Sunday, 13 October 2019
TAFAKARI YA MASOMO YA MISA, DOMINIKA YA 28 YA MWAKA "C" WA KANISA
MASOMO YA MISA, DOMINIKA YA 28 YA MWAKA "C" WA KANISA
2 Fal 5:14-17
Naamani alishuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi. Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako. Lakini akasema, Kama Bwana aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa. Naamani akasema; Kama sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa baghala wawili; kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa Bwana.
Zab 98:1-4
(1). Mwimbieni Bwana wimbo mpya, Kwa maana ametenda mambo ya ajabu. Mkono wa kuume wake wenyewe, Mkono wake mtakatifu umetenda wokovu
(K) Bwana ameufunua Soloviev wake machoni pa mataifa
(2). Bwana ameufunua wokovu wake, Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake
(K) Bwana ameufunua wokovu wake machoni pa mataifa
(3). Miisho yote ya dunia imeuona wokovu wa Mungu wetu, Mshangilieni Bwana, nchi yote. Inueni sauti, imbeni kwa furaha
(K) Bwana ameufunua wokovu wake machoni pa mataifa
2 Tim 2:8-13
Mkumbuke Yesu Kristo, aliyefufuka katika wafu, wa uzao wa Daudi kama inenavyo injili yangu. Nami katika hiyo nimeteswa hata kufungwa kama mtenda mabaya; lakini neno la Mungu halifungwi.
Kwa ajili ya hilo nastahimili mambo yote, kwa ajili ya wateule, ili wao nao waupate wokovu ule ulio katika Kristo Yesu, pamoja na utukufu wa milele. Ni neno la kuaminiwa.
Kwa maana, Kama tukifa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia; Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi; Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa.
Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.
Yn 10:27
Aleluya, aleluya Kondoo wangu waisikia sauti yangu, asema Bwana: Nami nawajua nao wanifuata. Aleluya
Lk 17:11-19
Yesu alipokwenda njiani kwenda Yerusalemu, alikuwa akipita katikati ya Samaria na Galilaya.
Na alipoingia katika kijiji kimoja, alikutana na watu kumi wenye ukoma; wakasimama mbali, wakapaza sauti wakisema, Ee Yesu, Bwana mkubwa, uturehemu! Alipowaona aliwaambia, Enendeni, mkajionyeshe kwa makuhani.
Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.
Na mmoja wao alipoona kwamba amepona, alirudi, huku akimtukuza Mungu kwa sauti kuu; akaanguka kifudifudi miguuni pake, akamshukuru; naye alikuwa Msamaria. Yesu akajibu, akanena, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu? Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa.
Copyright © 2016 by shajara and published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
see: imani-katoliki.blogspot.com
Sunday, 22 September 2019
WIMBO WA KATIKATI DOMINIKA YA 26 MWAKA "C"
✝πΆπΆπ΅π΅πΆπ΅π΅✝
MTUNZI: CAROL STEPHEN
Maneno ya wimbo
- Bwana, huishika kweli kweli milele, huwafanyia hukumu walio onewa.
- Bwana, huwafumbua macho walio pofuka, huwainua walio walio inama.
- Bwana, huwategemeza yatima na mjane, Bali njia ya wasio haki huipotosha.
Monday, 15 July 2019
JUMATATU YA 15 YA MWAKA "C" WA KANISA.
Somo la Kwanza
Tuesday, 9 July 2019
MASOMO YA MISA
Monday, 8 July 2019
NENO LA MUNGU 8/07/2019, JUMATATU YA 14 YA MWAKA 'C' WA KANISA.
