Wednesday, 31 August 2016

TAFAKARI NZURI YA MASOMO YA MISA,31/8/2016 "nguvu ya mamlaka".


TAFAKARI
Jumatano, Agosti 31, 2016,
Juma la 22 la Mwaka wa Kanisa
1 Kor 3: 1-9 Zab 32: 12-15, 20-21 Lk 4: 38-44
      NGUVU YA MAMLAKA!
     Katika Injili ya leo, tunaona Yesu akimponya mkwewe Simoni. Mara nyingi Yesu aliponya kwa kugusa bali pia alikuwa na neno la mamlaka la kuponya kwa kuamuru. Msisitizo unaoneshwa kwenye Injili, ugonjwa ndio unao amuriwa, kama Yesu alivyo amuru mawimbi ya bahari ya Galilaya kwa mamlaka, “hali ikawa shwari” na Amani ikawapo (Mk 4: 39), na mawimbi yakatulia. Je, hili linawezekana kwa mfuasi wa Yesu katika nyakati hizi!. Ukweli ni kwamba amri ya kuamuru inatoka katika mamlaka sio katika nguvu. Kwahiyo tunapaswa kuwa wafuasi tuliojazwa na mamlaka sio nguvu. Hili linawezekana tu, namaanisha tu kwa kukutana na Yesu nakumvaa yeye sio kwakuwa na elimu ya Yesu tu. Ni katika kufikia kiwango cha kusema kama Paulo kuishi kwangu sio mimi bali Kristo anaishi ndani yangu. Twaweza kufanya yote kama tutaunganika na Yesu kweli kweli, si katika kuwa na elimu kuhusu maandiko na kushindwa kuyaruhusu yakufanye uunganike na Yesu. Kwa njia nyingine tumvae Kristo. Kama tunavyosikia katika somo la kwanza, tumruhusu Mungu akuze maisha yetu, tumuache Kristo afanye mabadiliko ndani yetu. Sisi ni shamba la Mungu tumruhusu Mungu akuze zawadi mbali mbali mioyoni mwetu ili tuweze kuzaa matunda yenye kumpendeza. Tushirikiane na Mungu ili zawadi anazo kuza ndani yetu ziweze kumrudishia sifa na utukufu. Sala: Bwana, tufanye washiriki wa mamlaka yako. Amina

MASOMO YA MISA,31/8/2016 Jumatano ya 22 ya Mwaka.


Jumatano ya 22 ya Mwaka
SOMO LA 1
1 Kor. 3:1 – 9
    Ndugu zangu, mimi siwezi kusema nanyi kama na watu wenye tabia ya rohoni, bali kama na watu wenye tabia ya mwilini, kama na watoto wachanga katika Kristo. Naliwanywesha maziwa, sikuwalisha chakula; kwa kuwa mlikuwa hamjakiweza. Naam, hata sasa hamkiwezi, kwa maana hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu? Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. Basi yeye apandaye, nay eye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe. Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jingo la Mungu.
WIMBO WA KATIKATI Zab. 33:12 – 15, 20 – 21
    Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, Watu aliowachagua kuwa urithi wake. Toka mbinguni Bwana huchungulia, Huwatazama wanadamu wote pia. (K)
Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake. Toka mahali pake aketipo Huwaangalia wote wakaao duniani. Yeye aiumbaye mioyo yao wote Huzifikiri kazi zao zote. (K)
Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake. Nafsi zetu zinamngoja Bwana; Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu. Maana mioyo yenu itamfurahia, Kwa kuwa tumelitumainia jina lake takatifu. (K)
Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, watu aliowachagua kuwa urithi wake.
SHANGILIO Yak. 1:21
    Aleluya, aleluya, Pokeeni kwa upole neno la Mungu lililopandwa ndani, liwezalo kuziokoa roho zenu. Aleluya.
SOMO LA INJILI
Lk. 4:38 – 44
      Yesu alitoka katika sinagogi, akaingia katika nyumba ya Simoni. Naye mkwewe Simoni, mamaye mwomba kwa ajili yake. Akasimama karibu naye, akikemea ile hma, ikamwacha; mara hiyo akaondoka, akawatumikia. Na jua lilipokuwa likichwa, wote waliokuwa na wagonjwa wenye maradhi mbalimbali waliwaleta kwake, akaweka mikono yake juu ya kila mmoja akawaponya. Pepo nao waliwatoka watu wengi, wakipiga kelel na kusema, Wewe u Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walimjua kuwa ndiye Kristo. Hata kulipokucha alitoka akaenda mahali pasipokuwa na watu; makutano wakawa wakimtafutatafuta, wakafika kwake, wakataka kumzuia asiondoke kwao. Akawaambia, Imenipasa kuihubiri habari njema ya ufalme wa Mungu katika miji mingine pia; maana kwa sababu hiyo nalitumwa. Basi, alikuwa akihubiri katika masinagogi ya Galilaya.

Tuesday, 30 August 2016

TAFAKARI NZURI YA MASOMO YA MISA,30/8/2016 "VITA VYAKI ROHO"

TAFAKARI
Jumanne, Agosti 30, 2016.
Juma la 22 la Mwaka
1 Kor 2: 10-16 Zab 144: 8-14 Lk 4: 31-37

      VITA VYA KIROHO!
    Leo katika somo la kwanza, Mt. Paulo anaongelea kuhusu Roho wa Mungu na roho wa ulimwengu, vita vya kila wakati katika mioyo yetu, tukivutwa huku na huku. Injili inamuonesha Yesu akitoa pepo, akiamuru “pepo mchafu” atoke ndani ya mtu. Watu wa Kapernaumu huenda walijua mtu yule alikuwa na pepo mchafu, lakini hawakujua nini, au nani, huyo pepo. Hawakuweza kulitambua kwa jina au kufahamu. Lakini Yesu aliweza. Umoja wake na Baba unampa utambuzi ambao wengine hawana. Mt. Inyasi wa Loyola anatumia neno la “utambuzi wa roho” kwa mpangilio uliojikita kwenye Imani kwa nia ya kutambua na kuelewa, nini kinaendelea ndani ya mioyo yetu na nini mapenzi ya Mungu kwa ajili yetu. Tuombe neema ya kutambua machafuko ndani ya mioyo yetu na kuisikiliza sauti ya Mungu. Sala: Baba Mungu, ninakuomba wewe “Roho ya utambuzi” ili niweze kukua daima na kusikiliza sauti ya Roho wako kwa haraka na kwa ufasaha kila wakati. Amina

MASOMO YA MISA,30/8/2016. Jumanne ya 22 ya Mwaka.

Jumanne ya 22 ya Mwaka
SOMO LA 1
1 Kor 2:10-16

       Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.

  WIMBO WA KATIKATI Zab 145:8-14           Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, Bwana ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote. (K)

Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote. Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru, Na wacha Mungu wako watakuhimidi. Wataunena utukufu wa ufalme wako, Na kuuhadithia uweza wako. (K)

Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote. Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari ya ufalme wake. Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote, (K)

Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote. Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote. Bwana huwategemeza wote waangukao, Huwainua wote walioinama chini. (K)

Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote.

SHANGILIO Lk 7:16
    Aleluya, aleluya Nabii mkuu ametokea kwetu; na, Mungu amewaangalia watu wake. Aleluya

SOMO LA INJILI Lk 4:31-37
      Yesu alishuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya, akawa akiwafundisha siku ya sabato; wakashangaa mno kwa mafundisho yake, kwa kuwa neno lake lilikuwa na uwezo. Na ndani ya sinagogi mlikuwa na mtu mwenye roho ya pepo mchafu, akalia kwa sauti kuu, akisema, Acha! Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Nakujua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, mtoke. Ndipo yule pepo akamwangusha katikati, akamtoka asimdhuru neno. Mshangao ukawashika wote, wakasemezana wakisema, Ni neno gani hili, maana awaamuru pepo wachafu kwa uwezo na nguvu, nao hutoka. Habari zake zikaenea kila mahali katika nchi ile.

Monday, 29 August 2016

TAFAKARI NZURI YA MASOMO YA MISA,29/8/2016 "Tusimame kwa ukweli".

