TAFAKARI
Jumanne, Septemba 6, 2016.
Juma la 23 la Mwaka
1 Kor 6: 1-11 Zab 149: 1-6, 9 Lk 6: 12-19
KUDUMISHA UHUSIANO!
Katika Injili ya leo, tunaona Yesu akidumisha ushusiano wake na Baba yake-katika kusala. Wengi wanaweza kujiuliza sasa Yesu anasali kwa ajili ya nini? Swali hili linaweza kutupa maana mbali mbali nini maana ya sala. Sio swala tu la kuomba au kuomba vitu. Pia sio swali tu la kutimiza amri ya dini yetu kwamba “kusali sala zetu”. Sala ni kufanya mawasiliano na Mungu- mwanzo na mwisho wa kila kitu. Ina leta maana kwamba Yesu alipenda kuwa na mahusiano yake ya ndani na Baba yake na kuwa na muda wa kuwa naye. Kitu muhimu katika maneno ya Yesu ni kwamba afanye mapenzi ya Baba yake. Sala ndicho kilikuwa kiungo muhimu kuhakikisha kwamba kuna muunganiko thabiti na mapenzi ya Baba yake. Luka anamuonesha Yesu akisali kila mara kabla hajakutana na umati wa watu wakati wa utume wa maisha yake. Leo baada ya kipindi cha sala kuisha, anawaita wafuasi wake na kati yao anawachagua mitume kumi na wawili. Leo tusikie mwito wa Yesu. Kwanza, kuwa mfuasi wake, tulio jikabithi katika kupokea ujumbe wake ili utubadilishe; pili, tukubali jukumu la kuhubiri Injili yake kwa ujasiri kwa jinsi tunavyoishi, kwa jinsi tunavyo ongea, na kwanjia ya mahusiano tunayo anzisha; tatu, tutoke njee tukutane na Yesu ili tuweze kuhisi uponyaji wake kila tunapo uhitaji. Sala: Niongoze mimi, Bwana. Wewe ni moyo wangu, wewe ni nguvu yangu, wewe ni tumaini langu. Nifundishe mimi, Bwana, na ongoza njia zangu- ninakupenda zaidi kila siku inayopita. Amina.

No comments:
Post a Comment
"Asante sana kwa maoni yako"