Somo la Kwanza
Mwa. 28:10-22
Yakobo alitoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulanl akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale. Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamisha juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama. malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake. Na tazama, Bwana amesimama juu yake, akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako. Na uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi, na mashariki, na kaskazini, na kusini; na katika wewe, na katika uzao wako, jamaa zote za dunia watabarikiwa. Na tazama, mimi nipo pamoja nawe, nitakulinda kila uendako, nami nitakuleta tena mpaka nchi hii, kwa maana sitakuacha, hata nitakapokufanyia hayo niliyokuambia. Yakobo akaamka katika usingizi wake, akasema, Kweli, Bwana yupo mahali hapa, wala mimi sikujua. Naye akaogopa akasema, Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka, hapa ni nyumba ya Mungu, napo ndipo lango la mbinguni. Yakobo akaondoka asubuhi na mapema, akalitwaa lile jiwe aliloliweka chini ya kichwa chake, akalisimamisha kama nguzo, na kumimina mafuta juu yake. Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu. Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu. Na jiwe hili nililosimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi.
Neno la Mungu;..... Tumshukuru Mungu.
Wimbo wa katikati
Zab 91:1-4, 14-15
Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu
Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
Nitasema, Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu nitakayemtumaini.
(K) Mungu wangu nitakayemtumaini.
Maana Yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji,
Na katika tauni iharibuyo.
Kwa manyoya yake atakufunika,
Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;
Uaminifu wake ni ngao na kigao.
(K) Mungu wangu nitakayemtumaini.
Kwa kuwa amekaza kunipenda
Nitamwokoa; na kumweka palipo juu,
Kwa kuwa amenijua jina langu.
Ataniita nami nilamwitikia;
NitaKuwa pamoja naye taabuni,
Nitamwokoa na kumtukuza.
(K) Mungu wangu nitakayemtumaini.
Shangilio
Lk.8:15
Aleluya, aleluya,
Wanabarikiwa wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao, hulisikia neno la Mungu na kulishika.
Aleluya.
Somo la Injili
Mt 9:18-26
Yesu alipokuwa akiwaambia hayo, tazama, akaja jumbe mmoja, akamsujudia, akisema, Binti yangu sasa hivi amekufa; lakini njoo, uweke mkono wako juu yake, naye ataishi. Akaondoka Yesu, akamfuata, pamoja na wanafunzi wake. Na tazama, mwanamke aliyekuwa na ugonjwa wa kutoka damu muda wa miaka kumi na miwili, alikuja kwa nyuma, akaugusa upindo wa vazi lake. Kwa maana alisema moyoni mwake, Nikigusa tu upindo wa vazi lake nitapona. Yesu akageuka, akamwona, akamwambia, Jipe moyo mkuu, binti yangu, imani yako imekuponya. Yule mwanamke akapona tangu saa ile. Yesu alipofika nyumbani kwa yule jumbe, aliona wapiga filimbi, na makutano wakifanya maombolezo, akawaambia, Ondokeni; kwa maana kijana hakufa, amelala tu. Wakamcheka sana. Lakini makutano walipoondoshwa, aliingia, akamshika mkono; yule kijana akasimama. Zikaenea habari hizi katika nchi ile yote.
Neno la Mungu;...... Sifa kwako Ee Kristo.
