Monday, 19 September 2016

MASOMO YA MISA, 19/9/2016 Jumatatu ya 25 ya Mwaka.


Jumatatu ya 25 ya Mwaka

SOMO LA 1
Mit. 3:27-34
          Mwanangu, Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; Nawe unacho kitu kile karibu nawe.Usiwaze mabaya juu ya jirani yako, Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama.Usishindane na mtu bila sababu, Ikiwa hakukudhuru kwa lo lote.Usimhusudu mtu mwenye jeuri, Wala usiichague mojawapo ya njia zake. Maana mtu mkaidi ni chukizo kwa Bwana, Bali siri yake ni pamoja na wanyofu.Laana ya Bwana i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki.Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema.

         WIMBO WA KATIKATI
Zab 15
         (1).   Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake, Asiyesingizia kwa ulimi wake.
           (K)Mtu aendaye kwa ukamilifu, atafanya maskani yake, katika kilima chako kitakatifu
        (2).    Wala hakumtenda mwenziwe mabaya, Wala hakumsengenya jirani yake. Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa, Bali huwaheshimu wamchao Bwana Ingawa ameapa kwa hasara yake, Hayabadili maneno yake.
             (K)Mtu aendaye kwa ukamilifu, atafanya maskani yake, katika kilima chako kitakatifu
        (3).  Hakutoa fedha yake apate kula riba, Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele.
             (K)Mtu aendaye kwa ukamilifu, atafanya maskani yake, katika kilima chako kitakatifu 

      SHANGILIO
Mt 5:16
           Aleluya, aleluya Nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. Aleluya

           SOMO LA INJILI

Lk 8:16-18
               Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Hakuna mtu ambaye akiisha
  washa taa huifunika kwa chombo, au kuiweka mvunguni, bali huiweka juu ya kiango, ili waingiao wapate kuona nuru yake.Kwa maana hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa; wala lililofichwa ambalo halitajulikana na kutokea wazi.Jiangalieni basi jinsi msikiavyo; kwa kuwa mwenye kitu atapewa, na yule asiye na kitu atanyang'anywa hata kile ambacho anadhaniwa kuwa nacho.

Copy right© by shajara and published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
      website:

No comments:

Post a Comment

"Asante sana kwa maoni yako"

NYIMBO ZA DOMINIKA YA 29 YA MWAKA- C WA KANISA.

Nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka C Karibu kwa ajili ya nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka "C" Mwanzo: Ee Bwana Nimekuita  ...