SOMO LA 1
1Kor. 11:17 – 26, 33
Katika kuagiza haya, siwasifu, ya kwamba mnakusanyika, si kwa faida bali kwa hasara. Kwa maana kwanza mkutanikapo kanisani nasikia kuna faraka kwenu; nami nusu sasadiki; kwa maana lazima kuwapo na uzushi kwenu, ili waliokubaliwa wawe dhahiri kwenu. Basi mkutanikapo pamoja haiwezekani kula chakula cha Bwana; kwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hata huyu ana njaa, na huyu amelewa. Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo. Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywa kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo. Kwa hiyo, ndugu zangu, mkutanikapo mpate kula, mngojane.

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 40:6 – 8, 16
(1) Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo, Masikio yangu umeyazibua, Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka. Ndipo niliposema, Tazama nimekuja.
(K) Mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.

(2). Katika gombo la chuo nimeandikwa, Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
(K) Mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.
(K) Mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.
(3). Nimehubiri habari za haki katika kusanyiko kubwa, Sikuizuia midomo yangu; Ee Bwana, unajua.
(K) Mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.
(K) Mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.
(4) Washangilie, wakafurahie, Wote wakutafutao. Waupendao wokovu wako Waseme daima. Atukuzwe Bwana.
(K) Mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.
(K) Mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.
SHANGILIO
Yn. 14:5
Aleluya, aleluya, Bwana anasema: mimi ndimi njia, na ukweli na uzima; mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya Mimi. Aleluya.

SOMO LA INJILI
Lk. 7:1 – 10
Yesu alipokwisha kuyamaliza maneno yake yote masikioni kwa watu, aliingia Kapernaumu. Na mtumwa wake akida mmoja alikuwa hawezi, karibu na kufa; naye ni mtu aliyempenda sana. Aliposikia habari za Yesu, alituma wazee wa Wayahudi kwake kumwomba aje amponye mtumwa wake. Nao walipofika kwa Yesu, walimsihi sana wakisema, Amestahili huyu umtendee neno hili; maana, analipenda taifa letu, naye alitujengea sinagogi. Basi Yesu akaenda pamoja nao. Hata alipokuwa si mbali na nyumba yake, yule akida alituma rafiki kwake, akamwambia, Bwana, usijisumbue, maana mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; kwa hiyo nilijiona sistahili mwenyewe kuja kwako; lakini, sema neno tu, na mtumwa wangu atapona. Kwa maana mimi nami ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, kufanya. Yesu aliposikia hayo alimstaajabia, akaugeukia mkutano uliokuwa ukimfuata, akasema, Nawaambia, hata katika Israeli sijaona Imani kubwa namna hii. Na wale waliotumwa waliporudi nyumbani, wakamkuta yule mtumwa ni mzima.

©Copy right by shajara
and publish by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG.
Contant us: ernest.magunus1500@gmail.com
Web site:
ernestliapanga.blogspot.com

No comments:
Post a Comment
"Asante sana kwa maoni yako"