TAFAKARI
Jumatatu, Agosti 29, 2016.
Juma la 22 la Mwaka
Kumbukumbu ya Kukatwa Kichwa kwa Mt. Yohane Mbatizaji
1Kor 2: 1-5; Zab 118: 97-102; Mk 6:17-29

TUSIMAME KWA UKWELI!
      Ushahidi wa Mt. Yohane Mbatizaji unatukumbusha kwamba wito wa muhimu katika Ukristo wetu kuliko yote ni kuishi Injili. Hatuna wasi wasi kwamba Yohane aliteseka gerezani na kifungo kama shahidi wa mkombozi, yeye alikuwa ndio mtangulizi. Mtesi wake, mfalme Herode na Herodia hawakumuhukumu ili amkane Kristo, bali walitaka akae kimya kuhusu ukweli, afiche ukweli. Lakini hakuweza kukaa kimya. Na matokeo yake ilimbidi kukatatwa kichwa chake na watesi wake. Alikufa kwa sababu ya ukweli, alikufa kwa ajili ya Kristo. Je, Yesu hakusema “mimi ni ukweli!” kwa hiyo kwa sababu Yohane alimwaga damu yake kwa sababu ya ukweli ni wazi na hakika kwamba alikufa kwa ajili ya Kristo. Je, tumekuwa waoga kufanya jambo sahihi au kutoa ushuhuda wa Imani yetu au kusimama kwa ajili ya ukweli kwa sababu tulikuwa tunaogopa wengine wanatufikiriaje au watatuambia nini? Nina Imani kwamba wengi wetu tulishakuwa hivyo, ni kitu ambacho tunapigana nacho kila wakati. Vijana wanateseka kupita katika makundi mbali mbali na hujikuta wanakuwa na tabia mbali mbali zisizo nzuri, wakati mwingine hujikuta wanahatarisha maisha yao. Wafanyakazi wanagoma kwa kutoa sababu za kupinga rushwa au tamaduni mbali mbali zisizo jali utu wa watu. Sisi Wakristo tunakuwa Wakristo wa jina tu sio wa matendo yetu. Ni kitendo cha vita kati ya dhamiri zetu na vionjo vyetu. Tuna mfano wa mfalme Herode, aliyejua kwamba kitu cha kweli cha kufuata ni kumsikiliza Yohane Mbatizaji na kumwachia huru, lakini alikuwa anaogopa wageni wake watamfikiriaje. Kinyume na nia yake nzuri, anamtoa Yohane auwawe. Yohane alitoa thamani ngumu, kwa sababu alifanya uchaguzi sahihi wa kuwa mwaminifu kwa Bwana na akasimama kadiri ya ukweli wa dhamiri yake. Ushuhuda wa Yohane ni mfano kwetu wakusimama imara kila mara kwa kuchagua lililo sahihi kila mara na kulifanya. Ni wazi mbele ya macho ya watu tunaweza kuonekana wajinga, lakini mbele ya Mungu tutaonekana kama watakatifu. Sala: Bwana, tufanye waenezaji wa ukweli kwa maneno na matendo yetu. Amina

MASOMO YA MISA,kufa shahidi Mt. Yohane

Kufa Shahidi Mt. Yohane
SOMO LA 1 1 Kor 2:1-5

       Ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima. Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa. Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko mengi. Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.

WIMBO WA KATIKATI Zab 119:97-102
  Sheria yako naipenda mno ajabu, Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa. (K)

Sheria yako, Ee Bwana, naipenda mno ajabu. Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu, Kwa maana ninayo sikuzote. (K)

Sheria yako, Ee Bwana, naipenda mno ajabu. Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo. (K)

Sheria yako, Ee Bwana, naipenda mno ajabu. Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako. (K)

Sheria yako, Ee Bwana, naipenda mno ajabu. Nimeiepusha miguu yangu na kila njia mbaya, Ili nilitii neno lako. (K)

Sheria yako, Ee Bwana, naipenda mno ajabu. Sikujiepusha na hukumu zako, Maana Wewe mwenyewe umenifundisha. (K)

Sheria yako, Ee Bwana, naipenda mno ajabu.

SHANGILIO Mt 5:10
     Aleluya, aleluya Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao Aleluya

SOMO LA INJILI Lk 4:16-30
       Yesu alienda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho. Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu. Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu? Akawaambia, Hapana shaka mtaniambia mithali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako; mambo yote tuliyosikia kwamba yametendeka Kapernaumu, yatende na hapa pia katika nchi yako mwenyewe. Akasema, Amin, nawaambia ya kwamba, Hakuna nabii mwenye kukubaliwa katika nchi yake mwenyewe.Lakini, kwa hakika nawaambia, Palikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita, njaa kuu ikaingia nchi nzima; wala Eliya hakutumwa kwa mmojawapo, ila kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni. Tena, palikuwa na wenye ukoma wengi katika Israeli zamani za nabii Elisha, wala hapana aliyetakaswa ila Naamani, mtu wa Shamu. Wakajaa ghadhabu wote waliokuwa katika sinagogi walipoyasikia hayo. Wakaondoka wakamtoa nje ya mji, wakampeleka mpaka ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa juu yake, wapate kumtupa chini; lakini yeye alipita katikati yao, akaenda zake.

Sunday, 28 August 2016

TAFARI YA MASOMO YA MISA,Dominika ya 22 ya Mwaka C wa kanisa.

TAFAKARI
Jumapili, Agosti 28, 2016.
Dominika ya 22 ya Mwaka C wa Kanisa
Ybs 3:19-21, 30-31; Zab 67: 4-7, 10-11; Ebr 12: 18-19, 22-24; Lk 14: 1, 7-14.

UNYENYEKEVU: TUNU TUPATAYO KWA UFALME WA MILELE
        Katika Injili zote nne, Yesu anaoneshwa mtu anayependa kuwa na watu, na hata kuhudhuria matukio ya kijamii kama harusi, kualikwa kwenye chakula, nk. Alienda mpaka hata kwenye nyumba za watoza ushuru waliokuwa wanachukiwa na Wayahudi na pia katika nyumba za Mafarisayo ambao kila mara walimjaribu kwa mitego ya maswali na kumlaumu na ambao mwishoni walipanga hata kifo chake. Katika Injili ya leo tunamuona Yusu alikuwa amealikwa kwa chakula katika nyumba ya kiongozi wa Mafarisyo na Yesu kama kawaida yake anakubali mwaliko. Injili inasema kwamba Mafarisayo walikuwa wanamuangalia kwa makini na kwasababu ilikuwa ni Sabato inaonekana mlo huu ilikuwa ni kwasababu ya kumtega kuona kama atavunja sheria za Sabato. Lakini Yesu pia anawaangalia wao pia. Na hapo Yesu anawapa mfano. Sehemu ya kwanza ya mfano huu unakuja kwasababu Yesu aligundua kwamba kati ya wageni wengi walioalikwa walikuwa wakitafuta nafasi za mbele za heshima. Kwa Wayahudi sehemu ya heshima ni kwa wale waliokaa upande wa kulia au kushoto karibu na meza aliokaa mgeni rasmi aliyealikwa au mwenye sherehe. Kwahiyo Yesu anatoa mfano wake akitumia mfano wa karamu ya harusi ambao ilikuwa ni tukio la kawaida katika jamii hii. Mafarisayo wakiwa ni watu wanaoheshiwa sana na Wayahudi kawaida walitegemea kukaa sehemu za heshima. Kwahiyo Yesu anawaonya akiwambia wasitafute sehemu za heshima kwasababu katika Ufalme wa Mungu haitakuwa hivyo. Mafarisayo walijua na kuamini kwamba kawaida wao wangekuwa wa kwanza kutumikiwa lakini hapa Yesu anafunga matumaini yao. Yesu anatambulisha kitu kidogo sana na chenye thamani sana “unyenyekevu” kadiri unavyokuwa mnyenyekevu kadiri unavyoheshimiwa. Mafarisayo somo hili lilikuwa ngumu kwao. Sisi nasi wakati mwingine tumejikuta tukitafuta heshima. Kumbuka maneno ya Yesu “watakao jikweza watashushwa na watakao jishusha watakwezwa”. Tubadilike leo tuache hali yetu yakutafuta heshima ya muda tuu na tutafute heshima ya uzima wa milele ambayo inapatikana kwa unyenyekevu. Katika sehemu ya pili ya mfano Yesu naongea na aliyemualika kuhusu wale walioalikwa. Yesu hapa anasema kitu ambacho ni jambo la kufikirika kwa akili zetu kwamba, kama mtu akimualika rafiki, ndugu, waheshimiwa, anatagemea kupata kitu kwao tena. Kama mtu akitupatia zawadi katika sikukuu ya kuzaliwa anategemea yeye naye akiwa na siku yake ya kuzaliwa nawe utampelekea chochote. Katika hali nyingine, Yesu anatualika tuwaalike masikini, vilema, wasiojiweza nk, ili tusitegemee kitu kutoka kwao kama malipo. Yesu anatu hakikishia kwamba kitendo hicho hakitaenda bure bila malipo kwa hakika utalipwa mbinguni. Tunachopata hapa ni kwamba tukifanya jambo ili kutegemea heshima na kusifiwa ni kwamba tunakuwa tumepoteza tuzo letu huko mbinguni badala yake tufanye yote kwa unyenyekevu kwa waliowanyonge katika jamii, tutapokea tuzo letu huko mbinguni. Katika maisha yetu ya kila siku kawaida kuna vita kati ya maringo na unyenyekevu. Tukiacha maringo yetu yakikuwa tutaanza kutafuta heshima na kama tutaacha unye nyekevu ukue tutaanza kuwa wadogo na wenye upole na upendo kwa wote. Yesu leo ametushauri leo tuwe wanyenyekevu, ni juu yetu kukubali au kukataa na kuendeleea kuwa kama mafariso ambao waliendela mpaka kumua Yesu. Sala: Bwana, nifanye mpole na mnyenyekevu wa moyo kama wewe. Amina.

