Saturday, 1 October 2016

TAFAKARI: 1/10/2016 Jumamosi ya 26 ya Mwaka-C " Kumbukumbu ya Mt. Theresia wa Mtoto Yesu, Bikira na Mwalimu wa Kanisa. "


TAFAKARI

        Jumamosi, Oktoba 1, 2016. Juma la 26 la Mwaka

        Kumbukumbu ya Mt. Theresia wa Mtoto Yesu, Bikira na Mwalimu wa Kanisa.

         Ayu 42: 1-3, 5-6, 12-17 Zab 118: 66, 71, 75, 91, 125, 130 Lk 10: 17-24

        MUNGU WA VITU VIDOGO!
        Somo la kwanza leo linatueleza ni kwa jinsi ghani Mungu alivyo zibariki siku za mwisho za Ayubu zaidi hata ya zile za mwanzo. Na Ayubu aliamini kwamba Mungu anaweza kutenda na kutoa vitu vyote kwa mwanadamu na kwamba hakuna lengo lake linalo weza kuzuiwa na kitu chochote au nguvu za muovu.
      Wale sabini wanavyorudi wakielezea ushindi, kuna aina tatu za furaha katika Injili ya leo:
          1) Furaha ya huduma
          2) Furaha ya ukombozi
          3) Furaha ya mamlaka. 
        Yesu aliwapa nguvu na uwezo wakuponya na kutoa pepo wabaya, na kuhubiri Neno, na hatimaye walishinda. Kila ushindi ni muhimu kwa Yesu, haijalishi ni namna ghani waweza kuonekana machoni petu. Lakini, Wafuasi hawapaswi kufurahi kwasababu pepo wabaya wana watii na kuwatoka watu bali kwasababu majina yao yameandikwa mbinguni. Furaha au ushindi waweza kumfanya mtu kuishia kujivuna. Muujiza mkubwa kuliko wote ni ukombozi wa roho iliyo potea. Furaha yetu haipatikani katika huduma, na wala si katika ukombozi, bali ni katika kujikabidhi kwenye mapenzi ya Baba Yetu wa Mbinguni, kwawasababu hii ndio sababu ya huduma na ukombozi.
         Leo Kanisa lina adhimisha kumbukumbu ya Mt. Teresa wa Mtoto Yesu, anaye elezewa kama mtakatifu mkuu wa kipindi cha sasa, huyu Bikira mdogo anaelezewa pia kama msimamizi wa utume.
       Huu ndio mchango wake na msukumu wa maisha yeke kwa ufupi. Kanisa likimtangaza kama ‘Mwalimu wa Kanisa’ linatambua mchango wake, tena mafundisho yake ya kawaida, ‘Njia ndogo”, kinachojulikana kama ‘Roho ya utoto’.
            Mafundisho yake yamejikita katika mafundisho na msingi wa maneno ya Yesu “Aliye mdogo na aje kwangu”. Na hivyo, Mt. Teresa hakuelewa tu siri hii kubwa katika unyenyekevu, kumwamini Mungu na kuwa wazi kwake, kujiamini na bila kumwacha, bali pia alitumia ngazi hii kukwea katika mlima wa ukamilifu na utakatifu na kuungana na Mungu.
        Teresa anatukumbusha kwamba, kiini cha ujumbe wa Mkristo ni kwamba, Mungu ni upendo, yeye ni Baba wa huruma, na anajitoa mwenyewe kwa wale wote walio maskini wa roho kwa ajili ya neno la Mungu. Ni nani kati yetu anaye shindwa kumtukuza Mungu kwa njia hii rahisi ya kumfurahisha Mungu na kukuwa katika utakatifu?
       Sala: Ee Bwana, tuongoze kwenye njia ya udogo na unyofu wa Moyo. Amina

Copyright © 2016 by shajara  and published MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
      see: imani-katoliki.blogspot.com

MASOMO YA MISA, 1/10/2016. " Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. "