Copyright ©2019, Shajara and published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG,
See: imani-katoliki.blogspot.com
Saturday, 6 July 2019
NENO LA MUNGU 06/07/2019,. JUMAMOSI YA 13 MWAKA 'C' WA KANISA
Somo la Kwanza
Mwa 27:1-5, 15-29
Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Nave akamwitikia, Mimi hapa. Akasema, Tazama, sasa mimi nimekuwa mzee, wala sijui siku ya kufa kwangu. Basi, nakuomba, chukua mata yako, podo lako na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie mawindo; ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukaniletee, ili nile; na roho yangu ikubariki, kabla sijafa. Na Rebeka akasikia, Isaka aliposema na Esau mwanawe. Basi Esau akaenda nyikani awinde mawindo, ayalete. Kisha Rebeka akatwaa mavazi mazuri ya Esau mwanawe mkubwa, aliyokuwa nayo nyumbani, akamvika Yakobo mwanawe mdogo. Na ngozi za wana-mbuzi akamvika mikononi, na katika ulaini wa shingo yake. Naye akampa Yakobo mwanawe mikononi mwake hicho chakula kitamu na mkate alioufanya. Akaja kwa baba yake, akasema, Babangu. Akasema, Mimi hapa, U nani wewe, mwanangu? Yakobo akamwambia babaye, Mimi ni Esau, mzaliwa wako wa kwanza, nimefanya kama ulivyoniambia. Ondo- ka, tafadhali, ukae kitako, ule mawindo yangu, ili roho yako inibariki. Isaka akamwuliza mwanawe, Imekuwaje umepata upesi namna hii, mwanangu? Akasema, Kwa sababu Bwana, Mungu wako, amenifanikisha. Isaka akamwambia Yakobo, Karibu, tafadhali, ili nikupapase, mwanangu, nione kwamba wewe ndiwe mwanangu Esau, ama siyo. Basi Yakobo akamkaribia Isaka, babaye, naye akampapasa, akasema, Sauti ni sauti ya Yakobo, lakini mikono ni mikono ya Esau. Wala hakumtambua, kwa maana mikono yake ilikuwa kama mikono ya Esau, ndugu yake, yenye malaika; basi akambariki. Akamwuliza, Wewe ndiwe kweli mwanangu Esau? Akasema, Ndimi. Akasema, Niletee karibu nami nipate kula mawindo ya mwanangu, ili roho yangu ikubariki. Akamsogeza karibu, naye akala; kisha akamletea mvinyo, akanywa. Isaka, baba yak, akamwambia, Njoo karibu sasa, ukanibusu, mwanangu. Akamkaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema, Tazama, harufu ya mwanangu Ni kama harufu ya shamba alilolibariki Bwana. Mungu na akupe ya umande wa mbingu, Na ya manono ya nchi, Na wingi wa nafaka na mvinyo, Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, na wana wa mama yako na wakusujudie, atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe.
Wimbo wa katikati
Zab 135:1-6
Aleluya.
Lisifuni jina la Bwana,
Enyi watumishi wa Bwana, sifuni.
Ninyi msimamao nyumbani mwa Bwana,
Nyuani mwa nyumba ya Mungu wetu.
(K) Msifuni Bwana kwa kuwa ni mwema.
Msifuni Bwana kwa kuwa Bwana ni mwema.
Liimbieni jina lake kwa maana lapendeza.
Kwa sababu Bwana amejichagulia Yakobo,
Na Israeli, wawe watu wake hasa.
(K) Msifuni Bwana kwa kuwa ni mwema.
Maana najua ya kuwa Bwana ni mkuu.
Na Bwana wetu yu juu ya miungu yote.
Bwana amefanya kila lililompendeza,
Katika mbingu na katika nchi,
Katika bahari na katika vilindi vyote.
(K) Msifuni Bwana kwa kuwa ni mwema.
Shangilio
Mt 4:4
Aleluya, aleluya,
Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Aleluya.
Somo la Injili
Mt 9:14-17
Wanafunzi wake Yohane walimwendea Yesu wakusema, Kwa nini sisi na Mafarisayo twafunga, bali wanafunzi wako hawafungi? Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kuomboleza, muda Bwana arusi akiwapo pamoja nao? Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana arusi; ndipo watakapofunga. Hakuna mtu atiaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu; maana kile kilichotiwa huonndoa kipande cha lile vazi, na pale palipotatuka huzidi. Wala watu hawatii divai mpya katika viriba vikuukuu; na kama wakitia, vile viriba hupasuka, divai ikamwagika, na viriba vikaharibika; bali hutia divai mpya katika viriba vipya, vikahifadhika vyote.
MIITO SHARTI IHUBIRIWE
Na Padri Innocent Bahati Mushi OFMCap.
Ni wazi kwamba familia, jumuiya na jamii nzima, inahusika sana kuipokea zawadi ya miito kwa kujijengea mazingira bora yanayovutia kwa wale walioitwa, kuitikia wito mtakatifu.
Mwitiko wa wito wa ndoa, upadre na maisha ya wakfu huzaa matunda pale ambapo mazingira yameandaliwa, kwenye udongo uliorutubishwa na Neno la Mungu, madhimisho ya kiliturujia, imani kwa Yesu Kristo, maadili mema na uadilifu, uchaji Mungu, moyo wa sadaka na majitoleo ya kila siku.