MASOMO YA MISA, Dominika ya 22 ya Mwaka C wa kanisa. 28/8/2016

Dominika ya 22 ya Mwaka
SOMO LA 1
Ybs 3:17-20, 28-29

       Mwanangu, wakati wa kufanikiwa uendelee katika unyenyekevu; hivyo utapendwa kuliko mwenye ukarimu. Kadiri ulivyo mkuu uzidi kujinyenyekesha, nawe utapata kibali machoni pa Bwana; kwa maana rehema zake Bwana zi kuu, na siri yake ni kwa wanyenyekevu. Msiba wa mwenye kiburi hauleti kupona, Mche wa uovu umepandika ndani yake. Moyo wa busara utatambua mithali, Na sikio sikivu ni tamaa ya mtaalamu.

WIMBO WA KATIKATI
Zab 68:3-6, 9-10
Wenye haki hufurahi, Na kuushangilia uso wa Mungu, Naam, hupiga kelele kwa furaha. Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake, Furahini katika Bwana, shangilieni mbele zake. (K)

Ee Mungu, Kwa wema wako uliwahifadhi walioonewa. Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane, Mungu katika kao lake takatifu. Mungu huwakalisha wapweke nyumbani; Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa; (K)

Ee Mungu, Kwa wema wako uliwahifadhi walioonewa. Ee Mungu, ulinyesha mvua ya neema; Urithi wako ulipochoka uliutia nguvu. Kabila yako ilifanya kao lake huko; Ee Mungu, kwa wema wako uliwaruzuku walioonewa. (K)

Ee Mungu, Kwa wema wako uliwahifadhi walioonewa.

SOMO LA 2
Ebr 12:18-19, 22-24

     Hamkufikilia mlima uwezao kuguswa, uliowaka moto, wala wingu jeusi, na giza, na tufani, na mlio wa baragumu na sauti ya maneno; ambayo wale walioisikia walisihi wasiambiwe neno lo lote lingine; Bali ninyi mmeufikilia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi, mkutano mkuu na kanisa la wazaliwa wa kwanza walioandikwa mbinguni, na Mungu mwamuzi wa watu wote, na roho za watu wenye haki waliokamilika, na Yesu mjumbe wa agano jipya.

SHANGILIO Mt 11:25
Aleluya, aleluya Ninashukuru Baba, Bwana wa mbingu na nchi, Kwa kuwa mambo haya uliwaficha wenye hekima na akili, Ukiwafunulia watoto wachanga. Aleluya

SOMO LA INJILI
Lk 14:1, 7-14
Yesu alipoingia ndani ya nyumba ya mtu mmoja miongoni mwa wakuu wa Mafarisayo siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia. Akawaambia mfano wale walioalikwa, alipoona jinsi walivyochagua viti vya mbele; akisema, Ukialikwa na mtu arusini, usiketi katika kiti cha mbele; isiwe kwamba amealikwa mtu mwenye kustahiwa kuliko wewe, akaja yule aliyewaalika wewe na yeye, na kukuambia, Mpishe huyu! Ndipo utakapoanza kwa haya kushika mahali pa nyuma. Bali ukialikwa, nenda ukaketi mahali pa nyuma, ili ajapo yule aliyekualika akuambie, Rafiki yangu, njoo huku mbele zaidi; ndipo utakapokuwa na utukufu mbele ya wote walioketi pamoja nawe. Kwa maana kila ajikwezaye atadhiliwa, naye ajidhiliye atakwezwa. Akamwambia na yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu, nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.

Saturday, 27 August 2016

MASOMO YA MISA JUMAMOSI,27/8/2016.

Sikukuu ya Mt. Monika
SOMO LA 1
1 Kor 1:26-31

       Ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.

WIMBO WA KATIKATI Zab 33:12-13, 18-21
Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao, Watu aliowachagua kuwa urithi wake. Toka mbinguni Bwana huchungulia, Huwatazama wanadamu wote pia. (K)

Heri taifa ambalo Bwana aliowachagua kuwa urithi wake. Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao, Wazingojeao fadhili zake. Yeye huwaponya nafsi zao na mauti, Na kuwahuisha wakati wa njaa. (K)

Heri taifa ambalo Bwana aliowachagua kuwa urithi wake. Nafsi zetu zinamngoja Bwana; Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu. Maana mioyo yetu itamfurahia, Kwa kuwa tumelitumainia jina lake takatifu. (K)

Heri taifa ambalo Bwana aliowachagua kuwa urithi wake.

SHANGILIO Yn 13:34
Aleluya, aleluya Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Aleluya

SOMO LA INJILI Mt 25:14-30
     Yesu aliwaeleza wanafunzi wake mfano huu: mtu aliyetaka kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake. Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri. Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano. Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida. Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake. Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao. Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida. Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida. Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako. Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya; basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako. Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya; basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake. Basi, mnyang'anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi. Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa. Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Friday, 26 August 2016

TAFAKRI YA MASOMO YA MISA IJUMAA,26/8/2016.

TAFAKARI
Ijumaa, Agosti 26, 2016,
Juma la 21 la Mwaka
1Kor 1:17-25; Zab 32: 1-2, 4-5, 10-11; Mt 25: 1-13

‘MJINGA’ KWA AJILI YA KRISTO?