KUMBUKUMBU YA MT. THERESIA WA MTOTO YESU
        
        SOMO LA 1
     Ayu. 42:1 – 3, 5 – 6, 12 – 17

               Ayubu alimjibu Bwana na kusema, najua ya kuwa waweza kufanya mambo yote, nay a kuwa makusudi yako hayawezi kuzuilika. Ni nani huyu afichaye mashauri bila maarifa? Kwa maana, nimesema maneno nisiyoyafahamu, mambo ya ajabu, ya kunishinda mimi, nisiyoyajua. Nilikuwa nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio; bali sasa jicho langu linakuona. Kwa sababu hiyo najichukia nafsi yangu, na kutubu katika mavumbi na majivu. Basi hivyo Bwana akaubarikia huo mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake; naye alikuwa na kondoo kumi nan ne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng’ombe elfu, na punda wake elfu. Tena laikuwa na wana waume saba, nab inti watatu. Akamwita huyo wa kwanza jina lake Yemima; na wa pili akamwita jina lake Kesia; na wa tatu akamwita jina lake Keren-hapuhu. Katika nchi hiyo yote hawakuwapo wanawake waliokuwa wazuri kama hao wana wa Ayubu; na baba yao akawapa urithi kati ya ndugu zao wana waume. Kisha baada ya mambo hayo Ayubu akaishi miaka mia na arobaini, naye akawaona wanawe, na wana wa wanawe, hata vizazi vine. Basi Ayubu akafa, mzee sana mwenye kujawa na siku.
          
     WIMBO WA KATIKATI
    Zab. 119:66, 71, 75, 91, 125, 130

         (1).   Unifundishe akili na maarifa, Maana nimeyaamini maagizo yako. Ilikuwa vema kwangu kuwa naliteswa, Nipate kujifunza mari zako.
                    (K) Umwangazie mtumishi wako uso wako, Ee Bwana.
        (2).    Najua ya kuwa hukumu zako ni za haki, Ee Bwana, na kwa uaminifu umenitesa. Kwa hukumu zako vimesimama imara hata leo, Maana vitu vyote ni watumishi wako.
                    (K) Umwangazie mtumishi wako uso wako, Ee Bwana.
       (3).    Mimi ni mtumishi wako, unifahamishe, Nipate kuzijua shuhuda zako. Kufananisha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga.
           (K) Umwangazie mtumishi wako uso wako, Ee Bwana.

       SHANGILIO
          Yn. 15:15
          Aleluya, aleluya, Bwana anasema: Siwaiti tena watumwa, lakini ninyi nimewaita rafiki, kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu, nimewaarifu. Aleluya.
   
      SOMO LA INJILI
      Lk. 10:17-24

            Wale sabini waliporudi kwa furaha, wakisema, Bwana, hata pepo wanatutii kwa jina lako. Akawaambia, Nilimwona Shetani, akianguka kutoka mbinguni kama umeme. Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru. Lakini, msifurahi kwa vile pepo wanavyowatii; bali furahini kwa sababu majina yenu yameandikwa mbinguni. Saa ile ile alishangilia kwa Roho Mtakatifu, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa mambo haya umewaficha wenye hekima na akili; umewafunulia watoto wachanga; Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyokupendeza. Akasema, Nimekabidhiwa vyote na Baba yangu, wala hakuna amjuaye Mwana ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba ila Mwana, na yeyote ambaye Mwana apenda kumfunulia. Akawageukia wanafunzi wake, akasema nao kwa faragha, Heri macho yaonayo mnayoyaona ninyi. Kwa kuwa nawaambia ya kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuyaona mnayoyaona ninyi wasiyaone; na kuyasikia mnayoyasikia ninyi wasiyasikie.

Copyright © 2016 by shajara and published MAMBO YAHUSUYO IMANI BLOG
      see: imani-katoliki.blogspot.com

NYIMBO ZA DOMINIKA YA 29 YA MWAKA- C WA KANISA.

Nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka C Karibu kwa ajili ya nyimbo za Jumapili ya 29 Mwaka "C" Mwanzo: Ee Bwana Nimekuita  ...