Kumbukeni kwamba maji hufuata mkondo au mfereji, tena udongo uliokulia huathiri sana namna yetu ya kuitikia wito au kuukata wito mtakatifu.
Kuandaa mazingira mazuri na malezi bora ni hatua za mwanzo katika kuitikia wito wowote. Maandalizi maridhawa ni pamoja na sala, mahubiri yanayobainisha umaana wa wito mtakatifu, faida na changamoto zake.
Mahali pengi ambapo miito ya ndoa, upadre na maisha ya wakfu imepungua, kuna uwezekano mkubwa kwamba kuna ukimya mkubwa kuhusu sala juu ya miito, na mafundisho juu ya miito yaliyoshehenishwa ushuhuda na uzuri wa maisha ya Jumuiya kwa wale waliokwishaingi katika maisha hayo.
Huenda sauti ya unabii imeshafifia mno na wanaoyaishi maisha yale hawatoi mwaliko wa furaha na matumaini kwa wale ambao wanawahudumia, katika hilo, jitihada inahitajika sana kufufua tena roho ya maisha ya kikristo.
Wanaohusika huenda wamekaa kimya au hawajali hali iliyopo kana kwamba kuna mambo mengine ya muhimu zaidi.
Miito iwe ni ya ndoa, utawa au upadre ni lazima ihubiriwe, isakwe na kuhamasishwa usiku na mchana, wakati ufaao na wakati usiofaa.
Hii ni changamoto kwa wale ambao wamepewa dhamana ya kuisakanya na kulea miito. Ni jukumu la wale wanaolea vyama vya kitume ambamo humo ni chimbuko la miito mingi.
Hatuwezi kusubiri kusema kwamba watakuja. Mtume Paulo anasema watakujaje wasipohubiriwa na kuhamasishwa?
Fr. Innocent Bahati Mushi OFMCap,
Mwenge Catholic University (MWECAU-MOSHI)
+255 755552538// +255783942208
Tuesday, 9 April 2019
UJUMBE WA KWARESMA 2019. Ter, 09/04/2019
1.Utangulizi&Sura ya I
Katika ujumbe wa mwaka huu Mababa Maaskofu wametoa mwaka huu kuwa ni mwaka wa familia. Ujumbe ukijikita katika 'FAMILIA NI KANISA LA NYUMBANI NA NI SHULE YA MAADILI'. Wanasisitiza juu ya kujifunza sala, kuhimiza kupokea Sakramenti, na kujifunza liturujia ni kazi ya wanafamilia kufunzana, hasa wazazi wawafunze watoto. Lkn sio tu wazazi hata watoto kuwakumbusha wazazi kusali pamoja na hata kuwafunza sala kama wamesahau. Watoto wanatakiwa kuwaombea na wapige kelele juu ya wazazi wasiosali wala kujishughulisha na mambo ya kanisa.
Maaskofu wanasisitiza juu ya utakatifu wa ndoa na maisha ya familia. Wazazi waheshimu ndoa zao na kurekebisha pale palipopotoka. Ili kulinda utakatifu wa ndoa wazazi waache kuendekeza michepuko, mitara, uzinzi ni vitu ambavyo vinaharibu utakatifu wa ndoa.
Watoto wajisikie amani wakiwa nyumbani kama vile wanavyojisikia amani wawapo kanisani kwani hapo nyumbani ni kanisani pia. Akinamama wapendeni waume zenu msiwafanye wakawa walevi kisa kukimbia manyanyaso ya familia na hata kuanzisha michepuko. Wanaume wajibikeni ktk familia zenu na sio kuwaachia majukumu ya familia akinamama.
Tunapoendelea kutafakari juu ya ujumbe huu wa Kwaresma wa mwaka huu juu ya familia, siku hizi familia zetu zimegeuka kuwa makambi ya mateso, jehanamu, na hata jela ndogo inayotokana na ukosefu wa upendo na ukatili uliopitiliza.
