Jumamosi ya 24 ya Mwaka
SOMO LA 1
1Kor. 15:35 – 37, 42 – 49
Labda mtu atasema, Wafufuliwaje wafu? Nao huja kwa mwili gani? Ewe mpumbavu! Uipandayo haihuiki, isipokufa; nayo uipandayo, huupandi mwili ule utakaokuwa, ila chembe tupu, ikiwa ni ya ngano au nyingineyo. Kadhalika na kiyama ya wafu. Hupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibika; hupandwa katika aibu; hufufuliwa katika fahari; hupandwa katika udhaifu; hufuliwa katika nguvu; hupandwa mwili wa asili; hufufuliwa mwili war oho. Ikiwa uko mwili wa asili, na war oho pia uko. Ndivyo ilivyoandikwa, mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni roho yenye kuhuisha. Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye huja ule wa roho. Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili atoka mbinguni. Kama alivyo yeye wa udongo, ndivyo walivyo walio wa udongo; na kama alivyo yeye wa mbinguni, ndivyo walivyo walio wa mbinguni. Na kama tulivyoichukua sura yake yule wa udongo, kadhalika tutaichukua sura yake yeye aliye wa mbinguni.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 56:9 – 13
(1). Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo. Neno hili najua kuwa Mungu yu upande wangu.
(K) Nienende mbele za Mungu katika nuru ya walio hai.
(2). Kwa msaada wa Mungu nitalisifu neno lake. Kwa msaada wa Bwana nitalisifu neno lake. Nimemtumaini Mungu, sitaogopa Mwanadamu atanitenda nini?

(3). Ee Mungu, nadhiri zako zi juu yangu; Nitakutolea dhabihu za kushukuru. Maana umeniponya nafsi yangu na mauti; Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke? Ili nienende mbele za Mungu Katika nuru ya walio hai.
V. (K) Nienende mbele za Mungu katika nuru ya walio hai.

SHANGILIO
2Tim. 1:10
Aleluya, aleluya, Mwokozi wetu Yesu Kristo alibatili mauti, na kuufunua uzima na kutokuharibika kwa Injili. Aleluya.

SOMO LA INJILI
Lk. 8:4 – 15
Mkutano mkuu ulipokutanika, na wale waliotoka kila mji wakimjia, Yesu alisema kwa mfano: Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu zake; naye alipokuwa akizipanda, nyingine zilianguka karibu na njia, zikakanyagwa, ndege wa angani wakazila. Nyingine zikaanguka penye mwamba; zilipoanza kumea zikakauka kwa kukosa rutuba. Nyingine zikaanguka kati ya miiba, na miiba ikamea pamoja nazo ikazisonga. Nyingine zikaanguka penye udongo mzuri; zikamea, zikazaa moja kwa mia. Alipokuwa akinena hayo alipaza sauti akisema, Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie. Wanafunzi wake wakamwuliza, Maana yake nini mfano huo? Akasema, Ninyi mmepewa kuzijua siri za ufalme wa Mungu; bali wengine kwa mifano, ili wakiona wasione, na wakisikia wasielewe. Na huo mfano, maana yake ni hii; Mbegu ni neno la Mungu. Wale wa karibu na njia ndio wasikiaopo hulipokea lile neno kwa furaha; nao hawana mizizi, huamini kitambo kidogo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga. Na zilipoanguka penye miiba ni wale waliosikia, na katika kuenenda kwao husongwa na shughuli na mali, na anasa za maisha haya, wasiivishe lolote. Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia.

No comments:
Post a Comment
"Asante sana kwa maoni yako"