         “Mungu ndio, Yesu ndio, Kanisa hapana!”. Namna hii ya kufikiri imezoeleka sana kati ya wengi. Je, sisi ni mmoja wao kati ya hawa “wengi”? Je kuna wakati tunajisikia mafundisho ya kanisa ni “yakizamani, yamepitwa na wakati, yasiofikirika na hivyo hayafai kuyaishi”? Na pia hayaendani na zama zetu za sayansi ya hali ya juu? Na hasa kuhusu, maadili na mambo ya maisha ya familia? Je, inawezekana kuwa Wakristo wazuri wanaoenda kanisani kila mara na bado kubaki bila kusumbuliwa na kufuata “majibu ya haraka yanayoonekana” ambayo “wenye hekima na akili” wa ulimwengu huu wanayotoa, wakati mafundisho ya Kanisa yanoonekana kupishana na mambo hayo? Mafundisho ya Kanisa yanaweza kuonekana kuwa “Msalaba”- lakini hii ni kwasababu hayajajengwa katika “sayansi ya mwanadamu au hekima ya mwanadamu”, bali katika maisha ya Kristo, msulubiwa. Mt. Paulo anatuambia wazi. “ujumbe juu ya Msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu” (1Kor 1: 18). Ni ukuweli usiopingika kwamba, Kanisa linaoongozwa na Roho Mtakatifu, anayetufundisha kila kitu, nakutukumbusha yote aliyofundisha Kristo na kusema kwetu kama alivyotuahidi mwenyewe. (Yn 14: 26). Je, inawezekana kwamba, “wanasayansi na wanafalsafa, watu mashuhuri na wanaojiona wenye akili sana- wanao tetea mawazo yao kwa kutoa hitimisho ya vitu vinavyoonekana –ambavyo kanisa linaona kwamba sio sahihi- kwamba wana akili na hekima zaidi kuliko Mungu aliyewaumba? “Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu.”(1 Kor 1: 25). Kufuata anachosema Mama Kanisa huenda kikaonekana upumbavu katika kiwango cha ulimwengu, hii ni kwasababu Mama kanisa anafundisha kuendana na utashi wa Kristo aliyefanya jambo lilionekana kuwa la aibu kwa kufa msalabani ili kutukomboa sisi, wadhambi. Pengine kwako kuungama unaona ni upumbavu au jambo la aibu! Ujue kuungama ni kwaajili ya ukombozi wa roho yako. Sisi tuwe kama Kristo, tukubali kuonekana kuwa wajinga wa ulimwengu huu, kwakufuata mafundisho ya Kristo aliyoyasimika katika Kanisa lake. Sala: Baba, tupe neema tuwe na utashi kama wa Kristo. Amina

MASOMO YA MISA IJUMAA YA 21 YA MWAKA. 26/8/2016

Ijumaa ya 21 ya Mwaka SOMO LA 1
1 Kor 1:17-25

        Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika. Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa. Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa. Kwa sababu Wayahudi wanataka ishara, na Wayunani wanatafuta hekima; bali sisi tunamhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upuzi; bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu. Kwa sababu upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.

WIMBO WA KATIKATI Zab 33:1-2, 4-5, 10-11
Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo. Mshukuruni Bwana kwa kinubi, Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa. (K)

Bwana anajaza nchi na fadhili zake. Kwa kuwa neno la Bwana lina adili, Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu. Huzipenda haki na hukumu, Nchi imejaa fadhili za Bwana. (K)

Bwana anajaza nchi na fadhili zake. Bwana huyabatilisha mashauri ya mataifa, Huyatangua makusudi ya watu. Shauri la Bwana lasimama milele, Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi. (K)

Bwana anajaza nchi na fadhili zake.

SHANGILIO Lk 21:36
        Aleluya, aleluya Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu. Aleluya

SOMO LA INJILI Mt 25:1-13
    Yesu aliwaambia wafuasi wake: Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu, na watano wenye busara. Wale waliokuwa wapumbavu walizitwaa taa zao, wasitwae na mafuta pamoja nao; bali wale wenye busara walitwaa mafuta katika vyombo vyao pamoja na taa zao. Hata bwana arusi alipokawia, wote wakasinzia wakalala usingizi. Lakini usiku wa manane, pakawa na kelele, Haya, bwana arusi; tokeni mwende kumlaki. Mara wakaondoka wanawali wale wote, wakazitengeneza taa zao. Wale wapumbavu wakawaambia wenye busara, Tupeni mafuta yenu kidogo; maana taa zetu zinazimika. Lakini wale wenye busara wakawajibu, wakisema, Sivyo; hayatatutosha sisi na ninyi; afadhali shikeni njia mwende kwa wauzao, mkajinunulie. Na hao walipokuwa wakienda kununua, bwana arusi akaja, nao waliokuwa tayari wakaingia pamoja naye arusini; mlango ukafungwa. Halafu wakaja na wale wanawali wengine, wakasema, Bwana, Bwana, utufungulie. Akajibu akasema, Amin, nawaambia, siwajui ninyi. Basi kesheni, kwa sababu hamwijui siku wala saa.

Thursday, 25 August 2016

TAFAKARI YA MASOMO YA MISA ALHAMISI,AGOSTI 25,2016

TAFAKARI
Alhamisi, Agosti 25, 2016, Juma la 21 la Mwaka 1Kor 1:1-9; Zab 144:2-7; Mt 24:42-51

    KUWA TAYARI !
        Injili ya leo inatangaza kuja sio kwa tufani bali ukombozi. Inatangaza kuja kwa Ufalme wa Mungu. Na hapo hapo tunaambiwa kwamba hatujui siku wala saa itakapokuja na kuja kwake kutakuwa kama ujio wa mwizi. Njia na silaha kubwa ya mwizi ni kuja kwakustukiza. Kuja kwa Ufalme wa Mungu hakutakuwa na kengele za tahadhari. Kuna silaha moja tuu ambayo tunaweza kuiandaa kwaujio wa ufalme wa Mungu nayo ni – kuandaa maisha yetu. Mungu ametupa sisi wanadamu uhuru wakuchagua. Kila mtu anauwezo wakuchagua jema na kutenda mema nakuishi vizuri na hapo ufalme wa Mungu ujapo atakuwa amejiandaa au mtu anauwezo wakuchagua kutenda dhambi na Mungu haingilii uhuru wake, lakini Mungu ameweka wazi njia yake kwamba kuchagua uovu sio kadiri ya sheria yake. Tuombee neema ya Mungu ili tuweze kutumia uhuru wetu vizuri tuchague kutenda mema kila wakati na tuwasaidie wengine waweze kuchagua kutenda mema ili ufalme wa Mungu ujapo kwa mara ya pili utukute tumejiandaa kila wakati. Tuna mengi sana ya kutufundisha sisi, kila mara tunawaona vijana wadogo wanapoteza maisha wakiwa na umri mdogo kabisa, pengine kwa ajali au kwa magonjwa, tunajiuliza hivi walijua kwamba Mungu angewachukua wakiwa wadogo namna hii? Tunajiuliza hivi walikuwa wamejiandaa? Sio kazi yetu kuhukumu nakujua kuhusu wema wao lakini tunachojifuza ni kwamba siku ya mwisho ya mwanadamu hapa duniani ni Mungu mwenyewe anayepanga, lililo bora tena sana ni kuwa tayari kwa ujio wa Mungu muda wowote ule. Tukiishi kwa matumaini yetu yakiwa ndani ya Kristo, siku hiyo itakuwa ya furaha kwetu na hatutaishi kwa woga. Hofu inakuja kwasababu ya dhambi, lakini tukijipatanisha na Kristo kila mara matumaini yetu kwake ni makubwa na furaha yetu ya kuungana naye itakuwa kubwa zaidi. Tuwasaidie ndugu zetu wote wamrudie Kristo, tukitambua kuwa hata jani la mwisho kabisa kwenye mti ni sehemu ya mti. Mkristo au ndugu unayemuona mdhambi sana bado ni sehemu ya mwili wa Kristo. Tuwasaidie ndugu zetu kwa kuwatia moyo ili wawe karibu zaidi na Kristo ili siku yake itakapokuja tuweze kupokea neema na kumlaki Kristo. Ni furaha yetu wote kwa pamoja kuuona uso wa Mungu. Sala: Bwana, kwakupokea sakramenti kila wakati, kwanjia ya sala zangu na ndugu zangu, kwa kutembea katika mwanga wa neno lako, naomba niwe tayari daima kukupokea wewe. Amina.

MASOMO YA MISA ALHAMISI 25 2016

Alhamisi ya 21 ya Mwaka
SOMO LA 1
1 Kor 1:1-9

Paulo, aliyeitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu. Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo. Namshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu mliyopewa katika Kristo Yesu; kwa kuwa katika kila jambo mlitajirika katika yeye, katika maneno yote, na maarifa yote; kama ushuhuda wa Kristo ulivyothibitika kwenu; hata hamkupungukiwa na karama yo yote, mkikutazamia sana kufunuliwa kwake Bwana wetu Yesu Kristo; ambaye atawathibitisha hata mwisho, ili msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. Mungu ni mwaminifu ambaye mliitwa na yeye mwingie katika ushirika wa Mwanawe, Yesu Kristo Bwana wetu.