Katika Mwaka huu 2019 kunamatukio makuu manne kama ifuatavyo.
1.1 Ni miaka 25 toka Sinodi ya kwanza ya Afrika iliyojikita katika kutafakari juu ya familia. Wanasisitiza kuwa kujenga familia imara ni kujenga jamii imara na kanisa imara. Tunawajibika kufundisha wanandoa juu ya majukumu yao ya malezi katika ngazi ya familia. Mfano akina baba wamewatulia majukumu ya malezi ya watoto akinamama na akinamama nao wamewatulia majukumu yao mahouse girls.
1•2 Mwaka huu ni wa 25 toka UMOJA WA MATAIFA ulipotangaza kuwa mwaka 1994 kuwa ni mwaka wa familia. Ulisisitiza kuwa familia inaunda kitengo cha msingi cha jamii, hivyo inatakiwa kuhakikishiwa ulinzi. Ni jukumu la viongozi wa serikali kuzihakikishia ulinzi familia. Viongozi wa serikali hasa watendaji katika tarafa, miji, vijijini na mitaa wanajukumu la kuibua matukio ya unyanyasaji ktk ngazi ya familia ambayo hufanyika kwa siri. Mfano kumeripotiwa watoto kufungiwa ndani kwa muda mrefu, watoto kunyimwa chakula, kubakwa, kulawitiwa, wazazi kuzaa na mabinti zao, akinamama kuwalaghai kimapenzi mahouse boys hali kadhalika akinababa na watoto wakiume kuwanyanyasa kingono mahousegirls, ukeketaji..n.k Vitendo hivi vipo ni kazi ya wanahabari za uchunguzi kuibua kadhia hizi ktk familia zetu ambapo ni vitu vinavyoondoa utakatifu wa familia na maana ya kanisa na shule ya maadili.
1.3 Mwaka huu pia ni jubilei ya miaka 50 tangu HALMASHAURI YA BARAZA LA WALEI kuanzishwa mwaka 1969. Ni ukweli usiopingika kwamba viongozi walei wa kanisa ktk maparokia mengi wamekuwa wakijitoa sana ktk kulihudumia kanisa. Viongozi hawa wapo tayari kutoa muda wao kuwahudumia mapadre, kuwatafutia usafiri, kuanzisha miradi ya parokia na kusimamia kanisa. Wapo wachache ambao kutokana na ufurufuru wa imaani wamekuwa miiba kwa maparoko na kanisa, wamekuwa wapinga maendeleo ya kanisa, wezi na wavurugaji wa imani, mwaka huu ukiwa wa uchaguzi, viongozi kama hawa wawekwe pembeni wajifunze dini kwanza. Ni wajibu wa Maparoko kuwafanyia kitu fulani cha pekee ktk mwaka wao huu wa jubilei ikiwa ni kuwapongeza, kuwafanyia sherehe, na mengine mengi kama kutambua kazi yao muhimu.
1.4 Mwaka huu ni jubilei ya dhahabu ya miaka 50 tangu TYCS\YCS ianzishwe. Hawa ni vijana ambao bado wanakuwa chini ya wazazi au walezi. Inatakiwa kuwaandaa vizuri ili waje kuwa waumini wazuri baadae. Tukiwafundisha vzr vijana hawa tutaondoa tatizo la kuingia ktk ndoa bila sakramenti, ubaridi wa kuchangamkia mambo ya kanisa, kusali, ambapo kwa sasa vijana wengi ni kama mtindo wao wa maisha. Mapadre hatuna budi kufanya makongamano ya kutosha kwa ajili yao kama vile Kongamano la Pasaka. Tuwalee vzr kwa kuwafundisha dini kwa usahihi. Kuwaongoza kumwelekea Yesu.
