada ya hayo hawana wawezalo kutenda Zaidi. Lakini nitawaonya mtakayemwogopa, mwogopeni yule ambaye akiishakumwua mtu ana uweza wa kumtupa katika Jehanam; naam, nawaambia, Mwogopeni huyo. Je! Mashomoro watano hawauzwi kwa senti mbili? Wala hasahauliwi hata mmojawapo mbele za Mungu. Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi, bora ninyi kuliko mashomoro wengi.


Copyright © shajara  and  published  by  MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG                    

NYIMBO ZA DOMINIKA YA 29 YA MWAKA- C WA KANISA.

Nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka C Karibu kwa ajili ya nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka "C" Mwanzo: Ee Bwana Nimekuita  ...