WIMBO WA KATIKATI Zab 145:2-7
    Kila siku nitakuhimidi, Nitalisifu jina lako milele na milele. Bwana ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, Wala ukuu wake hautambulikani. (K)

Ee Bwana, nitalihimidi jina lako milele na milele. Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako, Kitayatangaza matendo yako makuu. Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, Na matendo yako yote ya ajabu. (K)

Ee Bwana, nitalihimidi jina lako milele na milele. Watu watayataja matendo yako ya kutisha, Nami nitausimulia ukuu wako. Watalihubiri kumbukumbu la wema wako mkuu. Wataiimba haki yako. (K)

Ee Bwana, nitalihimidi jina lako milele na milele.

SHANGILIO Mt 24:42a, 44
Aleluya, aleluya Kesheni basi; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja. Aleluya

SOMO LA INJILI Mt 24:42-51
    Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Kesheni basi; kwa maana hamjui ni siku ipi atakayokuja Bwana wenu. Lakini fahamuni neno hili; kama mwenye nyumba angaliijua ile zamu mwivi atakayokuja, angalikesha, wala asingaliiacha nyumba yake kuvunjwa. Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyodhani Mwana wa Adamu yuaja. Ni nani basi yule mtumwa mwaminifu mwenye akili, ambaye bwana wake alimweka juu ya nyumba yake, awape watu chakula kwa wakati wake? Heri mtumwa yule, ambaye bwana wake ajapo atamkuta akifanya hivyo. Amin, nawaambieni, atamweka juu ya vitu vyake vyote. Lakini mtumwa yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia; akaanza kuwapiga wajoli wake, na kula na kunywa pamoja na walevi; bwana wake mtumwa huyo atakuja siku asiyodhani, na saa asiyojua, atamkata vipande viwili, na kumwekea fungu lake pamoja na wanafiki; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Wednesday, 24 August 2016

TAFAKARI YA MASOMO YA MISA LEO 24/8/2016

TAFAKARI Jumatano, Agosti 24, 2016, Juma la 21 la mwaka
Sikukuu ya Mt. Bartolomayo, Mtume Ufu 21: 9-14; Zab 144: 10-13, 17-18; Yn 1: 45-51

NJOO NA UONE: KUKUTANA NA YESU!
       Leo kanisa linafurahia kwa kuadhimisha sikukuu ya Mt. Bartolomayo Mtume. Anajulikana pia kwa jina la Nathanael na alikuwa mmoja wao wa mitume kumi na mbili wa Bwana wetu Yesu Kristo. Alikuwa ni mmisionari akiwa na Philipo na Tomas. Inasemakana alihubiri Injili katika maeneo haya ya, Armenia, India, Persia na Phrygia. Katika Injili ya leo tunamuona jinsi Philipo anampeleka Nathanaeli kwa Yesu ili aweze naye kukutana na Masiha. Kwahiyo Philipo anatoa ushuhuda ghani kwa Nathanaeli? Badala ya kuchukua muda wakubishana na rafiki yake, Philipo anaamua kuchukua uamuzi wa hekima wa “Kumpele na kumuona” Yesu kwa macho yake mwenyewe, Yesu huyu anayezungumzwa na watu. Philipo alitambua kwamba kukutana na Yesu mtu binafsi inaweza ikabadilisha maisha ya mtu kabisa. Wakati watu wanapopokea neno la Kristo, na wanapoona upendo wake katika matendo, Yesu mwenyewe, kwa njia ya Roho Mtakatifu, anagusa mioyo yao na kufungua mioyo na akili zao kwenye ufunuo wa Mungu. Wakati Philipo alivyomleta Nathanaeli kwa Yesu, Yesu alifanya kitu ambacho ni Mungu mwenyewe tu anaweza kufanya! Alifungua moyo wa Nathanaeli na mawazo yake ya ndani ukaweza kutamani ufunuo wa Mungu. Nathanaeli aliyatambua maandiko, alisoma Torati na Manabii na alikuwa akitazamia ahadi ya Mungu itimizwe kwaajili ya watu wa Israeli. Nathanaeli alikuwa ni mtu anayemtafuta Mungu kutoka moyoni. Hakufikiri tu kukua katika akili ya elimu ya Mungu bali alifikiri kuhusu jinsi ya kuungana na Mungu pia. Ndio maana alikuwa tayari kukutana na Yesu, na kuona kama huyu mtu anayefanya miujiza kutoka Galilaya kuwa anaweza kuwa Masiha anayesubiriwa. Mungu ameweka katika kila moyo wa Mwanadamu hamu na tamaa ya kumtafuta, yeye aliyetuumba wote kwa upendo wake. Sisi pia tunaalikwa tuweze kuwa na uhusiano mzuri na Yesu binafsi. Pia tujitahidi kuwaelekeza wengine waweze kukutana na Yesu. Tusiwe chanzo cha kuwapeleka wenzetu kwenye uovu unaowaweka mbali na Yesu. Tuwafariji wale waliokata tamaa, tuwapeleke kwa Yesu kwenye matumaini ya kweli, tuwapeleke wakakutane na Mungu ili aweze kugusa maisha yao. Sisi wenyewe tuimarishe uhusiano wetu na Mungu ili kwa uthabiti wetu tuweze kuwavuta wengine kwa Yesu. Tujaribu kuwa na Yesu daima katika maisha yetu ya kila siku na tuwe mashaidi wake wa kweli. Sala: Bwana Yesu, jifunue mwenyewe ndani yangu ili niweze kuwa nawe daima katika maisha yangu. Amina.

MASOMO YA MISA LEO 24/8/2016

Kumbukumbu ya Mt. Bartholomeo
SOMO LA 1 Ufu 21:9-14

     Malaika alinijia akanena nami, akisema, Njoo huku, nami nitakuonyesha yule Bibi-arusi, mke wa Mwana-Kondoo. Akanichukua katika Roho mpaka mlima mkubwa, mrefu, akanionyesha ule mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mwenyezi Mungu; wenye utukufu wa Mungu, na mwangaza wake ulikuwa mfano wa kito chenye thamani nyingi kama kito cha yaspi, safi kama bilauri; ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu, wenye milango kumi na miwili, na katika ile milango malaika kumi na wawili; na majina yameandikwa ambayo ni majina ya kabila kumi na mbili za Waisraeli. Upande wa mashariki milango mitatu; na upande wa kaskazini milango mitatu; na upande wa kusini milango mitatu; na upande wa magharibi milango mitatu. Na ukuta wa mji ulikuwa na misingi kumi na miwili, na katika ile misingi majina kumi na mawili ya wale mitume kumi na wawili wa Mwana-Kondoo.

WIMBO WA KATIKATI Zab 145:10-13, 17-18
Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru, Na wacha Mungu wako watakuhimidi. Wataunena utukufu wa ufalme wako, Na kuuhadithia uweza wako. (K)

Wacha Mungu wataunena utukufu wa ufalme wako, Ee Bwana. Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari ya ufalme wake. Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote, Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote. (K)

Wacha Mungu wataunena utukufu wa ufalme wako, Ee Bwana. Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote, Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote. Bwana yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu. (K)

Wacha Mungu wataunena utukufu wa ufalme wako, Ee Bwana.

SHANGILIO Yn 1:49b
Aleluya, aleluya Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli. Aleluya

SOMO LA INJILI Yn 1:45-51
      Filipo alimwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na manabii, Yesu, mwana wa Yusufu, mtu wa Nazareti. Nathanaeli akamwambia, Laweza neno jema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone. Basi Yesu akamwona Nathanaeli anakuja kwake, akanena habari zake, Tazama, Mwisraeli kweli kweli, hamna hila ndani yake. Nathanaeli akamwambia, Umepataje kunitambua? Yesu akajibu, akamwambia, Kabla Filipo hajakuita, ulipokuwapo chini ya mtini nilikuona. Nathanaeli akamjibu, Rabi, wewe u Mwana wa Mungu, ndiwe Mfalme wa Israeli. Yesu akajibu, akamwambia, Kwa sababu nilikuambia, Nilikuona chini ya mtini, waamini? Utaona mambo makubwa kuliko haya. Akamwambia, Amin, amin, nawaambia, Mtaziona mbingu zimefunguka na malaika wa Mungu wakikwea na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.