******Itaendelea*****
By; Fr. Kawonga
Holy Family Parish-Mkongo
Saturday, 7 July 2018
TAFAKARI YA MASOMO YA MISA, DOMINIKA YA 14 YA MWAKA, "B"
“MBEGU ZA UZIMA”
Julai 8, 2018
Dominika ya 14 ya Mwaka
Eze 2:2-5
Zab 123 (K. 2);
2 Kor 12:7-10;
Mk 6:1-6.
KUTESEKA KWA NABII
Watu wengi ambao ni wakuu katika sehemu nyingi wamepeita mateso na changamoto mbali mbali na hivyo hata kuvishinda na kusimama imara.
Huenda, watu wao wenyewe waliwakataa na walikuwa na wakati mgumu sana kuikabili jamii. Wale wote waliotumwa na Mungu nao pia wanakutana na magumu.
Hata Mwana wa Mungu, ambaye watu walimsubiri kwa muda bado alipokuja walimpinga na hata watu wa nyumbani kwake hawakumuelewa.
Katika somo la kwanza, Ezekieli anakuwa kama chombo cha Mungu cha amani, akiwa kama balozi wa Mungu kati ya watu wake katika miaka hiyo kabla na baada ya Wayahudi hawajaanguka kwa Wababiloni. Manabii walipewa nguvu ya Roho wa Mungu kubainisha ukweli na haki na uaminifu katika hali ambayo sifa hizi zilifunikwa kwa uongo, ukosefu wa haki, na kutokuwa na imani kwa vizazi kadhaa. Unabii Wake ulikuwa katika hali husika ya kitaifa hususani ya kisiasa na ya kidini. Watu walikuwa wasumbufu kwasababu hawakutaka kumsikiliza Mungu.
(Ez 3:7). “Usiwaogope hao, wala usiyaogope maneno yao.” (Ez 2:6). Wanaweza wasiyaogope maneno yako, lakini walau “watajua yakuwa nabii amekuwapo miongoni mwao.” (Ez 2:5). Huu ni wito wa nabii.
Ni mtu ambaye Mungu ameudhihirisha ukweli wake ili kuuwasilisha kwa watu wake.
Katika somo la pili, Paulo anaelezea upinzani wake. Inawezekana pia Paulo aliyafikiria matatizo mengi ya kichungaji yaliyolikabili kanisa la Korintho kama ni mwiba katika nyama yake. Mwanzo aliuliza kuwa mwiba huu utolewe kwake, lakini mwishowe aliukubali, na hata kutukuzwa katika kejeli, mateso, na magumu ambayo aliteseka nayo kwa ajili ya Kristo (2Kor 12:10).
Katika Injili, tunaona kukataliwa kwa Yesu na ndugu zake wa mitaa yake.
Zaidi ya hili, Yesu alikutana na vikwazo kutoka katika mamlaka ya Wayahudi.
Marko anahesabu muendelezo wa matukio matano ya upinzani ambapo Yesu ilimpasa ajitetee yeye mwenyewe: nguvu yake ya kusamehe dhambi (2:1-12); upendo wake kwa watoza ushuru na wadhambi (2:13-17); mitazamo yake juu ya kufunga (2:18-22); uelewa wake juu ya usafi wa utamaduni (2:23-28); na nguvu zake za kuponya siku ya Sabato (3:1-6).
Katika Injili ya leo, ni kusanyiko la watu wa nyumbani ndio waliomsaliti Yesu. Alipitia kile walichokipitia Isaya, Yeremia na Ezekieli – yakuwa nabii hakubaliki nyumbani kwake. Ingawa watu wa Nazareti walifurahishwa sana na mafundisho ya kukubali asili yake ya miujiza na matendo yake, hawakuenda mbali na kushangawa kwao. Badala yake, waliishia kuoanza kutazama hali yake ya zamani na familia aliotoka.
Badala ya kuwa na Imani wanaanza kuangalia mambo ya nje ambayo sio muhimu kwa wokovu wao.