Tuesday, 23 August 2016

Music notes (nota za muziki).

  Katika kuhakikisha kwamba uinjili shaji unakua tumekuletea nata zanyimbo za kikatoliki hizihapa Bofya hapa                                                                                                                       https://drive.google.com/folderview?id=0BzEHH5E3LxEhd211LTM1Qkt5MnM

Monday, 22 August 2016

Tafakari ya neno la mungu leo 23/8/2016

TAFAKARI
Jumanne, Agosti 23, 2016, Juma la 21 la Mwaka
2 Thes 2:1-3, 14-17; Zab 95:10-13; Mt 23:23-26

UHURU KWA KUACHANA NA UNAFIKI!
Ipo wazi kutoka katika maisha ya Yesu na mifano kwamba hakulaumu yeyote; alilaumu dhambi yenyewe si mdhambi. Hata leo katika Injili ya leo, analaumu njia ambayo Mafarisayo na Walimu wa sheria, wametumia dini na matendo ya dini vibaya kwaajili ya manufaa ya wao binafsi. Yesu analaumu unafiki wa watu. Katika uhalisia unafiki maana yake ni mtu kujifanya kuwa na kitu ambacho katika hali ya kweli hana. Kusema uongo na unafiki huwa vinaenda sambamba. Yesu hapendi maisha ya namna hii. Katika hali ya maisha ya unafiki maana halisi ya dini inapotea, na hapo dini inakuwa inafanywa kwa njia zisizo eleweka. Yesu aliweza kutambua mara moja waliokuwa waaminifu na wale walikuwa wanafiki. Kwahiyo alilaumu unafiki wao kwa ujasiri kabisa. Wanafiki walijaribu kwa njia zote ili kupata wafuasi. Walipopata mfuasi, maisha yake yanafanywa kuwa maguu kwa kumtambulishia sheria nyingi, mila nyingi za njee na mambo mengi yakufanya. Kwahiyo Watu walipoteza muelekeo kamili wa yaliokuwa ya muhimu katika dini, na kushikilia mambo yasio ya lazima. Mambo yote, mila na tamaduni za kidini yanapaswa yatuongoze kwa Mungu. Ni njia zinazo tumika katika dini ili kutuleta karibu na Mungu. Ni njia zinazotumika katika dini ili kutuleta karibu zaidi na Mungu, na mambo hayo sio mwisho wa kila kitu, mwisho unapaswa kuwa Mungu. Yesu analaumu aina zote za unafiki zinazomfanya Mungu awe mbali nasi katika matendo yetu ya Imani (dini). Sala: Mungu Baba yetu wa Mbinguni tuweke huru kutoka katika tabia ya unafiki wetu katika kumfuata Mwanao. Amina.

Masomo/neno la mungu leo 23/8/2016

Jumanne ya 21 ya Mwaka SOMO LA 1 2 The 2: 1-3, 14-17

Tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake, kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitushwe, kwa roho, wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo. Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yo yote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu; akafunuliwa yule mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu; aliyowaitia ninyi kwa injili yetu, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo. Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu. Na Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu, aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema, awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema.

WIMBO WA KATIKATI Zab 96:10-13

Semeni katika mataifa, Bwana ametamalaki; Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike, Atawahukumu watu kwa adili. (K)

Bwana anakuja aihukumu nchi Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie, Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Mashamba na yashangilie, na vyote vilivyomo, Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha; (K)

Bwana anakuja aihukumu nchi Mbele za Bwana, kwa maana anakuja, Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa uaminifu wake. K)

Bwana anakuja aihukumu nchi

SHANGILIO Ebr 4:12
Aleluya, aleluya Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Aleluya

SOMO LA INJILI Mt 23:23-26
     Yesu alisema,Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka za mnanaa na bizari na jira, lakini mmeacha mambo makuu ya sheria, yaani, adili, na rehema, na imani; hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache. Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia. Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang'anyi na kutokuwa na kiasi. Ewe Farisayo kipofu, safisha kwanza ndani ya kikombe, ili nje yake nayo ipate kuwa safi.

Saturday, 20 August 2016

Masomo/neno la mumgu leo 20/8/2016

Jumamosi ya 20 ya Mwaka SOMO LA 1 Eze 43:1-7

Bwana alinileta mpaka langoni, yaani, lango lile lielekealo upande wa mashariki; na tazama, huo utukufu wa Mungu wa Israeli ulitokea kwa njia ya mashariki; na sauti yake ilikuwa kama mshindo wa maji mengi, nayo nchi iling'aa kwa utukufu wake. Na maono niliyoyaona yalikuwa kama maono niliyoyaona nilipokuja kuuharibu mji; nayo maono niliyoyaona yalikuwa kama maono niliyoyaona karibu na mto wa Kebari; nikaanguka kifudifudi. Na huo utukufu wa Bwana ukaingia ndani ya nyumba, kwa njia ya lango lile lielekealo upande wa mashariki. Kisha Roho ikaniinua, ikanichukua mpaka ua wa ndani; na tazama, utukufu wa Bwana uliijaza nyumba. Nikasikia sauti ya mmoja asemaye nami, itokayo katika nyumba hiyo; na mtu akasimama karibu nami. Akaniambia, Mwanadamu, hapa ni mahali pa kiti changu cha enzi, na mahali pa nyayo za miguu yangu, nitakapokaa kati ya wana wa Israeli milele; na nyumba ya Israeli hawatalinajisi jina langu takatifu tena, wao, wala wafalme wao, kwa mambo yao ya kikahaba, na kwa mizoga ya wafalme wao, katika mahali pao pa juu;

WIMBO WA KATIKATI Zab 85:8-13 Na nisikie atakavyosema Mungu Bwana, Maana atawaambia watu wake amani, Hakika wokovu wake u karibu na wamchao, Utukufu ukae katika nchi yetu. (K)

Utukufu wa Bwana ukae katika nchi yetu. Fadhili na kweli zimekutana, Haki na amani zimehusiana. Kweli imechipuka katika nchi, Haki imechungulia kutoka mbinguni. (K)

Utukufu wa Bwana ukae katika nchi yetu. Naam, Bwana atatoa kilicho chema, Na nchi yetu itatoa mazao yake. Haki itakwenda mbele zake, Nayo itazifanya hatua zake kuwa njia. (K)

Utukufu wa Bwana ukae katika nchi yetu.

SHANGILIO Mt 23:9b, 10b
Aleluya, aleluya Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni, kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo. Aleluya

SOMO LA INJILI Mt 23:1-12

Yesu aliwaambia makutano na wanafunzi wake,akasema, Waandishi na Mafarisayo wameketi katika kiti cha Musa; basi, yo yote watakayowaambia, myashike na kuyatenda; lakini kwa mfano wa matendo yao, msitende; maana wao hunena lakini hawatendi. Wao hufunga mizigo mizito na kuwatwika watu mabegani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao. Tena matendo yao yote huyatenda ili kutazamwa na watu; kwa kuwa hupanua hirizi zao, huongeza matamvua yao; hupenda viti vya mbele katika karamu, na kuketi mbele katika masinagogi, na kusalimiwa masokoni, na kuitwa na watu, Rabi. Bali ninyi msiitwe Rabi, maana mwalimu wenu ni mmoja, nanyi nyote ni ndugu. Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. Wala msiitwe viongozi; maana kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo. Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. Na ye yote atakayejikweza, atadhiliwa; na ye yote atakayejidhili, atakwezwa.

Friday, 19 August 2016

Tafakari ya masomo ya leo 19/8/2016

TAFAKARI
Ijumaa, Agosti 19, 2016, Juma la 20 la Mwaka Eze 37: 1-14; Zab 107: 2-9; Mt 22: 34-40

AMRI KUU
        Injili ya leo inatualika tutafakari njia iliyo kuu ambayo kila mfuasi wa Kristo inapaswa kuwa msingi wake. Upendo kwa Mungu na upendo kwa jirani. Kwanza kabisa upendo kwa Mungu ni kushuhudia na kukiri upendo wa Mungu kwetu sisi. Sisi ni dhaifu sana na tunashindwa kumpenda Mungu kama inavyotupasa. Lakini ndani ya Yesu tunahisi upendo wa Mungu kwetu. Kwahiyo, kuhisi upendo wa Mungu, licha ya upweke wa mtu mwenyewe inamfanya mtu ampende Mungu kama matokeo ya kuhisi upendo huo. Huu ndio mwanzo wa kumpenda Mungu. Wakati mtoto anavyohisi upendo wa Mama, hafanyi kitu kinyume na Mama. Hii ndio maana ya kumpenda Mungu. Tukihisi upendo wa Mungu hatutafanya mambo kinyume na Mungu, hatujiingiza kwenye dhambi, bali tutafanya yote yenye kumpendeza. Inamfurahisha Mungu tukiwapenda wengine. Kwahiyo, wakati mtu anampenda Mungu, anaanza kumpenda jirani pia. Je, ni muda ghani upendo wangu juu ya jirani unapokuwa kamilifu? Tunapowapenda ndugu zetu tunakuwa tunatamani na wao kila wakati wawe washiriki kwenye uzima wa milele. Tunakuwa tunatamani na kuomba kwamba waishi maisha yao yote katika neema. Kwahiyo wanakuwa washiriki wa uzima wa milele zawadi tuliopewa na Yesu. Tunakumbuka alichosema Yesu ‘mlicho watendea wadogo hawa mme mtendea yeye’. Tutoke njee ya nafsi zetu, tuweze kukutana na watu waliowahitaji, tuwasaidie kadiri ya uwezo wetu. Huu ndio upendo kwa jirani zetu. Sala: Bwana nisaidiye niweze kukupenda wewe ili niweze kuwapenda wengine. Amina

Neno/masomo ya leo 19/8/2016

Ijumaa ya 20 ya Mwaka SOMO LA 1 Eze 37:1-14

Mkono wa Bwana ulikuwa juu yangu, naye akanichukua nje katika roho ya Bwana, akaniweka chini, katikati ya bonde; nalo limejaa mifupa; akanipitisha karibu nayo pande zote; na tazama, palikuwa na mifupa mingi katika ule uwanda! Nayo, tazama, ilikuwa mikavu sana. Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe. Akaniambia tena, Toa unabii juu ya mifupa hii, uiambie, Enyi mifupa mikavu, lisikieni neno la Bwana. Bwana MUNGU aiambia mifupa hii maneno haya; Tazama, nitatia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi. Nami nitatia mishipa juu yenu, nami nitaleta nyama iwe juu yenu, na kuwafunika ngozi, na kutia pumzi ndani yenu, nanyi mtaishi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana. Basi nikatoa unabii kama nilivyoamriwa; hata nilipokuwa nikitoa unabii, palikuwa na mshindo mkuu; na tazama, tetemeko la nchi, na ile mifupa ikasogeleana, mfupa kwa mfupa mwenziwe. Nikatazama, kumbe! Kulikuwa na mishipa juu yake, nyama ikatokea juu yake, ngozi ikaifunika juu yake; lakini haikuwamo pumzi ndani yake. Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapuzie hawa waliouawa, wapate kuishi. Basi nikatabiri kama alivyoniamuru; pumzi ikawaingia, wakaishi, wakasimama kwa miguu yao, jeshi kubwa mno. Kisha akaniambia, Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli; tazama, wao husema, Mifupa yetu imekauka, matumaini yetu yametupotea; tumekatiliwa mbali kabisa. Basi tabiri, uwaambie, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitafunua makaburi yenu, na kuwapandisha kutoka katika makaburi yenu, enyi watu wangu, nami nitawaingizeni katika nchi ya Israeli. Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, nitakapoyafunua makaburi yenu, na kuwatoa ninyi katika makaburi yenu, enyi watu wangu. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, nanyi mtaishi, nami nitawawekeni katika nchi yenu, nanyi mtajua ya kuwa mimi, Bwana, nimesema hayo, na kuyatimiza, asema Bwana.

WIMBO WA KATIKATI Zab 107:2-9

Na waseme hivi waliokombolewa na Bwana, Wale aliowakomboa na mkono wa mtesi. Akawakusanya kutoka nchi zote, Mashariki na magharibi, kaskazini na kusini. (K)

Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni Mwema. Kwa maana fadhili zake ni za milele. Walitanga-tanga jangwani katika njia ya nyika; Hawakuona mji wa kukaa. Waliona njaa, waliona na kiu, Nafsi yao ilikuwa ikizimia ndani yao. (K)

Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni Mwema. Kwa maana fadhili zake ni za milele. Wakamlilia Bwana katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao. Akawaongoza kwa njia ya kunyoka, Wapate kwenda mpaka mji wa kukaa. (K)

Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni Mwema. Kwa maana fadhili zake ni za milele. Na wamshukuru Bwana, kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu. Maana hushibisha nafsi yenye shauku, Na nafsi yenye njaa huijaza mema. (K)

Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni Mwema. Kwa maana fadhili zake ni za milele.

SHANGILIO Zab 25:4b, 5a
Aleluya, aleluya Unifundishe mapito yako, Uniongoze katika kweli yako, Aleluya

SOMO LA INJILI Mt 22:34-40
   Mafarisayo waliposikia ya kwamba amewafumba kinywa wale Masadukayo, walifanya shauri pamoja. Mmoja wao, mwana-sheria, akamwuliza, akimjaribu; Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii.

Thursday, 18 August 2016

Tafakari katika sara

Hati mbali mbali za sala na tafakari zina patikana hapa.   Bofya hapa https://drive.google.com/folderview?id=0BzEHH5E3LxEhSDN6ZzRBUmFmWU0

Masomo ya leo 18/8/2016 hapa

Alhamisi ya 20 ya Mwaka SOMO LA 1 Eze 36:23-28

     Neno la Bwana lilinijia hivi: nitalitakasa jina langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, asema Bwana MUNGU, nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao. Maana nitawatwaa kati ya mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe. Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.

WIMBO WA KATIKATI Zab 51:10-13, 16-17
   Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu Usinitenge na uso wako, Wala roho yako mtakatifu usiniondolee. (K) Nitawanyunyizia maji safi; Nanyi mtakuwa safi, nitawatakaseni na uchafu wenu wote. Unirudishie furaha ya wokovu wako; Unitegemeze kwa roho ya wepesi. Nitawafundisha wakosaji njia zako, Na wenye dhambi watarejea kwako. (K) Nitawanyunyizia maji safi; Nanyi mtakuwa safi, nitawatakaseni na uchafu wenu wote. Maana hupendezwi na dhabihu, au ningeitoa, Wewe huridhii sadaka ya kuteketezwa. Dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika; Moyo uliovunjika na kupondeka, Ee Mungu, hutaudharau. (K) Nitawanyunyizia maji safi; Nanyi mtakuwa safi, nitawatakaseni na uchafu wenu wote. SHANGILIO Zab 95:8 Aleluya, aleluya Ikiwa leo mwaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu; Aleluya

SOMO LA INJILI Mt 22:1-14
    Yesu aliwaambia makuhani na makutano kwa mithali, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwanawe arusi. Akawatuma watumwa wake wawaite walioalikwa kuja arusini; nao wakakataa kuja. Akatuma tena watu kwa wengine, akisema, Waambieni wale walioalikwa, Tazameni, nimeandaa karamu yangu; ng'ombe zangu na vinono vimekwisha kuchinjwa, na vyote vimekuwa tayari, njoni arusini. Lakini hawakujali, wakaenda zao, mmoja shambani kwake, mmoja kwenye biashara yake; nao waliosalia wakawakamata watumwa wake, wakawatenda jeuri, na kuwaua. Basi yule mfalme akaghadhibika; akapeleka majeshi yake, akawaangamiza wauaji wale, akauteketeza mji wao. Kisha akawaambia watumwa wake, Arusi i tayari, lakini wale walioalikwa hawakustahili. Basi enendeni hata njia panda za barabara, na wote mwaonao waiteni arusini. Watumwa wale wakatoka wakaenda njia kuu, wakakusanya wote waliowaona, waovu kwa wema; arusi ikajaa wageni. Lakini alipoingia yule mfalme ili kuwatazama wageni wake, akaona mle mtu mmoja asiyevaa vazi la arusi.Akamwambia, Rafiki, uliingiaje humu nawe huna vazi la arusi? Naye akatekewa. Mfalme akawaambia watumishi, Mfungeni mikono na miguu, mchukueni mkamtupe katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno. Kwa maana waitwao ni wengi, bali wateule ni wachache.