Wanashindwa kupokea ujumbe wa kiroho. Pengine nasi tunaweza kuwa kama watu wa Nazareti, tukawa tumejijengea kwamba unabii wa kweli hauwezi kutoka sehemu fulani au tukashindwa kupokea ukweli kwasababu tunadhani huyu hawezi kutuambia kitu. Pengine Padre fulani, ulimuona akikuwa au akiwa mseminari na sasa anakuhubiria unaanza kusema haka katoto kajuzi mbona nakifahamu vizuri hakina lolote? Tuangalie sana tusije tukamfukuza Yesu katika maisha yetu akashindwa kutenda miujiza akaenda kutenda miujiza sehemu nyingine. Katika hali ya leo pia, hali haijabadilika.
Tumeitwa kuwa manabii kwa watu wetu wenyewe, huenda ikahitaji kusimama kwa ajili ya matendo maovu ndani ya jamii, kuongea kwa ajili ya watu wasio na sauti au kuwatetea masikini na wananyanyaswaji.
Tunapaswa kujiandaa na hata kutukanwa. Huu ndio wito wetu. Wito wetu wakushiriki katika unabii ya Kristo.
Sala: Bwana, niimarishe mimi katika utume wangu kama nabii nihubiri ujumbe wako.
Copyright ©; 2018 by shajara and published by MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
see: imani-katoliki.blogspot. com
MASOMO YA MISA LEO
Friday, 6 July 2018
Thursday, 5 July 2018
MASOMO YA MISA
HISTORIA YA MT. MARGARETA MARIA ALAKOK, MTAWA.
Historia ya Mt. Margareta Maria Alakok, Mtawa
Kule Ufaransa katika karne ya 17, upendo kwa Mungu ulikuwa umepooza sana.
Watu wengi waliuacha mwenendo wa kikirstu na wengine waliukubali uzushi wa Jansenio aliyehubiri kwamba Mungu hawapendi watu wote sawa, bali anawapenda wengine, na baadhi yao anawaacha kabisa.
Ili kuwaamshia wakatoliki upendo kwa Mungu, watakatifu watatu hasa walioishi kati ya miaka 1625 na 1690, walliieneza, kwa bidii sana, ibada kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu, nao ni Mt. Yohani Eudes (1610-1680).Margareta Maria alizaliwa katika nchi ya Ufaransa mwaka 1647.
Baada ya kifo cha baba yake, wakamwingiza katika shule ya shirika la Mt. Klara. Alipokuwa na umri wa miaka kumi na mmoja alishikwa na ugonjwa na kwa sababu hiyo hakuweza kutembea kwa muda wa miaka minne. Kisha kupona, alianza kuzipendelea anasa za ulimwengu, kwa kuvaa kimalidadi. Bwana wetu alimtokea akamwambia. "Ukiniacha mimi na kutaka mchumba mwingine, mimi nitakuacha kwa siku zote".
Margareta alisikiliza mashauri ya Yesu na alipokuwa na umri wa miaka ishirini na miwili, akaingia katika shirika la masista wa Maonano (Visitation Sisters) huku Paray-le-Monial (Ufaransa).Mwaka 1673, alipokuwa akisali mbele ya Saktramenti Kuu Bwana Yesu alimtokea akamwonyesha moyo wake akisema:
“Tazama moyo wangu unaowaka mapendo kwa watu.Ningetaka kuwafumbulia watu moyo wangu, na kuwagawia neema zote zilizomo".
Siku nyingine, Mwokozi alimtokea akamwonyesha vidonda vitano mwilini mwake akisema:
"nimewapenda watu kwa mapendo makubwa. Lakini watu hawana shukrani. Laiti watu wengi wangeyafikia mapendo yangu, ningekuwa tayari kufanya zaidi, na kufanya bado zaidi kwa ajili yao. Lakini watu wanaonionyesha ubaridi na ugumu wao. Ewe mwanangu, unifurahishe kidogo pahali pa wakosefu hao".
Mwezi Juni mwaka 1675, Bwana wetu alimwonyesha tena moyo wake akisema: “Ndio moyo huu unaopenda sana watu, na watu hawaupendi. Kwa Masomo ya Misa za kila siku.