Tuesday, 16 August 2016

Tafakari ya somo/neno la mungu leo 16/8/2016

TAFAKARI
Jumanne, Agosti 16, 2016,
Juma la 20 la Mwaka Eze 28:1-10; Kumb 32:26-28, 30, 35-36; Mt 19:23- 30

KUACHA YOTE NA KUMFUATA KRISTO!
Kilele cha mwisho kabisa cha mwanadamu ni kujua, kupenda, kumtumikia Mungu na kufurahia maisha ya milele pamoja naye daima. Na Mungu anapenda kutushirikisha uzima huu wa milele. Ni zawadi kutoka kwa Mungu. Hatuwezi kupata uzima huu kwa nguvu za kibinadamu. Tungeachiwa sisi tu, ingekuwa vigumu sana kwetu sisi kuupata. Lakini kwa neema ya Mungu yote yanawezekana. Lakini, mali na utajiri vinaonekana viashiria vinavyo hatarisha kutokuupata ufalme huu wa milele. Katika ulimwengu huu wa sasa wenye mambo mengi inakuwa vigumu kwa wengine kukwepa hili. Ni jambo kubwa la kweli “kuacha yote” lakini kubwa zaidi “kumfuata Yesu”. Kumfuata Yesu ni kazi yetu. Katika hili linabeba ukombozi wa mwanadamu, lakini hatuwezi kumfuata Kristo kama hatutaacha yote yanayotufunga tushindwe kumfuata. Nabii Ezekiel katika somo la kwanza anatoa angalisho kwa mji wa Tiro na viongozi wake waliopata mafanikio makubwa na nguvu. Wameweka ulinzi wao na Imani yao katika utajiri na mali ambavyo vimegeuka kuwa miungu yao. Lakini Petro anasema, “tumeacha yote” sio tuu vitu vya ulimwengu, lakini pia tamaa zinazopendwa na mioyo yetu. Wanaobaki wakiwa wameshikilia baadhi ya vitu inakuwa hawajaacha yote. Kwanini anatoa ujumbe mkali namna hiyo kwa matajiri? Kwanini Yesu anaongea sana kuhusu mali? Ni kwasababu mali inaweza kutufanya tusiwe huru au kutupa uhuru wa ouongo. Wengine wameshindwa kumfuata Yesu kwasababu ina maana ya kuacha baadhi ya uhusiano, na wengine kama yule tajiri, ni kwasababu watapoteza nafasi yao ya heshima au njia zao za kupata mali. Wewe je? Sala: Bwana, naomba nikufanye wewe wa kwanza katika maisha yangu na nikuchague wewe kwa uhuru kamili hata kama kukufuata inagarimu.

Somo/neno la mungu leo 16/8/2016

Jumanne ya 20 ya Mwaka SOMO LA 1 Eze 28:1-10
Neno la Bwana likanijia tena, kusema, Mwanadamu, mwambie mkuu wa Tiro, Bwana Mungu asema hivi; Kwa kuwa moyo wako umeinuka, nawe umesema, Mimi ni Mungu, nami nimeketi katika kiti cha Mungu, kati ya bahari; lakini u mwanadamu wala si Mungu, ujapokuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu. Tazama, una hekima kuliko Danieli; hapana neno la siri watu wawezalo kukuficha; kwa hekima yako na kwa fahamu zako umejipatia utajiri, nawe umepata dhahabu na fedha katika hazina zako; kwa hekima yako nyingi, na kwa biashara yako, umeongeza utajiri wako, na moyo wako umeinuka kwa sababu ya utajiri wako; basi, kwa hiyo, Bwana Mungu asema hivi; Kwa kuwa umeweka moyo wako kama moyo wa Mungu; basi, tazama, nitaleta wageni juu yako, watu wa mataifa wenye kutisha; nao watafuta panga zao juu ya uzuri wa hekima yako, nao watautia uchafu mwangaza wako. Watakushusha hata shimoni; nawe utakufa kifo chao waliouawa kati ya bahari. Je! Utazidi kusema mbele yake huyo akuuaye, Mimi ni Mungu? Lakini u mwanadamu, wala si Mungu, mkononi mwake akutiaye jeraha. Utakufa kifo cha hao wasiotahiriwa, kwa mikono ya wageni; kwa maana mimi nimenena neno hili, asema Bwana Mungu.

WIMBO WA KATIKATI Kumb 32:26-28,30,35-36
Nalisema, Ningewatawanyia mbali, Ningekomesha kumbukumbu lao kati ya wanadamu; Isipokuwa naliogopa makamio ya adui, Adui zao wasije wakafikiri uongo, (K) Naua Mimi, nahuisha Mimi. Wasije wakasema, Mkono wetu umetukuka, Wala Bwana hakuyafanya haya yote. Maana hawa ni taifa wasio shauri, Wala fahamu hamna ndani yao. (K) Naua Mimi, nahuisha Mimi. Mmoja angefukuzaje watu elfu, Wawili wangekimbizaje elfu kumi, Kama Mwamba wao asingaliwauza, Kama Bwana asingaliwatoa? (K) Naua Mimi, nahuisha Mimi. Maana siku ya msiba wao imekaribia, Na mambo yatakayowapata yatafanya haraka. Kwa kuwa Bwana atawaamua watu wake, Atawahurumia watumwa wake, (K) Naua Mimi, nahuisha Mimi.

SHANGILIO 2Kor 8:9
Aleluya, aleluya Bwana wetu Yesu Kristo alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake. Aleluya

SOMO LA INJILI Mt 19:23-30
Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Amin, nawaambieni, ya kwamba itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. Nawaambia tena, Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu ya sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu. Wanafunzi waliposikia, walishangaa mno, wakisema, Ni nani basi awezaye kuokoka? Yesu akawakazia macho, akawaambia, Kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana. Ndipo Petro akajibu, akamwambia, Tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata; tutapata nini basi? Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu kabila kumi na mbili za Israeli. Na kila mtu aliyeacha nyumba, au ndugu wa kiume au wa kike, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia, na kuurithi uzima wa milele. Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.

karibu tujifunze kuhusu imani katoriki

                   KARIBU SANA
        HII NIBLOG INAYO JUMUISHA WATU WAIMANI YEYOTE TUKIJIFUNZA KWA PAMOJA KUHUSU IMANI ZENU TUKITOANA DUKUDUKU NA MASHAKA KATIKA IMANI KUMBE UNAKALIBISHWA SANA TUJIJENGE KIIMANI.
           
                   Unaruhusiwa kuuliza swali lolote kuhusu imani zetu na utapatiwa majibu mazuri hivyo basi tunakukaribisha sana. Pia utapata nafasi ya kujifunza zaidi kwa sala na tafakari zuri.
                        Angalisho:
          Huwenda blog hii ikaelemea zaidi katika imani katoliki lakini MTU imani yeyote anaruhusiwa kuuliza ama kuchangia/kuelimisha katika blog hii.
                                           Karibuni sana

NYIMBO ZA DOMINIKA YA 29 YA MWAKA- C WA KANISA.

Nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka C Karibu kwa ajili ya nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka "C" Mwanzo: Ee Bwana Nimekuita  ...