Kwa Masomo ya misa na Sala mbalimbali na historia za maisha ya Watakatifu tembelea: MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG.
Monday, 2 July 2018
MASOMO YA MISA JUMATATU YA 13 YA MWAKA. 'B' WAKANISA.
Amo. 2:6 – 10, 13 – 16
Haya ndiyo asemayo Bwana; Kwa makosa matatu ya Israeli, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewauza wenye haki kwa fedha, na maskini kwa jozi ya viatu; nao hutwetea kuipotosha njia ya mwenye upole; na mtu na baba yake humwendea mwanamke mmoja, hata kulitia unajisi jina langu takatifu; nao hulijaza karibu na kila madhabahu juu ya nguo zilizowekwa rehani, na katika nyumba ya Mungu wao hunywa divai ya watu waliotozwa fedha. Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini.
Pia naliwapandisha ninyi kutoka nchi ya Misri, nikawaongoza muda wa miaka arobaini jangwani, ili mpate kuimiliki nchi ya Mwamori. Tazameni, nitawalemea ninyi, kama gari lilemeavyo lililojaa miganda. Naye apigaye mbio atapotewa na kimbilio; Wala aliye hodari hataongeza nguvu zake; Wala shujaa hatajiokoa nafsi yake; Wala apindaye upinde hatasimama; Wala aliye mwepesi wa miguu hataokoka; Wala apandaye farasi hatajiokoa nafsi yake; Naye mwenye moyo mkuu miongoni mwa mashujaa atakimbia uchi siku ile, asema Bwana.
Zab. 50:16 – 23
(1). Mtu asiye haki, Mungu amwambia, Una nini wewe kuitangaza sheria yangu, Na kuliweka agano langu kinywani mwako? Maana wewe umechukia maonyo, Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.
(2). Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye, Ukashirikiana na wazinzi. Umekiachia kinywa chako kinene mabaya, Na ulimi wako watunga hila.
(3). Umekaa na kumsengenya ndugu yako, Na mwana wa mama yako umemsingizia. Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza; Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe. Walakini nitakukemea; Nitayapanga hayo mbele ya macho yako.
(K) Yafahamuni hayo, ninyi mnaomsahau Mungu.
Shangilio
Yn. 14:5
Aleluya, aleluya. Bwana anasema: mimi ndimi njia, na ukweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. Aleluya.
Somo la Injili
Mt. 8:18 – 22
Yesu alipoona makutano mengi wakimzunguka, aliamuru kuvuka kwenda ng’ambo. Mwandishi mmoja akamwendea, akamwambia, Mwalimu, nitakufuata kokote uendako. Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana vioto; lakini Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake. Mwingine katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, nipe ruhusa kwanza, niende nikamzike baba yangu. Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao.
Saturday, 23 June 2018
Friday, 12 May 2017
BWANA, NATAMANI DAIMA KUWA NAWE.
NYIMBO ZA DOMINIKA YA 29 YA MWAKA- C WA KANISA.
Nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka C Karibu kwa ajili ya nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka "C" Mwanzo: Ee Bwana Nimekuita ...
-
Katika kuhakikisha kwamba uinjili shaji unakua tumekuletea nata zanyimbo za kikatoliki hizihapa Bofya hapa ...
-
JUMAPILI YA 28 YA MWAKA-C Somo I: 2Fal 5:14-17 Zab/Kit: 98:1-2, 3ab, 3cd-4 Somo II: 2Tim 2:8-13 Injili: Lk 17:11-19 Nukuu ...
-
Nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka C Karibu kwa ajili ya nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka "C" Mwanzo: Ee Bwana Nimekuita ...
-
Dominika ya 28 ya Mwaka SOMO LA 1 2 Fal 5:14-17 Naamani alishuka, akajichovya mara saba katika Y...
-
Dominika ya 30 ya Mwaka SOMO LA 1 Ybs 35:12-14,16-19 Kwa kuwa Bwana ndiye mhukumu wala hakijali cheo cha mtu. Hatamkubali ye yote juu...










